Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Voda mnakula MB za internet fasta mno kuliko mitandao mingine , punguzeni bas
 
Mimi hutumia sana simu yangu...kwa kufanya huduma za money transaction japo sina voda shop; nilikuwa na enjoy sana ile huduma ya kupiga namba moja kwa reduced price. Niliiona kama zawadi yangu ya kutumia huduma zao. Naomba irudishwe

Asante
 
Nikama miezi miwili sasa mawasiliano nishida huku wilaya ya korogwe vijijini kama vile kwasunga,kiloza mgobe hadi Korogwe,ukiongea namtu mnaweza msielewane kunakuwa na mikwaluzo,lakini ukipigiwa na mtu wa mtandao mwingine mnaongea vizuri bila matatizo

Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza, tunashughulia tatizo hili kuhakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora. Tunaomba uvumilivu wako.
Voda mnakula MB za internet fasta mno kuliko mitandao mingine , punguzeni bas

Mkuu uishaji wa kifurushi unatokana na matumizi, kadri intaneti inavyokuwa kasi ndivyo ambavyo kifurushi kinakwenda.
 
Hivi kwa nini mna sponsor blog zenye matusi za watanzania?

Kwa kweli kwa jina la vodacom/vodafone duniani mnatia aibu sana ku sponsor blog ya mwanamke anayetukana watanzania wenzake na kusisisitiza uadui na mabaya hata kuhatarisha maisha ya watu kwa kutoa dtails zao private.

inabidi mauahane na haya ma blog esp ya huyo mdada, najua mnaijua ila mmefumbia macho. soon itabidi na magazeti yaongelee hii issue na wateja wenu waone hata wale wateja wanaotaka jiunga nanyi wawakimbie maana ni hatari sana kwa mnalofanya.

eti mnasponsor matusi, ugomvi, bullying, detah threats, mengi tu
Ahsante kwa ushauri ndugu mteja. Shukrani
 
Voda nyinyi ni wezi sana na laiti kama hao wahudumu wenu nilioongea nao tar 22 na 23 wangekuwa karibu ningewazaba vibao wanavunga wanajua kumbe hawajui yaani nyie ni wezi nyie ni maescrow kabisa mnatuibia hela zetu makusudi tukiwapigia na vielelezo kamili mnabisha tu acheni hizo hata Sisi tuna uchungu wa pesa zetu Sisi siyo mitaji yenu wala mashamba yenu mmenibore sana kwa majibu yenu na soon nitawahama hata of a zenu wizi tu
Mtu nmenunua Salio mpesa kwa confirmation BK81GN266 halafu mnanijibu eti hiyo hela imeletwa tar 14 cha kushangaza napiga tena naambiwa hiyo hela haitambuliki kabisa tena kwa kukwepa maswali kanakimbilia kuniambia eti Vodacom inakutakia siku njema then kanakata Simu acheni ufisadi mmenibore mtandao siyo wenu tu hata ttcl zantel Tigo na airtel tutahamia na kama ni hivi basi punde mtaanza hata kutuibia kwenye account zetu za mpesa.
Mmeniudhi sana sina hamu na nyie na siweki Salio tena mpaka nitakapovunja line yenu.....0763994423 ndo namba yangu.
Habari Yohana, tunawasiliana nawe kwa msaada zaidi. Pole sana
 
Vodacom mimi nawapa BIG up sana...
sasa hivi tuna wapata vizuri Arusha hadi Ngorongoro hadi kule pande la serengeti
M - pesa naona pia iko poa labda matatizo ya kawaida ya mtandao
Nina zaidi ya miaka kumi kwenye huduma/namba yangu ya vodakom

LANGU MOJA TU
Rudisheni huduma ya kupiga namba moja kwa bei poa ili tuweze kudumisha ndoa tukiwa safarini hata kama mshiko umepungua
mfano shs 5000 kupiga kwa mwezi namba moja ya voda (muda wowote ila kupunguza jam...labda muweke jumla ya dkk zote ziwe lisaa moja kwa siku). mnaweza kukaza masharti kidogo; mfano mtu anaweza kubadili mara mbili tu kwa mwezi
Mbona naona kama italipa tu
 
Nyie Vodacom kuna tetesi kwamba mdada anaeitwa Violet Njau au Viola amejiua baada ya kutukanwa kwenye blog ambayo mnaisponsor. Kwahiyo mnaendorse cyberbullying?? Vodacom kifo cha huyu dada na damu yake kiko mikononi mwenu kwa sababu nyie ndo the only sponsor wa that blog. Kwanini hamuangalii makampuni makubwa duniani. Mfano tiger woods alipata scandal makampuni yote yakamdrop nyie mnaendelea kusponsor a website inayotukana na kudhalilisha wateja wenu wenyewe. Kwa hiyo inamaanisha mmeyaendorse yale matusi sio...kama mna maadili basi onesheni maadili yenu
 
Tunahitaji kuwekewa mnara was Vodacom ka hama Mpunze Wateja ni wengi
 
Kitu kingine kinacho niuzi unapopiga simu huduma kwa wateja basi utawekewa matangazo karibia saa nzima wewe nikusikiliza matangazo masikio yanauma wao namatangazo litatoka hiri wataweka hiri basi hasira hadiunaongea namuhudumu masikio yameshakua mazito ,kwani kunahaja gani yamatangazo yote hayo?! Kama hudama zenu nzuri wateja tupo wengi tu lakini kama mbovu hats kama kila tunapo kanyaga mungeweka matangazo hamutupati boresheni hudumazenu lakini kwa hili lamatangazo binafsi munanikera sana munaniumiza masikio
 
Tarehe 14 January nilijiunga na kifurushi cha unlimited internet cha mwezi mzima(20000), ambacho kinatakiwa kuisha February 13.

Pamoja na kifurushi hiko, pia huwa naweka kifurushi kingine weekly Kwa ajili ya airtime ambacho pia kina mb chache za internet, ambazo huwa zikiisha naendelea kuwa na internet ile ya unlimited niliyoweka swali mpaka muda wake utakapoisha.

Jana sasa, naamka asubui nataka nifanye shughuli zangu online nashangaa internet hakuna! Huku nikijiamini kwa kuwa najua internet yangu, bado sana mpaka February nikajua labda matatizo yao YA kiufundi ambayo pia huwa hawa compensate ata SIKU moja kwa usumbufu.

Baada ya kuona hali haibadiliki nikaamua kupiga customer service, jamaa mmoja akaniambia ishu NI kwamba eti kwasababu niliweka kifurushi kingine kikaingilia kile kilichokuwepo kwahiyo kilivoisha basi kikaondoka na kile cha mwezi cha internet, na akasema habari ndo hiyo hana msaada!

Nikamueleza kuwa huwa nafanya hivo mara nyingi lakini haijawahi kutokea kifurushi changu cha internet nilicholipia 20000 kikafutika wakati muda wake bado.

Sasa nikaona hii ni too much na no wizi, Maana kuna wakati niliwahi kuweka internet ya wiki unlimited ikasepa after 2 days. Sasa nimeona huu wizi na dhuluma nikiikalia tu, watakuwa wanatuibia KILA siku, ma milioni ya watu.

Nipo kwenye early stages za kuwa sue, na kama kuna yeyote aliyedhulumiwa kwa ataivo hii ya kidigitali naomba tuwasiliane tuunde jeshi kuwakabili hawa wezi, watufidie, haiwezekani wachukue pesa bila Huduma staili.
 
Back
Top Bottom