Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Binafsi nawashangaa watu wengi hapa
Badala ya kutoa mawazo yao na matatizo yao ili yaonekane kama yana uhusiano yaweze kushuhulikiwa wao ni kudandia tu hoja za wengine na kushabikia bila hata kutoa hoja yenye mashiko..

Kwa upande wa simu hapa sitachangia ila kwa Internet mpo juu sana. Nimejaribu wengi ila niligundua wababaishaji sana..unaweza kupewa MB nyingi ila hazifungui kitu. Vodacom hata U tube natumia kwa kwenda mbele
ila mngetuboreshea tupate MB nyingi zaidi kwa bei ile ile hasa wanunuzi wa wiki/mwezi ...naona zinaisha mapema sana



sijaona kama vodacom..wanajisifia ila wapo slow kama konokono.
'
nikarudi..wengi waongo
 
Nyie@Vodacom Tanzania

1. Muanzishe kifurushi cha wiki cha University offer (CHEKA YA CHUO) kama ndg zenu Tigo na Airtel. Sie wanachuo hatuna hela za kuunga kila siku; sehemu ni vyuo vikuu vyote , Tanzania.

2. KUHAMISHA SALIO: Tatzo liko kwenye kuhamisha salio kutoka mtu mmoja voda kwenda mwingine voda. Mnakata tozo (ada) na hela (salio) then salio halimfikii mlengwa, huku mmeisha lamba hela. Bolesheni system ya Me2u. Tz nzima.
3. M-PESA: Kwasababu product ya M-PESA, ni leading Mobile Money Transfer Agent in Tanzania. Nawaomba muanzishe No (For calling, free of charge) special kwa ajili ya huduma ya Miamala iliyo kosewa (kutuma/kupokea) pesa. Huwa mna ile 100, iko too busy sana. Wajanja wa hapa town ukikosea tu dk1 washa kuliza na line-tupa kule.

4. Muwe na Customer Service Officers walio somea IT jameni, achaneni na warembo wanao paka lipstick na rangi hadi kwenye meno, huku wakiwa wamesoma, Bachelor of Arts in Education (Geography&Kiswahili).Hawajui kitu wala kutatua tatizo hawawezi. Nafahamu hapa ni vigumu kunielewa kwani ni vitowewo vyenu-ila jaribuni!!

5.SWITCHING MOBILE PHONE OFF WHILE SERVING: Ni vyema mkawa na muda wa kuchat na Simu ofisini either Tea Break or Lunch time (uwepo lakini) kwani nyie mnatuhamasisha Tujismartphonishe, na kuzima simu wahudumiapo. HIZI SIMU ZA DIGITAL NI HATARI KWA MUDA WA KAZI. Na hawa warembo-nilio wataja hapo(4), ni mabingwa wa kupiga picha na kupost nguo zake zote za kabatini, huwa wanatumia masaa 2 kati 8 ya kazi (Working hours ) kuchati. Either Akiwa anapost picha au ana Tag picha au ana LIKE au ana COMMENT au akiwa ana SEMA Ahsante kama kasifiwa, hadi amalize ndio akusikilize. Hii pia itawasaidia BENKI mbalimbali nchi Tz, kwa ufanisi bora.

Feedback kwangu ni jambo nalo lipa kipaumbele, kila la kheri ktk kuijenga Tz nyenye ufanisi.

Ni hayo tu mura, mjipange!!!
 
Voda ukicheka kwa sh 1750 unapewa dakika 56 wakati Airtel ukinunua kifurushi cha sh 1500 unapewa dakika 145. Uongozi wa voda unaweza kutoa maelezo, au tuhamie airtel wote?
 
Mimi nimekuwa nakatwa mb bila matumizi yoyote nimeripoti malamiko hadi nimechoka nimeenda ktk ofisi zenu za mlimani hakuna msaada wowote
 
Voda ukicheka kwa sh 1750 unapewa dakika 56 wakati Airtel ukinunua kifurushi cha sh 1500 unapewa dakika 145. Uongozi wa voda unaweza kutoa maelezo, au tuhamie airtel wote?

Ndugu mteja tutafanyia kazi ni kweli inaonesha tunawapunja kuliko wengine. Ushauri: MAUMIVU YAKIZIDI MUONE DAKTARI
 
I have about three concerns.. ya kwanza ni menu yenu(ukipiga *149*01#), jaribuni kui review naona kama haiko vizuri uki compare na ya airtel.. yenu ina repetition nyingi.. second khs hivi vifurushi vya bila kikomo, hii sio bila kikomo ukitumia MB kadhaa unaambiwa kimeisha na hali hizo siku hazijaisha utaendelea kuchajiwa kwenye normal account which is not fair na wakati mnasema bila kikomo like you make us stupid, la tatu I appreciate you for the very best network.
 
Vodacom acheni WIZI hivi inakuwaje mtu anajiunga na kifurushi halafu mnakata hela lakini akiongea nyie mnamkata kama vile hajajiunga.Yaani umeshakata hela yangu halafu kuongea mpaka wewe uniruhusu.Huo ni wizi mkubwa sana mnaotufanyia wateja!
 
Mkiendelea na huo upuuzi wenu sisi tunajiunga na kifurushi na mnatukata hela halafu nikongea mnakata hela as if sikujiunga haki ya nani nachoma line zenu za voda zilizo katika familia yangu.haiwezekani nmejiunga na nmepata sms yenu na salio mmekomba nlivyotaka kuongea baada ya dk.kama kumi mnaniambia sina salio.imenitokea karibu mara nne.acheni upuuzi.
 
Vifushi vya masaa 24 voda kwenda voda
Tsh 150=10 sms

Tsh 500= dk 15+250sms+8mb

Tsh 650= dk 30+300sms+8mb

Tsh 1000= dk 50+300sms+8mb

vodacom kwenda mitandao mingine

Tsh 150= sms 10

Tsh 499= dk 7+300sms+8mb

Tsh 649= dk13 +450sms+8mb

Tsh 999= dk 20+1000sms+8mb

vifurushi vya wiki voda kwenda voda

Tsh 1050= sms 70

Tsh 2000= dk 60+150sms+60mb

Tsh 2800= dk 85+700sms+60mb

Tsh 4000= dk 140+1750 sms+60mb

Tsh 7000= dk 250+2100sms+60mb

Tsh 10000= dk 360+2500sms+60mb

vodacom mitandao yote kwa wiki

Tsh 1050= sms 70

Tsh 1999= dk 29+500sms+6omb

Tsh 3999= dk 49+500sms+60mb

Tsh 4999= dk 91+1000sms+60mb

Tsh 9999= dk 190+1000sms+60mb

HIVI KWELI NYIE Vodacom Tanzania MMEKAA MKIWA NA AKILI ZENU TIMAMU MKAPANGA NA KUJA NA VIWANGO VYA KIJINGA KAMA HIVI..?
 
Last edited by a moderator:

Hawawezi kuwa serious huu ni upuuzi baada ya kuana hi sikuamini nikaangalia nilichokuta 😱
 
Last edited by a moderator:
Hawawezi kuwa serious huu ni upuuzi baada ya kuana hi sikuamini nikaangalia nilichokuta 😱

Mkuu mie niko voda toka day one.. Na sio muumini wa kubadilisha namba but kama ikitokea hawatabilisha hii nitawahama rasmi na sim card yao nitawarudishia ili wakamuuzie mtu mwingine namba yangu.. Huu ni ujinga completely.. Uhuni uliopitiliza na ukahaba toka kwa kampuni kubwa kama ya Vodacom..
 

yaani leo nilikuwa nataka kujiunga nilipokutana na hiyo menu mpya i was like wtfk!!!! haki yanani nikahamia airtel hawa voda wehu washalewa sifa so wanafanya wanavyojisikia
 

upuuzi wa hali ya juu, hata sijui nini wanafikiria
 
Last edited by a moderator:

Nimetoka kuwapigia simu kuulizia kama ndio vifurushi vipya hivyo au vipi; jibu nililipewa na customer care ni eti labda itakuwa nimekosea kusoma...wakati kumbe ndio hali halisi. NIMEKUJA KUGUNDUA HAWA JAMAA NI MAJAMBAZI
 
Last edited by a moderator:
Inamaana hata customer care wa voda hawajui mabadiliko haya ya vifurushi vya cheka au wanafanya makusudi??. Nataka majibu haraka nyie Majambazi mnaowaibia wananchi maskini kila kukicha bila hata haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…