Viwango mlivyoweka Vodacom kwa sasa ni vya kipuuzi kuliko kawaida. Mb 60 nazifanyia nini? Acheni kutuibia. Hii ni namna ya kurudisha faida kwenye promotion mnayoendelea nayo, we are not that stupid. Rudisheni viwango vya zamani otherwise you will loose. Kwa sasa Airtel are far better than you. Acheni upuuzi.!!
Hawa Jamaa ni Washenzi Sana.
Hivi inawezekanaje 500 na 1000 Upate kiwango sawa cha MB???.
Tumeshahama ila airtel nako kuna mabadiliko karibu tutarudia masanduku yetu ya posta
Waambie na wao waame, na kabla ya kuhama, waambie wakope buku kila mmoja wao.Naumia nitapoteza friends kwa kuhama ila kwa hali hii inabidi tu nihamie airtel maana hii haikubaliki kabisa ,mb 8 dah
Una point mkuu. Huo huenda ndio ukweli wenyewe
Tumeshahama ila airtel nako kuna mabadiliko karibu tutarudia masanduku yetu ya posta
Nafikiri afisa masoko wao hajui anachokifanya.
Ndugu mteja,
Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?
Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.
Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:
- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.
Karibu
Vodacom Tanzania
Njooni huku mjibu tuhuma za wizi huu mlioanza mbona mnakaa kimya acheni masikhara watu wana hasira na huduma zenu
Hawawezi kuja huku, wakiweka vipromo vyao ni kelele dunia nzima itajua lakini kwenye wizi kimya kabisa
Waambie na wao waame, na kabla ya kuhama, waambie wakope buku kila mmoja wao.
TTCL amkeni hawa wahuni wanatumaliza jamani