Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Eti wamenitumia message wamenianzishia huduma ya games ambayo sio bure. kama sitaki nitume neno UNSUB kwenye namba 15362. Mimi sijawahi kuomba hiyo huduma isitoshe ku UNSUB sio bure hiyo message unalipia. Nina hakika watumiaji wengi sio makini wasipo UNSUB wanatozwa kwa huduma hujahitaji. Hebu fikiri licha ya wizi wa mchana usumbufu gani huu. Isitoshe wanageuza simu yako ubao wa matangazo ya biashara bila ruksa yako au kukupatia chochote. Ukikaa kidogo unasikia 'kabang' unadhani ujumbe wako ukiangalia unakuta tangazo la vodacom. Mamlaka inayohusika hebu tuokoeni na huu ubeberu wa makampuni ya simu.
Mwenyewe najaribu ku UNSUB kama walivyoelekeza ujumbe hauendi sijui hii ndio nini. Zipo taarifa wenyewe kwa wenyewe wanahisa wa voda wameibiana mabilioni ya dola ndio sisi wateja tutasalimika?nielekeze jinsi ya kujitoa mwenzangu,hata mie yamenikuta
Vodacom wanatuibia sana,
mara nyingi ukiweka salio ili ujiunge utakuta mtandao unakujibu kuwa salio lako halitoshi kujiunga na huduma hii. Mfano juzi na jana nikuwa nikiweka tsh 1100 ili kujiunga data bila kikomo ya 1000 sasa wanakuambia salio halitoshi, hata ukiongeza sh.1300 ili upate data ya 1000 bado unaambiwa salio halitoshi. Hadi uweke sh1400 au zaidi ndio utaunganishwa data ya 1000, cha ajabu hiyo 400 inayobaki hutaiona tena, huu si wizi jamani?
halafu hata hawarespond!! sasa kwanini wamekuja hapa JF? Wanatudharau hawa tuhamasishane kuwahama...Wamenchefua sa hiv yaaan wameniharbia cku mfyuuu
Ndugu mteja,
Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?
Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.
Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:
- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.
Karibu
Vodacom Tanzania
halafu hata hawarespond!! sasa kwanini wamekuja hapa JF? Wanatudharau hawa tuhamasishane kuwahama...