Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania naombeni mnisaidie kurejesha pesa yangu ambayo nilikua nalipa Zuku last month nikilipa kwa 220220 badala ya account yangu. Naombeni msaada maana zuku wanasema hio pesa iko kwenu ni Tsh.32,000 ili niingize kwenye malipo ya mwezi huu. Shukrani
 
Last edited by a moderator:
Eti wamenitumia message wamenianzishia huduma ya games ambayo sio bure. kama sitaki nitume neno UNSUB kwenye namba 15362.

Mimi sijawahi kuomba hiyo huduma isitoshe ku UNSUB sio bure hiyo message unalipia. Nina hakika watumiaji wengi sio makini wasipo UNSUB wanatozwa kwa huduma hujahitaji. Hebu fikiri licha ya wizi wa mchana usumbufu gani huu.

Isitoshe wanageuza simu yako ubao wa matangazo ya biashara bila ruksa yako au kukupatia chochote. Ukikaa kidogo unasikia 'kabang' unadhani ujumbe wako ukiangalia unakuta tangazo la vodacom.

Mamlaka inayohusika hebu tuokoeni na huu ubeberu wa makampuni ya simu.
 
Eti wamenitumia message wamenianzishia huduma ya games ambayo sio bure. kama sitaki nitume neno UNSUB kwenye namba 15362. Mimi sijawahi kuomba hiyo huduma isitoshe ku UNSUB sio bure hiyo message unalipia. Nina hakika watumiaji wengi sio makini wasipo UNSUB wanatozwa kwa huduma hujahitaji. Hebu fikiri licha ya wizi wa mchana usumbufu gani huu. Isitoshe wanageuza simu yako ubao wa matangazo ya biashara bila ruksa yako au kukupatia chochote. Ukikaa kidogo unasikia 'kabang' unadhani ujumbe wako ukiangalia unakuta tangazo la vodacom. Mamlaka inayohusika hebu tuokoeni na huu ubeberu wa makampuni ya simu.


Vodacom imegeuka kijiwe cha madalali na MATAPELI!
 
nielekeze jinsi ya kujitoa mwenzangu,hata mie yamenikuta
Mwenyewe najaribu ku UNSUB kama walivyoelekeza ujumbe hauendi sijui hii ndio nini. Zipo taarifa wenyewe kwa wenyewe wanahisa wa voda wameibiana mabilioni ya dola ndio sisi wateja tutasalimika?
 
harafu wengine hatunaga tabia ya kusoma ma meseji itakuwa nimeli delete harafu wataendelea kunikata. Nikigundua wamenikata naachana nao kabisa nitawataarifu ndugu na jamaa namba yangu mpya.
 
sio vodacom tu hata mitandao Mingine wanaboa na vimeseji vyao vya kila mara ukiangalia salio, ukimaliza kupiga, basi ili mradi tu
 
Vodacom wanatuibia sana,
mara nyingi ukiweka salio ili ujiunge utakuta mtandao unakujibu kuwa salio lako halitoshi kujiunga na huduma hii. Mfano juzi na jana nikuwa nikiweka tsh 1100 ili kujiunga data bila kikomo ya 1000 sasa wanakuambia salio halitoshi, hata ukiongeza sh.1300 ili upate data ya 1000 bado unaambiwa salio halitoshi. Hadi uweke sh1400 au zaidi ndio utaunganishwa data ya 1000, cha ajabu hiyo 400 inayobaki hutaiona tena, huu si wizi jamani?

Wamenchefua sa hiv yaaan wameniharbia cku mfyuuu
 
Tafadhali naomba nirudishiwe pesa mlizikata tangia tarehe 30 mwezi wa nne za Jay milioni . Mimi sija wahi kujiunga na hiyo kitu. Nimeshangaa leo sina salio kwenye simu na jana nilijiunga na kifurushi cha week.
 
Mimi sina hamu nao kabisa na hasa matangazo yao na mambo ya katiba pendekezwa kila siku wanatuma while I am not interested na katiba pendekezwa! Usiombe wakakuibukia na matangazo ya katiba pendekezwa,inaingia message unadhani ni message ya maana unakumbana na katiba pendekezwa
 
Sasa kina Makamba na TCRA wamekaa kimya tu hawa jamaa wanazidi kutuibia,yani hamna company zenye afadhari kwenye simu.
ndio wanafanya tuhisi kuwa wanapewaga bahasha ndio maana hawafuatilii ata tukiibiwa.
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania

Kwa kipindi cha wiki moja sasa line ya vodacom sms haziendi (yaani ukituma sms inakupa jibu message not sent) lakini sms zinaingia kama kawaida. Hakuna mabadililiko yoyote niliyofanya kwenye simu na salio liko la kutosha. Msaada tafadhali. Natumia android
 
mimi kuna kitu huwa sikielewi. Unakuta umejiunga na kifurushi cha wiki au mwezi. Katikati humo unataka labda kufanya "sim banking". Unaweka elfu 1 au 2 halafu panatokea jambo lingine unasema hili swala la benki nitafanya baadae. Ukirudi hiyo baadae ambayo inaweza kuwa ni dk 5 au 10 unaambiwa muamala hauwezi kukamilika. Heee! eti salio huna? Sasa zinaendaga wapi??? Basi mwenzenu nikitaka kufanya kamuamala na benki kupitia simu nanunua kajero haraka haraka nafanya yangu haraka kama nakimbizwa kabla sijaambiwa muamala hauwezi kukamilika. Kuna mahali nakosea au na wengine yanawakuta?

Halafu huwa kuna message inakuja "mlio wako wa "kesho" umewekwa upya. Ndo nini? Wangu kivipi, toka lini? Uliwekwa mara ya kwanza lini?
 
Vodacom mnakera sana ktk bei za vifurushi vyenu angalieni mitandao mingine oni ongezeni Mb
 
Back
Top Bottom