Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Kumdaka boya kama huyo ni kitu kirahisi sana kama voda watakupa ushirikiano! waambie wakupe number za watu anaowasiliana nao mara kwa mara then wapigie hao watu kama watapatikana fanya juu chini ukutane nae halafu umwambie unashida nae akuelekeze kwake huyo jamaa uliemtumia pesa kimakosa! mbona utamdaka tu! au weka number yake hapa tumfume sasa hvi!
 
Sio polisie wetu wa kibongo, mana hapo wanawaza wao watafaidika na nni huku akiwaza kota anayoishi inataka kudondoka kule nyumbani
 

Sasa mkuu usidhani kila mtu yuko dar.
Unakuta mtu yupo mbali ambapo hata ukiambiwa ni fulani yupo sehemu fulani ila umbali wake ni mrefu hakuna jinsi nyingine zaidi ya kusamehe tu.
Fikiria unafunga safari toka lindi kumfuata mtu kigoma halafu huna uhakika wa kulipwa! au unafika unamkuta ni mwanafunzi wa kidato cha pili.
 
yani mda huo unaomba ushauri huku jamaa kasha itoa ni bora ungeongea na huduma kwa wateja
 
sasa ushauri wa nn wakati pesa imetolewa..polisi watakulia hela zaidi hawawezi kuganya kazi bure.potezea tu...
 
pole sana kwani hilo tatizo hata limeshanikuta nilikosea kutoa pesa zikaenda kwa mtu mwingine na yule mtu akawa ameshaenda kutoa ile pesa nikipiga cm voda wakanimambia niwe nawapigia cm kila mara huyu mtu akitumiwa pesa watanitumia mpaka leo sijafanikiwa kupata hizo pesa mpaka nimesahau.
 

Wacha uongo wewe. Hakuna mchagga anamrushia binti tena asiyemfahamu laki 5 labda Kyasaka anayetumia chagga land kama boya tu.
 
Hivi kwanini huduma sensitive kama ya kutuma fedha ambayo kuna uwezekeno mkubwa wa mtu kukosea namba wasingeweka double check ili kuhakikisha unayemtumia fedha ndio yeye! eg Wangeweka mtumaji lazima aingize namba ya anayemtumia na jina lake kamili (surname na first name) halafu kabla fedha hazijaenda system ina-check kuhakikisha number = = to the names ndio iruhusu kuhamisha! Unapokuwa designer wa application yoyote kitu cha kutilia umuhimu kabisa ni user's error and mistakes!
 

lakini kabla hujaweka pin (kwa tigo) na 1 kuhakiki (kwa Voda). system si huwa inaleta jina?
labda kama anatuma mtandao tofauti.
 
 
msaada wenu wadau,jamaa kashaitoa na voda wanasema hawana jinsi ya kufanya labda mpaka jamaa aweke pesa kwenye akaunti yake ndio wataikata. polisi nao wamesema watafuatlia ni siku ya nne sasa! jamaa anapatkana ila hapokei simu na akipokea haongei.

tuwekee hiyo namba tumtafute
 
lakini kabla hujaweka pin (kwa tigo) na 1 kuhakiki (kwa Voda). system si huwa inaleta jina?
labda kama anatuma mtandao tofauti.

Sawa mkuu. Mimi situmii hizi huduma ndio maana nimeshangaa inakuwaje error ya namna hiyo inatokea. Lakini kulingana na maelezo ya wengi ni kuwa bado ni watu wengi wanafanya makosa, which means designers wa hizo program inabidi warudi tena mezani waone namna ya ku-rectify hili tatizo
 
double cheki ipo,jamaa ni mzembe tu,maana huwa wanakuuliza uinataka kutuma pesa kwa fulani,wanakutajia jina then unaconfirm kwa kubonyeza namba moja,na kama umekosea unacancel kwa kubonyeza namba 2.
sasa huyu alikuuwa anatuma pesa huku amelala au?

Kulingana na maelezo ya thread za aina hii ni kuwa bado kuna watu wengi wanafanya makosa ya kutuma fedha kwa watu wasiotakiwa. Najua watanzania tuna tatizo kubwa kabisa la kutokuwa makini kwenye kuandika nk hivyo labda wangejaribu kuangalia njia nyingine ya kuepuka haya makosa.
 
tarehe 9.5.2015 nilinunua umeme lkn sikupata umeme mpaka leo. kila nikipiga custumer care naambiwa nisubiri saa 24 lakini mpaka leo sijarudishiwa pesa wala kupewa umeme. mnakera sana na mbaya zaidi hamtatui shida za wateja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…