KASHOROBANA
JF-Expert Member
- Jul 30, 2011
- 3,241
- 964
Sasa hats kama ni uchaguzi Msitunyanyase kwani mmeanza kupunguza MB kutoka MB200 kwa Tsh500 sasa mnatoa MB180 je tuamie wapi???
NAWE USIWE KAMA MTOTO MPUMBA.FU, IVI NI LAZIMA UWE NA MTANDAO WA VODACOM KT SIMU YAKO?? KIUKWELI NAKUFANANISHA NA MNYWA GONGO KWANI HATA KAMA GONGO ILO LINAMUUMIZA KIASI GANI BADO HACHOKI KWENDA KWA MUUZA GONGO NA KUINYWA TENA, Tia ADABU WEWE!!!!
1.Kifurushi cha internet Mb 200 cha tsh 500 sasa ni Mb 180 je mabadiliko haya yana gusa kifurushi cha bila kikomo siku cha 1000?
2. Kiuhalisia kuna kiwango cha mbs katika bila kikomo ya siku ya 1000 ila hamsemi. Je ni mb ngapi zimo humo kama ilikuwa ni gb1 kwa mabadiliko ya kifurushi cha internet ya 500 na huku kwenye bila kikomo siku 1000 hali ya mabadiliko ikoje?
Nilikuwa nasikia tu kwa wengine leo nimehakikisha kuwa hawa Voda kweli ni wezi. mimi ni mteja ninayetumia mtandao wa voda namba 0762749205,jana usiku saa nne nilinunua solio la sh.1000 kupitia m-pesa na kupata sms "BR04DY593 Imethibitishwa umenunua Tsh1,000 ya muda wa maongezi saa 10:02 PM Tarehe 11/7/15 Salio lako jipya la akaunti ya M-PESA ni Tsh19,670" kuonyesha kwamba nimepata salio hilo la sh 1000,na nikapata sms nyingine kutoka voda "Umepokea Tsh 1000.00. Salio lako jipya ni Tsh 1000.00. Kumb. 444323401339996668. Time: 7/11/2015 10:00:36 PM" hivyo nikajiunga na kifurushi cha siku internet bila kikomo na kupata ujumbe kua ombi langu linashughulikiwa lakini sikupata sms yoyote kunijulisha kuwa nimeunganshwa kwenye kifurushi hicho. nipoangalia salio la maongezi nikakuta zero ,ilipofika saa tano yaani saa moja baadae ndipo nikapata sms "Salio lako halitoshi kununua kifurushi cha Data.Tafadhali ongeza salio lako na kisha jaribu tena au nunua kifurushi kidogo cha data. Time: 7/11/2015 11:02:46 PM" siku yapili yake jumapili saa 1.30PM nikampigia mhudumu wa wateja na kunijibu kwa kwa maneno rahisi tu kuwa internet ni ghali sana na salio langu limeshatumika ingawa nilimuleza kuwa nilikuwa off-line imekuwaje salio litumike.lakini aling'ang'ania maeleo yake ya awali.Kuna wizi mkubwa kwa fedha za salio za wateja unaoendelea sasa hivi katika mtandao wa Vodacom.
Kwa vile hili si jungu bali ukweli nimisha report wizi huo katika kitengo cha malalamiko TCRA kwa hatua zaidi.
Nimeweka salio la Tsha 10,000 mchana wa leo kwa Mpesa ref Y23SY687 na baada ya muda mfupi nikakuta salio langu la maongezi ni sifuri.
Nikanunua vocha na kutumiwa tshs 10,000 na hela yote imekatwa tena.
Wateja wa Vodacom jihadharini, kuna mwizi kaingia mtandaoni Vodacom
UPDATE
=====
VODACOM wamefanya ustaarabu wa kunipigia baada ya kuona detail ya transaction hapo juu, na kuiona kwenye mtandao wa Jamiiforums.
Kimsingi wameapologise kwa mtafaruku uliotokea lakini wamenieleza nifike ofisini kwao kuona aian ya simu ninyotumia isije ikawa data apps ziko wazi.
Na kweli baada ya maongezi ya kuchunguza, mobile data setting ilikuwa ON, na mimeizima sasa.
Hata hivyo ni vema nitaenda kupata maelezo ya kuyeyuka kwa salio langu , karibu 20,000, kwa siku moja.
Wanabodi mtajulishwa inawezekana kuna wenye tatizo kama langu.
UPDATE
=====
Nimeonana na waheshimiwa sana wa Customer Care pale Block 4 Mlimani City.
Cha kusikitisha ni wao kushindwa kuchukua malalamiko yangu na kuyafanyia kazi, na hii ni licha ya kuwaelewesha kuwa hili tukio nalijawahi kunitokea na hii kuwa ni mara ya kwanza.
Hawa jamaa wa Customer Care ni kama mabalozi waliopewa jukumu la kusafisha kampuni ya VODACOM hata kama inanuka kwa wizi uliodhahiri.
Kitu ambacho hawajui ni kuwa nilifanya due diligence kupitia wafanyakazi ndani ya VODACOM walionidhihirishia kuwa kuna wafanyakazi wasio waaminifu ambao wana access na personal security settings za wateja.
Na wafanyakazi hao huwa "wapiga kishenzi" fedha za wateja.
Kwa kifupi mtu wa Customer Care ameshindwa kuniconvince na maelezo yake ya upotevu wa Tshs 20,000 katika mtandao wa VODACOM.
Nachukia sana kitendo cha kununua kifurushi cha internet halafu kikiisha eti siwezi nunua tena mpaka muda uishe. Mambo gani ya technologia ya kizamani