Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Naomba mjue asilimia 90 ya wateja wenu Ruaha National Park tunatumia smartphones, mtuwekee 3G
 
Voda acheni upuuzi,nimenunua kifurushi cha wiki (10,000) nimetumia siku moja tu nashangaa Leo nashindwa hata kufungua page,mnavyo tufanyia sio vzr,huo ni wizi wa wazi kabisa.
 
Voda ni waizi wa waziwazi, nimenunua umeme through mpesa sijapata majibu mpaka leo na imepita wiki sasa, jana nimenunua umeme mara mbili no msg no token, ukiongea na hao customer care hawajui chochote.
Unamuelezea mtu shida yako eti ananiambia niende tanesco nikaulizie wakati mimi nimenunua umeme kupitia simu yenye mtandao wa voda.
Tanesco wana kitengo cha simu kuhusu token zilizogoma kuja to my phone?
Nyie voda mna akili sawasawa kweli au hao watu wa customer care ni vilaza to the xtreme?

Jana nikanunua umeme tena msg ikafail lkn balance ya mpesa ikakata sasa hapa niende wapi coz customer care waliniambia nisubiri 24hrs hela itarudi au nitapata msg ya token, mpaka sasa inaenda 30hrs no any msg.
Customer care kila mtu ana jibu lake sasa najiuliza huko customer care ni makampuni tofauti ya simu au ni vodacom?
Nimechoka na nimesurrender.

Poor Vodacom popote ilipo.
Mtumiaji kaa mbali sana na vodacom hawa ni waizi wa kimachomacho.

Mitandao mingine system ikigoma unarudishiwa balance yako hapohapo.
CC: Vodacom Tanzania
 
Last edited by a moderator:
Nilituma fedha kidogo mwishoni mwa juma kwa familia huko nyumbani kwa njia ya M-Pesa kupitia Western Union. Nilipata notification kuwa fedha zimeshatumwa na watu wote niliowatumia walipata kwenye "salio" lao fedha hiyo - kuonesha kuwa imefika. Ngoma imekuwa kwenye kwenda kuichukua hiyo fedha. M-Pesa (voda) wanawaambia bado "iko hewani". Sasa hiyo ilikuwa Jumamosi na sasa leo ni Jumatano.

Sasa labda niulize kuna tatizo gani na kuna wengine wameathirika na hili? Ni tatizo la WU au M-Pesa wenyewe? Kama kuna tatizo ni vizuri wakawajulisha watu watumie WU kwa njia ile ya zamani (kwenda posta au benki au wakala wa WU) ambapo hakuna matatizo.

Zamani ilikuwa ni huduma nzuri sana kuweza kufikisha fedha kwa ndugu na jamaa zetu huko nyumbani kwa kutumia M-Pesa lakini nadhani hii itakuwa ni mara ya mwisho kwangu.
 
Ila mi nimeshahamia halotel huu mtandao mpya

Net yao ni nzuri sn tena sn H+ imejaa kila mahali

Haina mfano kwa hapa tz na mitandao mingine aisee
 
Voda hujuma sn yani mnamakato sn

Mtu unajiunga na kifurushi cha voda kwa voda cha 650 hupewi hata sms 1

Wkt zaman mlikuwa mnatupa sms

Hii imeniudhi sn
 
Vodacom wafanyakaz wenu kushirikiana na max malipo kutaka kupiga hela za wateja jiangalieni itawatokea puani.
 
Tunaomba mje UDOM mboreshe huduma ya internet ni mbovu mno kias wanafunzi tinaenda kufanya shughul zetu za kimasomo mjini!!
 
Mtandao wenu ovyoo&too costful...Yaani natumie line yenu pale ninapowasiliana na mama kijijini(No option)....ambapo nampigia mara 1 kwa week 2...
 
Nilinunua umeme..
Nikaja kuupata baada ya siku 12..Nayo ni baada ya kuhenyeshwa sana....
Customer care yenu ya DODOMA Mjini ipo OVYO MNO..
Wana majibu ya SHOMBO..Tangu manager wao.
Na yule Dada mwenye pregnant......
SINTOKAA NINUNUE CHOCHOTE through m-pesa
 
Afu kwann hii 100;# ya huduma kwa wateja..
Mme-associate na matangazo?...
MNACHOFANYA HAPO NI ...
sawa na kuweka..."tangazo la biashara msibani".
Mtu anashida...yake tayari...
anatafuta msaada we unamlazimisha na VIMATANGAZO.....


Ovyoooo...--->(Vibaya mnajitembeza)
Boresheni huduma...shusheni bei zenu...watakuja tu wenyewe.
 
WEKENI CUSTOMER CARE VIJANA WALIOSOMA /Wenye degree master,Wenye utu.......WANAOJITAMBUA NA WALIOSOMEA CUSTOMER CARE MANAGEMENT.....
(Mnaweka vi form 4.....afu vinajibu majibu mabovu utafikiri ndo vitajiri vyenyewe....hasa Dodoma mjini....Nikiwa na shida ntapanda gari kwenda customer care ya Morogoro na sio Dodoma mjini vodashop...)
 
Vodacom ni mtandao ninaotumia siku zote ni sijawahi toka huko ila kwa walichonifanyia sitatuma hela, sitatumia tena internet yao, sitatuma tena voda kufunga ama kupay bills zangu hawa jamaa wamegeuka wakatili vibaya badala ya kuenjoy service imekuwa ni kero hata nilipopiga simu customer care eti nakaripiwa na mhudumu eti mimi nimsumbufu hivi ni nani ataamka asubuhi aache familia yake aanze kuwasumbua vodacom customers care?? nilichojifunza ni kwamba huu mtandao sasa hivi haujali mteja maadam unaweka hela basi mteja kwao si lolote hasa wakishakata hela yako. Nimefedheheshwa sana na mhudumu wenu anaitwa Anna sijadhani kama ni sahihi badala ya kusikiliza tatizo langu yeye ananinyamazisha eti yeye ndo anajua ananiambia eti kama huelewi nenda vodashop namwambia mama hapa nipo malinyi hiyo vodashop maeneo nilipo hakuna ni mbali sana kufika cha msingi uniambie hela karibu 48,000 imeishaje ndani ya saa 24 na mi sijapiga simu??mhudumu ananiambia nenda kamuulize huyo mwajiri wako kama kaweka hela na uache ubishi na gafla nikakatiwa simu.Hii ndo customer care tunayopewa I Wish wakurugenzi na maboss wa voda wangekuwa wanajua tunayofanyiwa na wafanyakazi wao kama huyu dada yaani hajui kama watu tunavyotumia mtandao ndo kampuni inatengeneza hela na kupata hela ya kumlipa mshahara!!! Huyu mhudumu Anna she has no respect to vodacom customers na amenifanya niwachukie voda I swear sitafanya transaction kupitia mtandao wao tena itabaki kutuma msg tu kupiga ntatumia mtandao mwingine asante Anna nakushauri ujirekebishe otherwise kwa hii treatment utafukuza wengi.Asante na Mungu awabariki
 
Unapokuwa airtime we use to receice a notification msg lakini sasa hivi hawatumi matokeo yake unajikuta umetumia hela yote unknowingly badala wangekufahamisha uka subscribe bundle wenyewe hawatumi msg ili wakucharge kwa rate kubwa wakati source ni wao kutokutuma msg na ukipiga kuuliza ni majibu ya kudiscourage kama ya dada Anna voda wakatili sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…