Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Jamani poleni kwa matatizo yote,lakini nina ushauri wangu kwenu,hamieni Halotel,kwanza uhakika wa mawasiliano yako kwa maeneo mengi Tanzania,(zaidi ya asilimia 90) mjini na vijijini),ubora wa huduma za upigaji,upokeaji wa simu za miito,ubora na spidi ya juu zaidi ya 3G mahali pote.Gharama nafuu zinazoendana na ubora wa huduma.

Karibuni Halotel
Pamoja katika ubora
 
Gharama nafuu my foot
 
wakuu naombeni internet setting ya vodacom ....nimenunua simu mpya samsung j7 naona kila nikijaribu kutia setting ya internet ininazopewa na watu haikubali ..naomba msaada please ..
 
VODACOM nyie ni wezi wa kufa mtu.
Jana nimeweka Tsh 2000 kutoka MPesa yangu kama credit.
Nikaweka Ths 999 kama Cheka time(hivyo nimebaki na Tshs1001)
Najaribu kuweka Internet ya bundle ya 500MB ya masaa 24, eti mtandao wa VODA ukasema sina salio!!!
Nikaamua kumuuliza dada wa customer service baada ya kudial 100, baada ya kujibaraguza kwingi akaniambia kama data function iko ON mtandao wa VODACOM unakomba hela zote!!
Nikamuuliza sasahii inakuwaje mtandao unakomba hela yangu wakati sikjatumia service ya VODA, huyo dada akasema naye hajui.
Mimi nikamwambia mtandao umekuwa set kuiba salio la wateja!!
Huyo dada akasema yeye ndio mwisho wake wa kujieleza!!!

Nami nikamwambia VODACOM NI WEZI!!
Watatumiaje salio langu wakati sijatumia service yao baada ya kuingiza salio?
SasaVodacom tudhihirishie kama ninyi si wezi.
 
...hii ipo hata huku nilipo,usipozima data function lazima utaliwa tu,jifunze kuzima data kabla hujaweka salio..
 
...hii ipo hata huku nilipo,usipozima data function lazima utaliwa tu,jifunze kuzima data kabla hujaweka salio..
Mkuu computer ni settings, kama umeziset kuiba salio za wateja hakuna njia nyingine za kuterm zoezi hilo, ni WIZI.
 
Mimi bwana ...naitumia kwa m pesa tu.ILA wameniudhi,nilienda kuomba taarifa fupi ya account yangu ya m pesa ya miezi 5,ajabu!niliambiwa nitoe elfu 6 kwa kila mwezi ninaotaka kuangalia taarifa zake...yaaani!Tatizo wao wanadominate huku kwetu vijijini kwao na mapadlock.
 
Utaratibu wenu wa kutoa line za M PESA sio mzuri leo nimeenda pale NHC customer care na vielelezo vyote eti mtanijibu ndani ya miezi mitatu jamani line ni yenu na nyie ndo mnanufaika sana kwa nini msiseme tu kama hamtoi kuliko kumwambia mteja asubiri miezi mitatu ni ukiritimba nimeondoka na vitu vyangu.mnajenga mazingira ya urasimu tu huku mtaani ukimpa mtu hela laki mbili anakuletea line tukifuata taratibu hamtoi ndo nini hivyo nimechukizwa sana na hilo.Maoni yangu msiwe walasimu wateja wengine hatupendi njia za mkato mfano mimi nimeamua kuacha coz of kukaa miezi mitatu wakati wengine wanaotoa hela ni siku moja
 
Vodacom Tanzania; kwanini mmeondoa vifurushi vya internet vya unlimited?!
Huu uamuzi wenu umeni-disappoint sana kwa kweli...
 
Nmeunga dk 90 voda to voda za wiki imepita cku mbili mnanambia kifurush kimeisha mda wake...hakiamungu ntawashitaki naomba mnirudishie dk zangu
 
Mimi nna maswali mawili
mna wateja wangapi wa smart phones now?
wangapi wako nje ya Dar?
 
HALOTEL ndo mpango mzima 3G full had huk pori,
TNASUBIRI HALOPESA TU.
Kw sasa nawachukia sana Voda,
 
Huu ujinga wa kuweka limit ya matumizi ya data ni wizi mweupe kabisa. Haiwezekani ninunue kwa mfano MB za buku mnilazimishe nitumie ndani ya siku moja,wakati huo huo kuna mtu anaweza tumia ndani ya masaa 6. kwa nini msiache nitumie hadi nitakapo zimaliza hata kama ni kwa wiki moja. tunatofautiana vipato na matumizi. eti zikibaki mnaziondoa,inamaana mnaziuza tena.
NITUMIE KADIRI NILIVYOLIPIA,YAWE MASAA SIKU,WIKI MIEZI N.K HIYO NDIYO PRICE YA BIDHAA NILIYOLIPIA IWEJE MZICHUKUE ZINAZOBAKI?
 

Naungana na Mpalakugenda ...................mashirika yote mnaiba hapa. na kwa kuwa mie ni mteja wenu Voda mnaniibia vifurushi vyangu vya interenet kia siku; nimeweka 1 GB for one week ilifanya kazi only 3 days siku nyingine zote ni chenga tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…