Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Voda wamekuwa wapuuzi sana.
Voda ni tatizo sana kwanza kabisa wamekuwa gharama sana Ina maana sasahivi huwezi jiunga bundle kwa shs 4,000 kwa wiki
Na ukijiunga hyo bundle ya wiki unapata kibubu sasa sielewi wkt gani hicho kibubu kinatumika voda kaeni chonjo
 
Leo 11/8/2016 nimenunua vocha ya vodacom na kuingiza kwenye simu yangu.Ukatokea ujimbe usemao:"Samahani kuna tatizo la mfumo, jaribu baadaye."

Nikasubiri kama dakika tano hivi nikaingiza tena vocha.Nikashangazwa na ujumbe uliotokea. Ukasema hivi: "Vocha unayojaribu kutumia yenye namba 7175831260 imeshatumika kwenye namba inayoishia 56498 tarehe 11/08/2016, namba nilizobold ni namba zangu tano za mwisho za simu yangu. Nikacheki salio, hakuna kitu.

Vodacom, ni kitu gani hiki?
 
Mmiliki wa ********** umechaguliwa kushiriki katika droo ya TZS 5,000,000 kesho! Tuma neno GO kwenda 15544 SASA & UJIUNGE Vodacom KAMATA MPUNGA! TZS 300/SMS

Acheni kutuma huu upumbavu.
 
Ahsante kwa kinivumbua macho naivunja voda hapa hapo wakuu mwenyewe natumia voda ila kununua vfurush na huwa natumia Universty bando kuna mda nikiweka salio nikitaka kuunga universty bandle wanaondoa ile menu na nikiunga vifurush vya kawaida saa 24 nikirudi nakuta menyu ya *149*42# imerudi! Kudadek nawashaurin watanzania tunaenda na mda tuachane nao kwanza wakisharekebisha huduma zao ndo turudi!
 
Majizi tu haya. Kampuni zinazofanya vizuri kama hii voda zinaharibiwa na waajiriwa wao walafi na wasio waaminifu, sijui michakato yao ya kupata wafanyakazi huwa wanaifanyaje?
 
Mimi wameniingizia elfu 50 kwa mpesa tangu j2. Imeonekana imeingia kutoka NMB (kwa mujibu wa sms waliyonitumia). Tangia hapo kila nikitaka kutumia huduma za mpesa naambiwa akaunti yako imefungwa. Nikitaka kuongea na huduma kwa wateja simu inakatwa pale inapofikia stage ya kuongea na mtoa huduma kwa wateja.

Wanakera sana hawa.
 
Hivi hii imekaa sawa?!! Maana nahisi kuumiaumia vile!
 

Attachments

  • 1472307807688.jpg
    45.2 KB · Views: 66
Mtandao wa vodacom na matangazo yake una kasoro nyingi,
Naanza kueleza ninazojua kama ifuatavyo
1.walipoleta ongea deile, walisema unajiunga, unaongea dakika 10, @sh 300, baada ya hapo unaongea deilee...

wee!
nikaweka salio 500, kufuatilia ofa then nikajiunga,nikapiga simu ya kwanza nikaongea dakika 3 SIMU ikakatika, nikatumiwa SMS kwamba bado kidogo nianze kuongea deilee (yaani niwe nimetimiza masharti ya kuongea muda Fulani bure) [dakika 60 kama sijasahau], nikanunua vocha ya pili ya 500 nikaongea ikaisha zikawa buku, meseji ikaja nyingine tena kwamba bado sijatimiza vigezo!!!

Kama masharti ni dk 10 kwa 300@dk baada ya kujiunga kwa nn buku iliisha kabla sijatimiza vigezo??!

2: nimekuwa nikinunua muda wa maongezi, nikinunua kifurushi SAA 11 jioni napiga SIMU 1 au 2 za dakika kama mbili mbili, kwa makusudi kabisa nikifuatilia upotevu ambao nauona kila siku, asubuhi nikiamka napiga mswaki tu SAA mbili meseji inaingia
"Kifurushi chako kimekwisha muda wake" mm! Asubuhi hii? Nikaona wizi huu!!
Nikaacha kuitumia kuongea, kwa kuwa niliko AIRTEL internet na tigo zote ni spidi ya Kobe nikaona hii sasa

3 itakuwa ya internet tu!
Mm nikawa nanunua bando,ila nikianza matumizi naona mda nfupi tu! Kifurushi kimekwisha nanunua tena uzi uelule
Nikaona aa! wapi
Nikanunua Halotel
Sasa natesa! Ingawa huenda nao watabadilika poa tu ila hawaibi kabisa,

Hata ukinunua kifurushi cha voda cha bei sawa na cha AIRTEL kwa matumizi Yale yale , cha voda kinaisha haraka!!

Voda kwa sasa naitumia, siwezi kuiacha kwa sababu INA huduma nyingine ambazo pia ni nuhimu pia ni special no, pia ila siyo first wala second inaish kwenye wallet pamoja na ATM's leseni na vitambulisho vingine!

Inawezekana
mitambo yao imezidiwa tuwasamehe bure ila tuwajulishe waangalie tatizo, maana kila mhudumu ana kasoro zake na ubora wake!!
 
Sikuwahi kufikiria kuhama mtandao ila itabidi tu niachane na Vodacom
Bundle za internet zinakera sana
 
Voda mm nimeifanya simu ya mezani kuna sh 70tu kwa ajiri ya dada wa nyumbani akiwa na shida anatubeep ni miezi 6sasa wamezidi na wizi Halotel ndio habari ya mjini
 
Nlijua tu mngeukimbia huu uzi wenu!!! Li line lenu naliweka kabatini
 
Mmmh kwani umefunga ndoa na vodacom ?
 
Mkuu napenda nikuhakishie kwamba vidacom ni majizi, tena majizi waliokubuhu.
 
Mkuu napenda nikuhakishie kwamba vidacom ni majizi, tena majizi waliokubuhu.
Mimi nina sim card mbili za voda tangu wamenitenda mwaka jana sijatumia tena hilo card zao nilinunua airtel. Nawapongeza wale woote mnaopaza sauti japo mimi niliwatoroka kimya kimya.
 
yani kifurushi kilichokuwa kinauzwa 1000 chenye mb 200 kwa wiki voda hakipo tena..eti kinauzwa shilingi 3000 kwa 4000..cijui lengo lao ni nini..
Artel nao wamepandisha bei za vifurushi..jamani hii ni kutuumiza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…