Ni aibu kubwa kwa mtandao mkongwe kama Vodacom katika huduma yake ya MPESA kutokuwepo na menu ya kumuwezesha mteja kurequest statement ya mwezi, miezi mitatu na miezi sita eti mpaka uende physically VODASHOP, This is ridiculous, yaani kwa karne hii kweli bado mmeshindwa kuwa wabunifu mkaweka hii huduma kwenye menu ya simu au la mmeshindwa kabisa tuwekeeni hiyo huduma kwenye website yenu. Watu wenu wa IT sijui wanafanya kazi gani??? La mmeshindwa igeni kwa wenzenu "tigo jihudumie" huduma bora kabisa iliyoko kwenye tigopesa.
Mimi ni mhasibu wa kikundi ambacho members hutuma michango yao...yaani members wakituma fee zao kupitia MPESA ni sheeeda, sometimes hata meseji haziji unakuta lumpsum, mpk uende vodashop kufuatilia statement ndo ujue nani walituma.....its bulsheet. INAKERA SANA.
Pili meseji inayokupa taarifa ya kiasi gani umetuma na balance gani imebaki haisemi kiasi gani mmekata kwa huduma husika kama wenzenu wa tigopesa wanavyofanya.
Tatu menu ya mpesa au sub menu zenu hazina option ya kurudi nyuma one step au kurudi menu kuu.....ukitaka kurudi nyuma mpk upige upya aidha *150*00* au ni kifurushi *149*01#....igeni wenzenu wa tigo ukishabofya *150*01# ukaingia kwenye submenu unaweza anza kurudi nyuma kwa kubofya 99.
Nimeripoti hili swala several times customer care...but hola...hamna utekelezaji....msitulazimishe tupige kampeni members wetu waache kutuma kwa mpesa.
Nawasilisha.
Sent using
Jamii Forums mobile app