Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Laini ukiipoteza au ukaiweka kapuni ikizidi mwezi hufungwa mwezi tena ukipita hufutwa mwezi unaofatia hupewa MTU mwingine

Ila kama una mpunga wako Mpesa njoo ofisini unapewa bila wasiwasi
 
Hapa nimepapenda,siku hizi nikiongea na CC akijitambulisha jina naandika katika kalatasi kabisa!sasa je ukipiga akapokea yule yule alienikwanza?nitajuaje ninaeongea nae supervisor?
-Matatizo yangu,mimi natumia huduma ya BBM,huwa najiunga kifurushi cha mwezi,wiki,na siku,inategemea kipindi hiko nina kiasi gani.
-Tatizo ni pale ninapojiunga na kifurushi cha siku(24),alafu unakuta zaidi ya matatu au manne huduma sijapata,unakuta nimejaribu kutoa betri ili kurestart,ila wapi,nawapigia CC wanaleta longolongo,na ikifikika saa 6 usiku,huduma inakua imeisha,Kwanini hamtufidii wateja kwa uzembe wenu,tatizo ni lenu si langu...!
-Tatizo lingine mmeweka ukomo wa kuwapigia CC(Customer Care
) kwa mwezi,hamjatenda haki kwa wateja,matatizo mengi ni yenu nyinyi Voda,kwanini mnilazimishe niende katika namba ya kulipia?kuongea na CC?
-Tatizo lingine linalotukera ni mesej na simu zenu za matangazo ambayo si muhimu kwa mteja,mfano kuchagua wimbo,nk,unakuta umelala unasikia cm inaita unaamka kupokea,unaambia sijui chagua Wimbo,unaoupenda...huu ni upuuzi sana,namba ya simu ni Mali yangu binafsi...kwanini mnikere.....
Naomba majibu

Masuala ya data kuna kitengo maalum cha data ukipiga omba unahunganishwa nao watakupa msaada mzuri zaidi
 
Ukomo lazima huwepo coz hakuna cha bure hata Voda wanatozwa kama mia mbili kwa kila simu ambayo wewe unaiita simu ya bure
 
Mimi nilipiga simu kulalamikia kutokutumiwa umeme wangu wa elfu 30,nikagombezwa baada ya apo nkafungiwa line yangu kupiga customer care naambiwa et kuna mtu ama report et simu yangu iyo imeibiwa,na mimi ndo mmilki wa iyo namba.msaada tafadhali

Aisee pole sana unaweza nitumie namba uliyotumia kupiga niwatafute wahusika walio kufanyia huo uhuni nisikilize call yako niweza kujudge
 
Mkuu napingana na wewe kwa asilimia mia hakuna watu wanaofanya kazi kama customer care wa Voda tena kwa ufanisi na kujali wa teja japo mishahara yao inasikitiasha na kuvunja moyo labda kama hujui agent mmoja anapokea zaidi ya simu mia mbili na kuendelea kutatua tatizo kujaza form za kila simu na kumantain quality ya Huduma hata kama Mteja akija kwa dharau hasira au matusi hana muda wa kupumzika zaidi ya muda wa lisaa limoja nalo uligawe muda wa chai na lanchi ni kosa la jinai kuingia katika taarifa za Mteja kinyume cha taratibu hata ni mkeo ni ukibainika ni nyumbani
Sasa usiongee kitu uasicho kijua
Tumekuletea hili tatizo tukijua waweza kulitatua.

Umeshindwa , sasa badala ya kujigamba mtandaoni hebu tupe uaratibu wa kulalamika au kufuatilia WIZI kama ulionipata mimi.

Kwamaba watu wa Customer Care wako overworked si suala la mteja , ni poor management system yenu , na halitakiwi kuwa utetezi kwa kutotatua wizi ndani ya mtandao wenu.

At any rate hiyo itaonekana kama ku condone unfaithfulness ya wafanyakazi wachache walio ndani ya kampuni yenu.

Kama mtashindwa hivyo basi tupe utaratibu wa kuwasilisha na kufuatilia TCRA.
WIZI upo ndani ya VODACOM hilo si suala la ubishi.
 
Tumekuletea hili tatizo tukijua waweza kulitatua.
Umeshindwa , sasa badala ya kujigamba mtandaoni hebu tupe uaratibu wa kulalamika au kufuatilia WIZI kama ulionipata mimi.
Kwamaba watu wa Customer Care wako overworked si suala la mteja , ni poor management system yenu , na halitakiwi kuwa utetezi kwa kutotatua wizi ndani ya mtandao wenu.
At any rate hiyo itaonekana kama ku condone unfaithfulness ya wafanyakazi wachache walio ndani ya kampuni yenu.

Kama mtashindwa hivyo basi tupe utaratibu wa kuwasilisha na kufuatilia TCRA.
WIZI upo ndani ya VODACOM hilo si suala la ubishi.

Kaka ebu kuwa specific
 
Huku bado baadhi ya sehemu kuna siku huwa haupatikani kabisa huku wateja tukiwa tumenunua vifurushi vya cheka ya kupiga,kutuma msg na kwaajili internet mbaya zaidi muda mnapokuwa hampatikani yaani minara yenu kushindwa kuwa vzr kwamaana simu huwa hazitoki wala kuingia kwa mteja aliyeko maeneo hayo.


Kwanini mnaporudi hewani halafu yule mteja kifurushi chake kikaisha muda wakati tatizo mmesababisha VODA kwa minara yenu na server kushindwa kuwaruhusu wateja kupiga simu wanapokuwa na virushi msiwarudishie vifurushi vyao kwakufidia makosa mliyofanya ninyi voda.


Jaribuni kuwa kama tigo wanapofanya makosa hurudisha kwa mteja wao muda wa maongezi,msg na kifurushi cha internet lakini pia wakimtaka radhi lakini kwa voda huwa wizi umeshamiri sana hasa kuna siku mtandao hauruhusu simu kwenda nje,yaani cheka inapokaribia mwisho mtandao unakorofisha.


Lipeleke hili kwenye uongozi wako minara inaposhindwa kufanya kazi na makosa ni yenu mturudishie muda wetu wetu wa cheka na bundle za neti.

Mkuu upo mkoa gani
 
Inakuaje voda inawateja wengi kuliko airtel lakini airtel wapo ktk ten large tax payers TRA vodacom wasiwepo?mbinu gani mnatumia kukwepa kodi?
 
Mkoa wa Kigoma wilaya ya Kasulu

Kaka tokea nianze kazi sijapata kuona mkoa wenye matatizo kama kigoma sijui kwa nini management hawalitii mkazo kutatua hilo tatizo moja kwa moja
 
Inakuaje voda inawateja wengi kuliko airtel lakini airtel wapo ktk ten large tax payers TRA vodacom wasiwepo?mbinu gani mnatumia kukwepa kodi?

Inaonekana huna habari Vodacom ndio wanaongoza kulipa kodi sambamba na kuchangia Huduma za jamii kupitia Vodacom foundation
Usisahau ndio wadhamini wakuu wa premiere league
 
Usipime asee,Bahati mbaya wanatajaga majina yao,namkumbka sana uyo sister nataka kujua namwazibu vip kwa hasara aliyonletea wiki mbili sasa sipatikani hewani kisa yeye ccpapiso

Tutembelee na kibarua chake kitategemea huruma yako Voda hawamvumilii hata wengi washafukuzwa
 
papiso,

Nimemtumia mtu 178,000 kupitia Mpesa kwenda namba yake ya TiGo nikafanya mistake ya digit moja zikamfikia mwingine, huyu mwingine alivyokuwa sharp kazi-draw zile pesa haraka haraka, kaniwahi hata kabla sijawajulisha Mpesa. Baada ya kuwajulisha Mpesa kupitia namba ya huduma ya kulipia 15366 wakasema kweli umetuma na kweli zimechukuliwa na watakuwa wanamkata au akiingiza pesa watanirudishia lakini niwe nawakumbusha kila siku.

Hili la kuwakumbusha kila siku ndio linanipa shida. Jee, kuna ufumbuzi mwingine wa kupata pesa zangu? Au ndio maasalama.
 
Last edited by a moderator:
Nimeanza kupokea SMS kutoka kwa watu mbalimbali nitaanza kushughulikia matatizo yenu Vodacom kazi ni kwako karibuni sana
 
Mkuu papiso nimekupm tokea asubuh iyo number iliyofungwa baada ya kununua umeme wa elfu 31500 na sijaupata mpaka leo na mpaka leo number imefungiwa,nlipiga customer care nikaambiwa et imekuwa reported imeibiwa kitu ambacho sijawahi fanya mkuu.kuibiwa simu big NOOOO
 
Back
Top Bottom