Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Zamani ilikuwa 24 hrs sasa ikaonekana wafanyakazi wengi wana access ya kufanya reversal ,ikaja changamoto ya security ya pesa ,walichofanya kuimarisha security ya pesa ya mtumiaji ni Huduma wakapunguza idadi ya watu wa kuingia kwenye system ndiyo kiss cha kuweka muda wa Masaa 72, huyo aliyekujibu kuwa nisiku saba alikuwa ana stress zake tu,ila wewe make sure kuwa jina linaloonyesha kabla ya kutuma ni la mlengwa acha uzembe unapo tuma pesa.
 
Siwatetei Voda, hata mimi nimeshakua muhanga wa hili jambo zaidi ya mara moja.

Nafikiri ni kutokana na haya mambo mawili, kwanza kabisa, uaminifu, kuna ile mtu anakutumia pesa kisha anapiga simu kusingizia amekosea namba wakati ki ukweli ameghairi au kuahirisha adhma yake, hapo inabidi kampuni ya simu wajirishe kabla ya kuugeuza muamala.

Pili, kuibuka kwa utapeli kwa baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu wa kwenye makampuni ya simu, hii imesababisha uimarishaji wa mchakato na uhakiki wa kurudisha hiyo miamala ili kupunguza kampuni kupigwa.
 
VODACOM

Wezi sana nimejaribu kuwafuata kwenye page yao , wananiambia huo ndo utaratibu wao , niko na rafiki yangu mumoja hapa alikosea pesa ofcoz ni uzembe lakini ilikaa wiki mbili, ukipiga simu wanongea ongea, mimi nafikili cha msingi this time naenda kuleft huduma hii
 
Juzi tu hapa nimekosea wamerudisha within 24hrs [HASHTAG]#Pesa[/HASHTAG] ni mpesa


Mimi niliwahi kusimuliwa na mtu kuwa VODOCOM sio watu wazuri wanachelewesha reversal , nilikataa na nikamwambia mimi nikipiga simu huwa hawachukuwi muda mrefu, masaa 72 yalikuwa hayafiki napata muamala na kuna siku nakumbuka nilifanyiwa reversal within the day, Ndungu yangu kama vile niliomba na mimi nikosea nipate uzoefu....

Hii inaitwa isije kukupata ukawaelewa Hatariiiiiiiiiiiiiiii alfu unaitaka hio pesa
 
Jamaa nia yko ni kuuza sura ili upate mademu ama!!!!!
 
Cheki sasa wanaume washalike you're lips
 

nimesikia mnauza vocha za Tsh 50 ,100 na 200 kwenye vituo vya mabasi ya mwendo kasi , je ni kweli mna vocha za aina hii?
 
Vodacom na mitandao mingine embu boresheni mifumo yenu haswa pale mtu anapotuma hela kimakosa mtandao mwingine.masaa 72 kusubiria hela irudi ilipotoka ni inshu.halafu sasa hela kule ilipoenda kimakosa kama imeshatolewa rudisheni basi majibu hata kwa sms.

Nilituma hela kimakosa kwenda voda kutoka tigo sijajibiwa na tigo hela haikukutwa kwenye hiyo voda iliyotumiwa hela.ingawa nimewapigia tigo five times.mara tu nilipotoa taarifa just 2-5 minutes nilishatoa taarifa tigo.

lakini hela haikurudi nabaki tu naambiwa tatizo lako tunalipatia ufumbuzi.halafu hizi kampuni customer care line ina matangazo mengi sana.punguzeni.nafaham ningeipata ile hela isingekuwa matangazo lukuki na ushirikiano wenu mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…