Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

kama ulishaipata shukru sana mimi saiz huu mwezi wa pili ambacho walikifanya walinipa namba ya kampuni ambako nilikosea ndo wanairudishie mpka nimekata tamaa


############Yajayo wanafurahisha wanasema ivo...
 
Nimetoka kuongea na customer care wenu hivi punde, ni washenzi sana yaan huyu dada ananikaripia wakati mi ni mteja? Shenzi.
 
Nimetoka kuongea na customer care wenu hivi punde, ni washenzi sana yaan huyu dada ananikaripia wakati mi ni mteja? Shenzi.
Sorry, nimekosea badala ya nmb nimepost kwenye vodacom. Voda nyie hamjawahi kuniangusha
 
 
Utasikia basi limeua wanne,
Piki piki imeua sita,
Au waliokufa muhimbili wamefika 100 kwa mwaka jana,
Meli ya Nungwi imeua 60,

Na hao ni wateja wa M-PESA, Tigo pesa na Airtel money,

Hela zao zinaendaga wapi?

Kuna utaratibu upi wa kuwapatia survivorship au next of kin wao?
 
namba yangu ya voda haipokei call za tgo na airtel baadhi na hata sms namba yangu 0764883712
 
Vodacom huu ushenzi wa mtu kununua bundle alafu ndo mnamtumia eti furahia instagram bure na Facebook yenye picha muache kabsa.
Mbona kabla ya kununua bundle hamtoi izo offer?
 
Leo ni siku ya nane hakuna huduma ya mtandao wenu Geita wilaya ya Mbogwe Masumbwe hebu shughulikieni ttz hilo watu wapate huduma.
 
Mkuu tafadhali nipatie utaratibu wa jinsi ya kuwa super agent wa m-pesa.
 
Mimi nimeboreka sana na Voda.
Juzi kati nilifiwa nikiwa nimesafiri.

Nilipopewa taarifa ya msiba nikawatumia nyumbani kiasi cha 550,000 kupitia voda kwenda tigo.
Cha kushangaza, pesa haikumfikia mlengwa japo ilikuwa imekatwa kwenye akaunti yangu

Nilipowauliza voda walinijibu kuwa kulikuwa na tatizo kwenye system yao,hivyo nisubiri siku tatu watarudisha pesa yangu.

Fikiria nina msiba na akiba niliyokuwa nayo yote imeepotelea hewani kwa matatizo ya vodacom.

Kwa kweli nilikwazika sana imgawa pesa ilikuja kurudishwa baada ya siku mbili.

Hata hivyo ni baada ya malumbano makali kati yangu ns uongozi wa voda.
Nashauri voda mjirekebishe kwenye hili,hasa inapotokea kwamba kosa sio la mteja wenu bali ni lenu.
 
Voda mnaudhi sana kwa vifurushi vyenu binafsi nimekuwa na disused card ya voda yaan hii haiwekwi vocha ila ipo hewan, nilikuwa nawekaga vocha ya 10000 napata dk 200 mitandao yote.

nikitaka voda to voda napata dk 300 ila nilipojiunga airtel nimewachoka mazima Kwa ten elfu napata dk 315 na huu mwezi wa pasaka nimepata dk 450 mitandao yote. nilichokipenda huku ni usikivu mzuri wakati wa kuongea na sim tofauti na voda usikivu hauko vizuri, pili punguzeni gharama, kinginene mtandao wenu hauna nguvu kwenye kupiga cm unaweza ukawa hewan ukipigiwa haupatikani.
 
Mimi nilinunua hisa ya Vodacom lakini mpaka sasa sijapata mrejesho wowote kuhusiana na hisa yangu.

Ninawazo la kurudisha cheti chenu mnipe changu.

Huu ni mwaka tangu mmetuingiza chaka pesa yangu mnaizalisha faida kwenu mimi sipati chochote naomba mnipe maelekezo wapi nije kudai amana yangu niliyowekeza.
 
SMS hili bando kuna muda zinakatka siku kazaa liko inactive na some times msg zinaanza kutoka baada ya kipindi chake kuisha.
 
Tusaidien vodacom msg kwenye hizi bundles ziwe active kutoka na kuingia mda wote
 
Nashauri unapolipia luku kumbukumbu za LUKU namba ya mita tuipate kwenye simu kama zamani sio kwenda kusoma mita kama ilivyo sasa
 
Vodacom , iko haja ya kuimarisha huduma za internet hasa vijijini, huduma hii ni dhaifu sana kwenye baadhi ya maeneo, smartphone haziko mijini tu.
 
Mbona mimi sipati huduma ya mkopo toka mpawa?? Ilihali ninaakiba tu ya kutosha niliyojiwekea kwenye mpawa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…