Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Mimi mmeniudhi kitu kimoja nimepoteza laini yangu kuirudisha naambiwa namba tano nilizokuwa nazipigia Mara kwa Mara sasa Mimi nazipata wapi wakati nimepoteza simu kitambulisho ninacho lakini mmeshindwa kunirudishia nimeamua kuachana na voda kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siwezi kuhangaika kujibizana nawe.unaonyesha tu jinsi uko mjinga au mlevi mlevi fulani.kweni umeona sina hiyo mitandao mingine?huu ni uzi wa halotel au tigo?pumbavu kabisa
 
Vodacom Tanzania sijui nianzie wapi kuelezea hili tatizo! Mwanzoni call quality kwa upande wa sound ilikua nzuri Sana.

Ila kwa sasa kwa kweli sio nzuri kabisaa inaumiza hadi masikio. Mmegusa nini huko kwenye mitambo yenu!? Unapiga simu inachukua dakika ku connect, au hata ku connect tu inakataa na if the call go through... It's quality is real poor you even hear ticking sounds humo humo kwa call Vitu kama "kwichi kwachu kwachu" yani ni kama vita. Mmepatwa na nini!?

Nilidhani ni simu yangu lakini sio kweli kwani nilibadili line na call quality ikawa safi kabisaa. Na sio peke yangu kwani hata wafanyakazi wenzangu wanalalamika hivihivi. Shida ni nini tena nipo Dsm inapopatikana 4g!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maswali ya kichochezi huwa hatujibu kwanza wewe tunamashaka na uraia wako[emoji1] [emoji1] [emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ukiwa unaambiwa kifurushi ni cha masaa 24 unatakiwa ukitumie chote kiishe ndani ya masaa 24, hapo unalalamika kitu ambacho vigezo na masharti yamezingatiwa, kuna vifurushi vya wiki mwezi jaribu hivyo au vp.

Afu kuliwa vocha ni simu yako ya smatifoni, mi kila nikiweka vocha nazima kwanza data maana simu itaichukua km kifurushi na kuanza kurefresh apps online.

Nimejibu km mteja tu wa vodacom sio muhusika wa vodacom.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila vodacom kuhusu swala la dar supa uni, tmk supa uni mnavurunda kweli, japo ipo kibiashara ingekuwa vizuri kutoa taarifa kuwa viwango vya kifurushi vitabadilika hapo baadae, sio kwa njia hii mnayotupiga sapraizi, mtu una jero lako unataka mb 500 za mtelezo unakuta holaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kero yangu ni hii tabia yenu ya kukatakata hela kwenye huduma ya SIM BANKING, yaani hata kama huduma ya benki haipatikani nyie mlishakata hela. Jirekebisheni jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NaitwaNm marwa
Ilitokea bahati mbaya nkakabwa na nikaibiwa namba simu na hivyo kupkupoteza till yangu ya mpesa.

Nauliza utaratibu wa kuirenew ukoje ukizingatia kukuwa niliinunua kwa mtu tu. Viambatanisho gani natakiwa kuwa navyo ili niniweze kuo renew?
Shukrani
 
Kuna matukio kadhaa nimeyashuhudia kwa macho na masikio yangu yaliyonifanya nihitimishe kuwa Vodacom ni mtandao mbaya Tz.

-Mtu mmoja kaweka vocha, vocha ikawa invalid tukawapigia Voda, wakatujibu kuwa iliingia sokoni kwa makosa, tusubiri baada ya siku 2 tutapata vocha nyingine. Shit , vocha niisubiri siku mbili, how.

-Line ya wife ilistack na Mpesa kuna kama laki 4, akarenew line sasa kurudishiwa huduma ya mpesa masharti mengi.

-Kuna mtu jana nilimpa kiasi fulani cha fedha aniwekee kwenye Tigo Pesa, ila aweke kwake kisha aitume kwangu mimi nilikuwa nimetingwa na majukumu. Kaweka kwenye Mpesa yake ili anitumie Tigo Pesa , Pesa kwake imeshatoka kwangu haipo. Unawapigia voda wanasema mtandao unasumbua.

Are they crazy?
Eti mtandao unasumbua utaipata, why ilikubali kutoka kwenye line moja?
Je, usumbufu nioioupata mtanilipa?
Ningekuwa na mamlaka kampuni kama hizi ningezifungisha virago.
 
Huelewi vyema nilichosema.kaa pembeni na ulevi wako,unatetea ujanja ujanja wa Vodacom unalipwa?kaa pembeni
 
Nina swali moja kwa watu wa mtandao, naombeni tafadhali mnijibu.

Ni hivi, kwa mfano mtu ameenda kusoma nje ya nchi hasa nchi za mbali huko, wakati akiwa nchini alikua akitumia mawasiliano ya simu kwa kupitia laini zenu je anavokua nje ya nchi halafu akakaa huko zaidi ya mwaka atakapokua amerudi masomoni ile laini yake ya simu atakua bado anaendelea kuitumia au haiwezekani na kama haiwezekani je kuna taratibu za kufuata ili aendelee kuitumia ile laini yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…