1. Mtu unakuta niko na simu nzuri kabisa ya kisasa(samsung/apple n.k) na settings zangu ziko sawa kabisa lakini kumekua na tatizo la internet kiasi mpaka inatia hasira.muda unaonunua kifurushi ndo unakuta muda unanyimwa huduma nzuri,mtandao unakua chini sana na upo town wala si porini kusema kwamba labda hakuna network la hasha.
2. Wateja tunanunua kifurushi na muda unapofika ule ulionunulia kifurushi kama ni 24hrs kifurushi kinaishia hapo hata kama MB bado uko nazo,huu nauita ni wizi mkubwa.kwa nini msiache mpaka MBs ziishe ndipo mtu anunue zingine?na kwa nini msiache mtu anapoingiza muda wa maongezi iwapo kifurushi cha internet kimekwisha ukiweka vocha inaliwa ghafla eti mpaka uzime data.kwa nini msiache muda wa mtu wa maongezi uwepo hewani mpaka tu pale yeye mwenyewe atakapoaamua kununua kifurushi cha internet?kuna aina ya ujanja ujanja m'baya sana mnaufanya.
3. Ninaamini 80% ya wanatumia mtandao wa Vodacom kama isingekua huduma ya m pesa yamkini mngekimbiwa na wateja wengi sana nikiwepo na mimi.
Jaribuni kubadilika
Sent using
Jamii Forums mobile app