Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Nimefurahi kuweza kuwafikia baadhi ya wadau wasilio wasilisha matatizo yao na kuwasaidia bure kabisa unangoja nini Vodacom IPO kwa ajili yako
 
Baada ya kumaliza majukumu yangu ya kikazi ngoja niwape taarifa.

Unapotaka kumtumia mtu pesa kwa njia ya Mpesa kwanza kabisa fanya mawasiliano na unayemtumia pili hakiki namba then tuma hela baada ya sekunde chache utapokea SMS ya kutuma pesa vilevile piga simu kwa muhusika kuthibitisha ikitokea umekosea usikimbilie kumpigia mtu ambaye umekosea ni kosa kubwa sana wahi kupiga simu Voda kuzuia hile pesa hakika itarudi
 
Carina umesahau hii ni jamii forum unajuaje labda Mimi nipo kwenye hiyo idara and I believe everything in here is confidential my aim is there help those in need what do you think they can do to me hack my info from jamii forum give me a break

Ha ha ha haaaa sawa Papiso, nimekukubali unaweza kweli ukawa kwenye hiyo idara
 
Ile Huduma ya kupokea SMS ya nani alikuwa amekutafuta sasa imefutwa
 
Mkuu mleta mada mbona tena kimya kingi ama maswali haya hayajibiki tena?
 
Carrina Mimi sipo Voda but I know how they operates kama una shida just say and I will help you out huuliza wadau watakwambia kuna wengine tushakuwa marafiki wakubwa humu ndani
 
Mambo niaje wadau..ebhana kwa anaejua hiki kifurushi cha voda cha bila kikomo kwa wiki nzima (TSH 12500) kinakuwa na GB ngapi? Na je kiko fasta kwa kudownload movies au magumashi?

Plss naomben mnisaidie kwa hilo na hata kama kuna kifurushi kingine cha ukweli cha download movies for cheaper price ntashukuru mkinifahamisha
 
2GB kwa speed ya juu, baada ya hapo speed inakua 30KBps mpaka tarehe ya mwisho




 
kifurushi hiki sio kizuri sana kwani speed hairidhishi ni pola uwe unaunga vifurushi vya kawaida tu.
 
Jamani mi mgeni hapa mwanza nimefika juzi tuu kutoka huko nitokapo, nimekuwa nashindwa hata kufanya mambo yangu kwenye net kwa kutumia mtandao wa voda, huwa una load hadi karaha, kwa wenyewe wa hapa ni mtandao gani kidogo upo fasta kwenye interner plse
 
Mods maomba uache uzi wangu huku huku.nilijiunga na unlimited bundle 1000 ya vodacom sasa kuna masharti ukitumia 1 gb speed inashushwa lakini nilitumia torrent kushusha 700 mb na nikatumiwa sms kwamba wanashusha speed kwakuwa 1gb imeisha.sasa nikijiunga hata cheka mpaka leo speed imepunguzwa mwanzo ilikuwa 5.2mbps lakini sasa 256 kbps mpka leo siku ya tano daah voda wezi
 
Hii ni kweli hata mimi imenitokea jana yani ni zaidi ya wizi
 
Hawa ndo zao,vocha inaisha hata kama hujapiga cm,kifurushi kikiisha hawakwambii unajkuta umekula salio,vfurushi usanii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…