Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Nimeshangazwa na utendaji wa Vodacom. Ni siku 40 zimepita tangu niwasilishe documents kupata till mpya zilizoibiwa, mpaka leo sijapata. Ttcl nilitumia dakika 8, in 24 hrs ikawa hewani.

Airtel nilitumia dakika 30, ndani ya saa 24 ikawa hewani. Tigo nilitumia dakika 20, nikapigiwa simu ndani ya saa 48 kuwa niwekee line kwenye simu ipo tayari.

Najuta na Vodacom!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vodacom ni janga kubwa kwa mawasiliano ya simu.
Ni kweli wanatoa huduma nzuri, lkn kununua vifurushi na muda wa maongezi ni wizi mtupu.

Juzi tarehe 2/4/2020 nilinunua kifurushi cha chuo, nikapewa na ofa ya dk 5 vodo to voda lakini kifurushi chenyewe sikupewa mpaka leo hii tar 4/4/2020.
Sasa hivi nimekubali hasara na nimebahatisha kupata kifurushi kingine ambacho nimenunua sasa hivi.
VODA angalieni, ikiwa mtakosa kuaminiwa na wateja wenu basi mjue kampuni itakuwa hatarini, na niseme mnaelekea kibaya.
Huwezi kupokea fedha za wateja, kisha usitoe huduma.
Na kibaya zaidi hata ile acces ya kuongea na mhudumu mmeiondoa, mnachofanya siyo wizi wa makusudi???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie mnazingua sana kwa sasa...mmebadili vigurushi ghafla tu april mosi.. vy mwezi mzima...na mkaweka vya bei naman hiyo...ukweli mmezingua sana...angalieni tena difference kubwa sana...kifurushi cha 30,000 mnatoa dk 500 kweli na gb 7...naamin mnaweza mkawa mmenote difference ya subscribers kwa vifurushi hasa vya mwezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Voda ni wezi na wanatoa huduma hovyo sana. Kifurushi cha chuo mwanzo kilikuwa 1500, unapata gb1+, kuna kipindi ghafla wakawa wananikata 2000 na kunipa gb1.2 na dk 150 v-v na dk 15, ghafla wakaanza nikata 3000 na kunipa gb1.2, dk 150 v-v na dk 10 mitandao yote. Mara wakarudi kwenye makato ya elf 2 na kunipa mb GB 1 na dk zao kama kawaida, sasa hivi kwa elf 2 wananipa mb 540, dk 150 v-v na dk 10 mitandao yote. Kwa kifupi wakati mwingine kutokana na ndugu, jamaa na rafiki zangu kuizoea hii namba kubafanya niendelee na huu mtandao,vinginevyo ningekuwa nishaangalia ustaarabu mwingine.
 
Tumefulia lakini tuachane na hayo boresheni bando zenu na muache kukata salio tukichelewa kujiunga maana mkiisha kata salio huwa hamuishi sababu za uongo na huwa hamrudishi haki zetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijataka kuanzisha Thread mpya, na Ku tweet.

Kwenye kifurushi cha Cheka 10,000 dk 1250 mnasema mitandao yote, nimenunu mnanipa dk 450 mitandao yote. 800 voda Voda. Huu ni wizi
 
Kwa kweli Voda hamjanitendea haki, yaani mmeizuia hela yangu toka Jumatano hadi leo, Pasaka mnataka nisheherekee vipi?

Kinachoniumiza tatizo ni la Agent wenu mwenyewe ambaye aliniruhusu nitoe hela wakati Cash hana.

Najua mmenikata ya kutolea lakini bado mnaing'ang'ania hela yangu, naomba mnirudishie niitumie kwenye pasaka. Nilitoa shilingi 110,000/= kwa agent mpumbavu Makambako mida ya saa Tisa unusu.

Sent using Smartika kitochi
 
Back
Top Bottom