Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Nilipiga huduma kwa wateja nikaulizwa ulishawahi kuripot account yako ifungwe nikwaambia hapana,
Wakaniambia niende vodashop nikatumia nauli
Nafika pale naambiwa kuna mtu ali riport ifungwe na isifunguliwe bila kupigiwa yeye na kaweka namba yake hapo, haya mpigieni hapatikani, basi nipeni namba hawataki kutoa namba!! Who are these if not Kima kama Kima??
 
Fanyeni mtu aweze kulipia kwa app za playstore automatically. Mpesa ya safaricom inahiyo huduma. Wakisema weka payment syastem kuwena option ya mpesa.
 
Hivi voda arusha mko wapi? Yaani olasiti mtandao wenu ni shida. Hasa upande wa data. Hebu fanyeni kitu,,tuone mabadiliko.
 
Nipo biharamulo kesho natupa laini yenu mmekuwa na tabia ikifika Saa moja jioni internet haifanyi kazi mpaka Saa tano usku Kila SKU sijajua lengo lenu ni nini mpaka sasa au mnataka tunaotoka makazini tustumie data zetu maana Saa tano mtu umeshalala kwaiyo muda wa kifurushi ukifjka mtu hujatumia data mpaka muda wa kuisha kinafika kesho natupa laini yenu na naenda kuifuta kabisa yangu na ya mke wangu
 
Kwa kweli naomba Vodacom muwafikirie Wateja wanaojiunga vifurushi mara kwa Mara wawe wanapunguziwa gharama na Sio kuongezewa gharama kama mnavofanya saizi!!!!!! HILO NDIO OMBI LANGU
 
Mnachofanya ni sawa na MTU mwenye Duka anampandishia Bei mteja mkuu sababu ananunua bidhaa zaidi ya wengine.

Wakati kiuhalisia angethaminiwa kwa kupunguziwa gharama na kupata offer zaidi.
 
Jamani ,jamani ,jamani.
Mbona katangazia Zanzibar? Ingekuwa enzi za Mwendazake,angetangazia Chato?
 
Huduma ya customer service ya voda ni mbovu kuliko maelezo, mtu unapiga simu umepoteza simu unapiga wafunge line eti wanakupa namba ya WhatsApp mchat au namba ya kawaida, huko nako hakuna msaada, si uhuni tu huu
 
Fanyeni mtu aweze kulipia kwa app za playstore automatically. Mpesa ya safaricom inahiyo huduma. Wakisema weka payment syastem kuwena option ya mpesa.
Siku mkipoteza pesa ndio ntajua umuhimu wa huduma hiyo..nilishawai kutuma laki 6 kimakosa nikawai na pesa yangu ikarudi isingekuwa hivyo pesa ingetolewa
 
Siku mkipoteza pesa ndio ntajua umuhimu wa huduma hiyo..nilishawai kutuma laki 6 kimakosa nikawai na pesa yangu ikarudi isingekuwa hivyo pesa ingetolewa
Kwani hawawezi kuzuia huduma ya M-pesa kwa laini husika bila kuifungia kabisa? Mbona baadhi ya mitandao wanakufungia kisha wanakupigia simu kukuekewesha kilichotokea? Unafungaje laini ya mtu moja kwa moja bila kumsikiliza? Kama kauza bidhaa je?!
 
Hii menu mpya mliyotoa ya kuset seed ya internet ina faida na hasara gani?
 
vodacom ni lini nitapata huduma ya mikopo ya songesha na m pawa? naona nafanya miamala sana.. 0752495777
 
Simu yangu Infinx Hot 9 Play X680. Inasoma mwisho 3G haisomi H+. Line ni Voda 4G. Msaada tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…