Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Kwa nn mnasumbua kutuma ma sms ya matangazo kwenye lain zetu
Tena hawajali muda hata usiku wa manane wanatuma tu simu ipo huko hunampango nayo inatumwa msg eti umefikia kikomo sijui mara nini sasa jichanganye uweke vocha sasa unatumiwa ujumbe hadi 4 za uthibitisho na mchnganuo tu
 
Bundle zenu hovyo kabisa hasa kipengele cha MB,na mtakimbiwa na watu wengi sn kwenda Tigo,airtel n.k
 
VODCOM NI WEZI WAKUBWA

Yaani nyie na makampuni zingine mna tabia ya kuunga watu kwa huduma ambazo hawajaomba.

Mnawatumia ujumbe za miziki, mapenzi, michezo, uganga, na maujinga kibao. Na mkikata hizo pesa ni kimya kimya wala hakuna SMS hivyo mteja hawezi kushtuka. Mnapata pesa kitapeli ambazo ni sawa na wizi.

Mtu akilalamika mnajibu ulijiunga mwenyewe wakati sio kweli. Mbaya zaidi mtu anasema ondoeni huduma zote hizo lakini mnakuwa na vichwa vigumu na kumpotezea. Mtu anatuma sms za kujiondoa lakini bado anakatwa.

Mnatengeneza billion za pesa kila siku ambazo ni sawa na utapeli na wizi.

Namalizia ku file up tutakutana TCRA na mahakama ya kimataifa, maana mnaona watanzania ni vilaza
 
Vodacom Tanzania hamjambo?

Naomba mnipe ufafanuzi kidogo. Ni sawa tunapenda muwe mnatoa update za app.

Leo nlikua na haraka kidogo kutokana na kuzoea app yenu ya Vodacom kununua bundle eneo ambalo mmeweka ile internet Supa likawa limebadilika ikanifanya ninunue kifurushi tofauti, Mnakiita bundle za silabu.

Shida sio hicho kifurushi bali ni hakijaelezwa matumizi yakee na nmetafuta mtandaoni hata hakipo.

Mmenilazimu ninunue kingine, Nmeandika kuhitaji maelezo hicho kifurushi cha bundle za silabu nakitumia wapi?

Screenshot_20221215-155719.jpg
 
1GB ya Safaricom ni kama 7GB ya Vodacom Tanzania na uzuri zaidi its in the same phone. Yaani itumie ukiwa Nairobi kisha itumie ukiwa Dar es Salaam
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

  • Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
  • Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
  • Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
  • Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
  • Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Tangu jumamosi Jioni 21 January 2023 kasi ya internet ilishuka ghafla kwenye eneo la Chigongwe ktk halmashauri ya Jiji la Dodoma. Maeneo mengine yaliyo athirika ni Kigwe na Msembeta.

Sijui mko wapi.
 
Wengine ndio wezi kushinda hawa voda mitandao mingine ni balaa iwe salio au acaunt
 
TCRA wana mtindo wa kukalia malalmiko ikipita wiki mbili hawakujibu wakilisha malalamiko kwenye tume yaa ushindani ofisi zao ziko Ubungo.
TCRA sio kazi yao malalamiko kuhusu wizi wa pesa mitandaoni hayo makosa hushughulikiwa police na police ndio walishughulikie na sio TCRA
 
Kuna kipindi nikitaka kuingia Facebook naambiwa wao Facebook wana haki ya kuchukua namba yangu ya simu kutoka kwenu vodacom kwa sababu mimi na nyie vodacom tuna makubaliano kwamba nyie mtaigawa namba yangu kwa Facebook. Sijawahi popote kufanya makubaliano na nyie kwamba mtagawa namba yangu. Hii imekaaje?
 
Kuna kipindi nikitaka kuingia Facebook naambiwa wao Facebook wana haki ya kuchukua namba yangu ya simu kutoka kwenu vodacom kwa sababu mimi na nyie vodacom tuna makubaliano kwamba nyie mtaigawa namba yangu kwa Facebook. Sijawahi popote kufanya makubaliano na nyie kwamba mtagawa namba yangu. Hii imekaaje?

Unapokua unajiunga facebook unaambiwa je utapenda namba yako ya simu itumiwe na facebook ukijibu ndio itatumika sasa apo kosa liko wapi tatizo wabongo wengi atusomi na izo mitandao za kijamii tunafunguliwa
 
kastama kea wa kampuni ya HALOTEL 13/2/2023 saa 7:35 usiku wanatuma sms yenye kichwa cha UTAPELI. Maelezo yake sasa "katika msimu huu wa valentine tunakushukuru kwa kutumia huduma zetu. Tunatoa surprise kwa wateja wetu watakao tembelea maduka yetu na kupata huduma. Asante!" Ila kwa voda mnajitahidi kidogo
 
Back
Top Bottom