Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Hii kali FCC kama mods wa JF. Utapigwa ban. Pole sana....[/QUOTE]

Hah! Labda mods watumie hasira, lakini kma wanakubali challange basi sina kosa hapo. Ni kweli wamekua wakifuta threads zinahusu malalamiko ya vodacom
 
Hapo ndipo penye tatizo. Hicho unachoambiwa ni unlimited, ni kifurushi cha ukubwa fulani, say 1Gb. Zikiisha kasi ya mtandao inakuwa ya chini sana sawa na hakuna. Kwanini watudanganye kwamba ni unlimited? Ndio wizi wenyewe.
 
Yaani Voda wanaboa sana mwenyewe huwa nanunua Bundle kufumba na kufumbua limeisha wizi mtupu
 
★★★★★ Habari!!
Vodacom Mnaonaje Katika MENU Yenu Ya
*149*01# Muongeze CHAGUO La "Kurudi
Nyuma" Ili Kumrahisishia Mteja Kutoanza Tena
Upya Kabisa, Baada Ya Kufika Hatua Ya Karibu
Na Mwisho Kuchagua Hitaji Alitakalo Na
Kugundua Kakosea Muamala?
Naamini Ombi Hili Litashughulikiwa.
 
Vodacom CS Support njoo huku!
 
Last edited by a moderator:
Ahsante kwa ushauri bampami, tayari wataalamu wetu wanashughulikia suala hili. Ahsante sana
 
Last edited by a moderator:
Kwa wiki nzima nimekuwa nikinunua vifurushi vya Cheka bombastiki lakini Hii imezidi.
Jana nimenunu Kifurushi cha kutosha na sina matumizi ya kukimaliza hata Kwa Siku tano.

Hongera!Umenunua Dakika 400 za kupiga mitandao yote,SMS 1500 mitandao yote TZ na 1024MB zitumike hadi 2014-08-10.Piga *147# kujua salio.

Na Leo mchana wananitumia kwamba kimekwisha.

Ndugu mteja, kifurushi chako cha Cheka kimekwisha. Furahia dk 30 kwa Tsh.495 tu saa 24.Kununua piga *149*01# na chagua Cheka Zogo.

Nimempigia customer care akajitambulisha Kwa jima La Ally hakuwa na msaada wa aina yoyote..

Goodbye Vodacom.
 
Mhhh!!!! nilizani ni mimi tu, kumbe wengi basi hii ndiyo utaratibu wao tutauzoea tu.
 
Kwani hamuwajui wenye hisa kwenye hiyo kampuni?

Kumbukeni mwakani tunahitaji viongozi wapya na ni lazima kutumia gharama ili tupate ushindi wa kishindo.
 
Kimekwisha yaani both bundle na dakika au bundle zimekwisha ila dakika zako zipo? kama ni bundle hiyo hata mie kila siku huwa inanikuta ila nilichogundua zile bundle huwa ni kwa ajili ya internet kwa kutumia simu ila ukiweka kwenye computer sometime unatumia muda mrefu ila wakati wingine ndani ya saa moja kimekwisha. Ukitaka kutumia muda mrefu nunua kabisa bundle for internet hiyo inachukua muda mrefu. Kiukweli wanaudhi ila kuna mazingira ni mitandao yote hufanya hivi maana mie nina ninatumia mitandao mitatu tofauti leo unakuta huyu yupo poa kesho unashangaa anakorofisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…