Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Sijui tutaponea wapi?Hakuna mtandao hata mmoja usio na ujanjaujanja huu.Mi natumia yote ulaghai wa aina km hiyo uko palepale.


Haya makampuni ya mitandao yamekuwa sawa kabisa na wale wanaojifanya wanauza simu kumbe ndani wameweka sabuni
 
Mkuu tzbiz,

I second you, hivi karibuni kuwekuwa na wizi wa ajabu Vodacom kwa wateja, binafsi nimekuwa nikijiunga na vifurushi vya kila siku kwa muda sasa, na matumizi hayajaongezeka lakini hivi karibu(wiki tatu sasa) kila nikijiunga within no time naambiwa "muda/ Salio wa kifurushi chako umekwisha" ninejaribu kujiunga vifurusgi vyote viwili vya wiki pamoja na vile vya siku kuthibitisha lakini bado 'mchezo mchafu' ni ule ule.


Vodacom you have to step up.
 
Last edited by a moderator:
Tumia Zantel ndio baba lao, hata km hujajiunga unapiga mitandao yotee bila shida
 
siku zote mitandao ambayo haina watumiaji wengi ndo inakua na huduma bora. fanya utafiti ni mitandao gan isiyona watu weng hapa tz
 
Habari Skype mafundi wetu wanajitahidi kutatua tatizo mara tu linapotokea, na katika hili tumefanikisha kulirekesha kwa sasa.
 
Last edited by a moderator:
Habari Skype mafundi wetu wanajitahidi kutatua tatizo mara tu linapotokea, na katika hili tumefanikisha kulirekesha kwa sasa.

Hongereni kama kweli mmefanikiwa kutatua tatizo hilo ila niwatakie kila laheri na wateja wenu, mimi nimewaogopeni sana na sina uwezo wa kuwalazimisha mfanye ninavyotaka mimi ili nifurahie huduma zenu. Kazi njema.
 

Si kweli KWA wiki mbili mfululizo nimepata Hilo tatizo, NA hela inakwenda
 
yaani mimi kilichonifanya nihame vodacom ni tatizo la kifurushi

ukijiunga una sh 550 unaambiwa hauna salio la kutosha hadi ukimbie tena dukani ukaongeza jero ili ujiunge na kifurush cha mia 500
 
yaani mimi kilichonifanya nihame vodacom ni tatizo la kifurushi

ukijiunga una sh 550 unaambiwa hauna salio la kutosha hadi ukimbie tena dukani ukaongeza jero ili ujiunge na kifurush cha mia 500

Na kifurushi kikiisha wanakata salio lote kabla ya kuanza kukutumia miujumbe eti kifurushi kimeisha. Ni watu wa maajabu sana.
 

bora umekuja mkuu, sijui siku izi mmekuaje, jana nimenunua kifurushi kwa ajili ya modem yangu, kwa ajili ya wyf na kwa ajili ya simu yangu ikiwa ni pamoja na dakika na sms, simu ya wyf ilikuwa na data ON, haikukaa nusu saa kikakata, nimechomeka Modem kudownlod Whatsapp app yenye MB 15 tu ila bunndle ikikata apo apo. Nimebaki na bundle ya simu yangu tu, nimeamua kuipa adhabu line yangu, ntakuwa nachomoa line ya simu ili nitumie kifurushi icho tu wiki nzima mpaka kiishe.

COMPLAIN 2
VodaCom siku izi mnakuwa wasanii, nilinunua simu kwenye duka lenu moja/naliifadhi, izo smartphone nilichukua mbili, moja iko poa ila nyingine Vodafone 875 black ni kimeo, ukipiga simu inakata netowrk apo apo, niliporudisha simu ilikuwa kimbembe kunielewa kuwa network ni mgogoro, bahati nzuri simu ikaita niko mbele ya maafisa wenu ikakata na kuandika EMERGENCE CALLS ONLY, apo ndo wakanielewa ila baada ya kutumia energy kuuubwa!!

Simu wakasema niwaachie ili irudishwe then watanipa jibu, wiki ya pili sasa kimya, yani najipanga nikirudi patachimbika,kwa nini mnazingua ivo?? Na sitakubali simu ile ile kama mmeenda kuirekebisha kama kuchomelea network Ic, nimenote specifications pembeni ikirudi ile kwa kweli sitawaelewa, pia mjue mtu akinunua kitu kibofu dawa ni kumpa kipya si kumzungusha, pia mimi sikununua simu makao makuu, iweje mniambie nisubiri ipelekwe makao makuu,nimeweka line pembeni nikisubiri simu wiki kibao............rekebisha aisee, otherwise nitakuwa balozi mbaya wa Vodacom!!!
 
Last edited by a moderator:

Mpaka sasa voda hawafai, wana jeuri, kiburi na dharau hasa huduma kwa wateja.
 
Mpaka sasa voda hawafai, wana jeuri, kiburi na dharau hasa huduma kwa wateja.

kweli mkuu, siku nilipopiga simu mdada kanibishia then anasema...nona unielewi,asante kwa kupga vodacom, akakata simu...nlishangaa sana
 
kweli mkuu, siku nilipopiga simu mdada kanibishia then anasema...nona unielewi,asante kwa kupga vodacom, akakata simu...nlishangaa sana

Hapa atakuja mr Vodacom Tanzania akupige Kiswahili weee mpaka ushangae. Ukimwambia habari za huduma kwa wateja anajifanya kupotezea na badala yake anakuja na habari za mafundi wao. Mi nimeamua kumnyamazia tu maana kampeni yangu ya kuwahamasisha ndugu, jamaa na marafiki wahame huko imefikia 76% mpaka sasa. Sipigizani kelele tena na huduma kwa wateja wa voda, niko mtandao wenye kujali shida za wateja.
 
Last edited by a moderator:
wanaanza kuiga style za safaricom. kwanza kifurushi cha 899 kilikua na 300 MB sasa ghafla wanashusha kuwa 100 MB . yaani punguzo la asilimia 200,kwa nini ,wanatumia ukweli hapo?
 
Kwa sababu Tanzania hakuna regulator ambaye anaweza kuwapiga faini, hii nchi ipo ipo tu watu wanafanya wanavyotaka na serikali dhaifu ina wacha walipa kodi wake wanateketea mbele ya Majambazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…