bora umekuja mkuu, sijui siku izi mmekuaje, jana nimenunua kifurushi kwa ajili ya modem yangu, kwa ajili ya wyf na kwa ajili ya simu yangu ikiwa ni pamoja na dakika na sms, simu ya wyf ilikuwa na data ON, haikukaa nusu saa kikakata, nimechomeka Modem kudownlod Whatsapp app yenye MB 15 tu ila bunndle ikikata apo apo. Nimebaki na bundle ya simu yangu tu, nimeamua kuipa adhabu line yangu, ntakuwa nachomoa line ya simu ili nitumie kifurushi icho tu wiki nzima mpaka kiishe.
COMPLAIN 2
VodaCom siku izi mnakuwa wasanii, nilinunua simu kwenye duka lenu moja/naliifadhi, izo smartphone nilichukua mbili, moja iko poa ila nyingine Vodafone 875 black ni kimeo, ukipiga simu inakata netowrk apo apo, niliporudisha simu ilikuwa kimbembe kunielewa kuwa network ni mgogoro, bahati nzuri simu ikaita niko mbele ya maafisa wenu ikakata na kuandika EMERGENCE CALLS ONLY, apo ndo wakanielewa ila baada ya kutumia energy kuuubwa!!
Simu wakasema niwaachie ili irudishwe then watanipa jibu, wiki ya pili sasa kimya, yani najipanga nikirudi patachimbika,kwa nini mnazingua ivo?? Na sitakubali simu ile ile kama mmeenda kuirekebisha kama kuchomelea network Ic, nimenote specifications pembeni ikirudi ile kwa kweli sitawaelewa, pia mjue mtu akinunua kitu kibofu dawa ni kumpa kipya si kumzungusha, pia mimi sikununua simu makao makuu, iweje mniambie nisubiri ipelekwe makao makuu,nimeweka line pembeni nikisubiri simu wiki kibao............rekebisha aisee, otherwise nitakuwa balozi mbaya wa Vodacom!!!