Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Nina miezi sasa,kila nikipiga huduma kwa wateja umefikia ukomo kupiga simu huduma kwa wateja,wanataka nitumie namba ya kulipia,nayo nawapigia sipati ufumbuzi,na ukiacha salio wanachukua!
Airtel nao majanga mwezi wa tatu sasa nikitaka huduma ya airtel Yatosha Noma(airtel to Airtel) inagoma ,ila kifurushi cha airtel kwenda mitandao yote inakubali,ambayo sihitaji,nawapigia CC wanataka tsh 60 kuungoea na mhudumu,nakubali wananikata...ila mhudumu hana uwezo wowote...hii ni tatatizo la shirika letu la Umma kufa TTCL wangekua wamejiamilisha mambo yangekua poa
 

Hii ndo Tanzania bwana, yaani kila kitu kiko kwenye auto pilot kinajiendea tu, marubani wote wamekata mbonji ila tutafika tu.

Vodacom kazi ni kwako
Airtel baba lao
Tigo kabaaang
TTCL ilishajifia
sijui twende wapi?
 
Vodacom majanga,, ya kwangu nimeacha kuiwekea vocha mwezi sasa na sina mpango kabisa. Aitel ndo mpango mzima najirusha cha wiki natumia saafii mpk vinakutana.
 
Vodacom ni majanga kupindua,with worst customer care ever
 
Si kweli KWA wiki mbili mfululizo nimepata Hilo tatizo, NA hela inakwenda
Habari Bijou tafadhali tutumie namba yako ya simu tufuatilie suala hili katika mifumo yetu. Ni kwamba hakuna kifurushi cha mteja kinaminywa/punguzwa.
 
Last edited by a moderator:
Habari Gsana kuhusiana na masuala haya tafadhali tutumie namba ya simu kwa mawasiliano zaidi.
 
Last edited by a moderator:
kweli mkuu, siku nilipopiga simu mdada kanibishia then anasema...nona unielewi,asante kwa kupga vodacom, akakata simu...nlishangaa sana

Wakuu maswala haya yote yanazingatiwa na kuchukuliwa hatua ikiwemo kuwawajibisha watoa huduma wenye kauli zisizostahili kwasababu simu zote zinarekodiwa. Ahsanteni
 

Habari tzbiz pole sana kwa suala hili na tunaomba kufafanua namna Happy Hour inavyokuwa. Ni kwamba huduma hii inakupa dakika 60 kupiga simu kuanzia muda uliojiunga, hii inaamanisha kuwa ukijiunga saa 2 asubuhi huduma yako itakwisha dakika 60 kutoka saa 2 asubuhi kwa maana ya saa 3. Ukipiga simu saa 2 dk 40 unakuwa umebakiza dakika 20 kufikia mwisho wa kifurushi chako.

Kwahiyo kifurushi ulichojiunga saa 1:30 cha dakika 20 ilikuwa ni sahihi kupokea ujumbe kuwa kifurushi chako kimekwisha dakika 30 baada ya kujiunga.Tunaimani maelezo haya yamefafanua vyema suala hili
 
Last edited by a moderator:

Habari hippocratessocrates tafadhali tutumie namba ya simu kwa mawasiliano zaidi.
 
Habari Gsana kuhusiana na masuala haya tafadhali tutumie namba ya simu kwa mawasiliano zaidi.

mkuu sisi apa jf members ni segment ndogo sana tunawakilisha jamii, sasa namba za simu utachukua ngapi? Ningekushauri uchukue complains zote zfanyiwe kazi then jamii itaona mrejesho ila utamaliza tatizo langu then kesho kwa mwingine, hope unanielewa mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Habari Gsana kuhusiana na masuala haya tafadhali tutumie namba ya simu kwa mawasiliano zaidi.

sawa mkuu ila nakuomba solve ili tatizo, mtu anakuja kununua simu, anapewa simu mbovu like touch screen, network issue, au kujizima, anairudisha then anaambiwa hakuna simu kupewa nyingine mpaka simu ipelekwe makao makuu then anaambiwa asubirie simu nyingine au jibu toka head office, iyo ni biashara gani mkuu??

Nadhani inafaa mjipange au pia uzeni simu zilizokuwa tested tayari sio kumuacha mtu akagundue tatizo mbele ya safari, inapunduza confidence na reputation ya kampuni.

Nasubiria simu yangu kwanza, isipoletwa au kiswahili kingine then ndo ntarudi kwako...
 
Last edited by a moderator:
Wakuu maswala haya yote yanazingatiwa na kuchukuliwa hatua ikiwemo kuwawajibisha watoa huduma wenye kauli zisizostahili kwasababu simu zote zinarekodiwa. Ahsanteni
Kwa sasa naiogopa voda hakuna mfano, itoshe tu kusema nimenyosha mikono.
 
Vodacom ni wezi sana yaani hiyo cheka bombastic kifurushi muda wa maongezi umepunguzwa lakini hela ya manunuzi ni Ile ile.Kinachoniudhi kupitia kiasi ni mb yaani ukiangalia video hata sek 30 unaambiwa kifurushi cha mb kimeisha yaani mnakera sana.Pia wahudumu wa voda ni wezi na matapeli kama pale mlimani city nishawahi kutapeliwa tshs 40000
 
Wamekuwa wakiiba hela kwenye account yangu, mfano jana sh. 500 ikapotea bila sababu.
Leo tena sh. 132 sijui imeenda wapi? Mnatia aibu sana vodacom.
Kuna thread nyingi sana humu, zikiwalalamikia voda lakini mbona hamjirekebishi?? Angrrrrrrr....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…