Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

.... nimeweka kiasi cha tsh 3500 nimejiunga bundle ya 3499 ya wiki ili nipate dk60 na mb200 chakushangaza napata ujumbe.

Salio langu halitoshi kujiunga....nikicheki salio *102# naona nina 3504.99 sasa nauliza inakuwaje nyie vodacom....
Umeibiwa kiasi gani? Maana kwa hizo namba zako hapo juu, ni kama vile salio limeongezeka kwa sh 4.99. Au kuna kitu sijaelewa?
 
Wamekuwa wakiiba hela kwenye account yangu, mfano jana sh. 500 ikapotea bila sababu.
Leo tena sh. 132 sijui imeenda wapi? Mnatia aibu sana vodacom.
Kuna thread nyingi sana humu, zikiwalalamikia voda lakini mbona hamjirekebishi?? Angrrrrrrr....

Habari Crimea tafadhali wasiliana nasi PM kwa msaada zaidi. Hakuna pesa ya mteja inayoibwa ndugu mteja. Ahsante
 
Alafu mnakera sana nyie,meseji unatuma leo inafika kesho..kama hamuwezi kutoa huduma bora muache tujue hampo kabisa...
Pengine kungekua na utaratibu wa kuwatoza faini kutokana na usumbufu mngeshika adabu na kujua nini mnakifanya.

Habari Platnam, tafadhali tutumie taarifa zifuatazo PM kwa msaada zaidi.
Namba ya mtumaji
Namba ya mpokeaji
Muda ujumbe uliotumwa
 
Last edited by a moderator:

Wanakera Sana.na wanapunguza mda wa maongezi na net bila taarifa.kwa tunavoelekea watatupa MB 100 kwa 3499.wizi mtupu
 
Sasa wewe jitie wa.zimu uhamie AIRTEL utajuta kununua simu. jitahidi ubaki VODACOM au sana sana hamia mtandao wa matuc yaani. 0713. huku spidi iko nyuma ya VODACOM ila usihamie airtel hata iweje.

Airtel wana nini nao?
 
Voda wanakera sana aisee, tena ni wizi wa wazi wazi, jana usiku nimeweka salio la 2000, then nikaactivate bandle ya 500tsh ya 200 MB, hata kufungua google ilichukua zaidi ya nusu saa. Baada ya kutuma mail nikatoa modem, naangalia salio nakutana na sh 0, na bandle nayo ni 0...f*ck.

Sent from my iPhone using JamiiForums
nimewahi kuweka 10,000 usiku kama saa 3 hivi ili asubuhi nijiunge bando, sikupiga wala kutuma sms hata moja. Asubuhi naambiwa ten yangu imeisha. Nikaamua sitaki tena mambo ya voda zaidi sana napokea simu tu
 
Habari Platnam, tafadhali tutumie taarifa zifuatazo PM kwa msaada zaidi.
Namba ya mtumaji
Namba ya mpokeaji
Muda ujumbe uliotumwa

Ndugu yangu mtachukua namba za watumiaji wa vodacom wangapi.? Haya malalamiko ni indication ya kwamba huduma zenu ni mbovu kupita maelezo. hata tukitoa namba zetu kuwapa, mtanitatulia tatizo mimi tuu ambaye nimepita JF, vipi wale wengine ambao hata smartphone ya kuingia mtandaoni hawamiliki.?

Hapa issue sio kutoa namba na kuwapatia, hapa issue ni kufanya auditing ya system yenu upya na kuangalia perfomance yake. Mimi binafsi nimeiweka line yangu ya vodacom kabatini mpaka pale mtakaporekebisha huduma zenu, na nasikitika kusema kuwa nishawashawishi wateja wenu zaidi ya watano wanaotumia vodacom kuhama vodacom, na nitaendelea kushawishi wengine mpaka pale mtakapojirekebisha.
 
Last edited by a moderator:
Leo asbh nimeweka kiasi cha tsh 3500 nimejiunga bundle ya 3499 ya wiki ili nipate dk60 na mb200 chakushangaza napata ujumbe.

Salio langu halitoshi kujiunga....nikicheki salio *102# naona nina 3504.99 sasa nauliza inakuwaje nyie vodacom...

KUANZIA LEO NAHAMA KABISAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA NAHAMIA KULE TIGO MINI KABANG SITANUNUNUA TENA VODA YENU.

TCRA MNAFANYA KAZI GANI JAMANI...JUZI NAPO WAMENIIBIA 500 SIJAPIGA WALA KUPOKEA WALA KUTUMA UJUMBE NA SIMU YANGU SIO SMARTPHONE.
Habari Kisendi, tunaomba namba ya simu PM kwa msaada zaidi tafadhali.
 
afu we mr/miss voda tunaomba mrudishe vifurushi vya internet km mwanzoa nawahama kuanzia ijumaa.

Mimi nimeshama, yani kila siku wanajibadilishia vifurushi kama wao ndo wanatununulia vocha.
 
Kwa wiki nzima nimekuwa nikinunua vifurushi vya Cheka bombastiki lakini Hii imezidi.
Jana nimenunu Kifurushi cha kutosha na sina matumizi ya kukimaliza hata Kwa Siku tano.

Hongera!Umenunua Dakika 400 za kupiga mitandao yote,SMS 1500 mitandao yote TZ na 1024MB zitumike hadi 2014-08-10.Piga *147# kujua salio.

Na Leo mchana wananitumia kwamba kimekwisha.

Ndugu mteja, kifurushi chako cha Cheka kimekwisha. Furahia dk 30 kwa Tsh.495 tu saa 24.Kununua piga *149*01# na chagua Cheka Zogo.

Nimempigia customer care akajitambulisha Kwa jima La Ally hakuwa na msaada wa aina yoyote..

Goodbye Vodacom.

voda ni wizi mtupu, nilikuwa na kawaida ya kununua vifurushi vya internet tangu mwezi huu uanze nime kumbana na tatizo la mtandao kuwa limited, mpaka sasa hivi nime hamia airtel
 
Kwa wiki nzima nimekuwa nikinunua vifurushi vya Cheka bombastiki lakini Hii imezidi.
Jana nimenunu Kifurushi cha kutosha na sina matumizi ya kukimaliza hata Kwa Siku tano.

Hongera!Umenunua Dakika 400 za kupiga mitandao yote,SMS 1500 mitandao yote TZ na 1024MB zitumike hadi 2014-08-10.Piga *147# kujua salio.

Na Leo mchana wananitumia kwamba kimekwisha.

Ndugu mteja, kifurushi chako cha Cheka kimekwisha. Furahia dk 30 kwa Tsh.495 tu saa 24.Kununua piga *149*01# na chagua Cheka Zogo.

Nimempigia customer care akajitambulisha Kwa jima La Ally hakuwa na msaada wa aina yoyote..

Goodbye Vodacom.

Mimi nilishahama siku nyingi kwa sababu ushenzi huo huo!
 
Tutumie namba ya simu na tuambie lini ulipata tatizo hili. Ahsante

Sipendi kupigiwa simu na mtandao mnanisisitiza nichague wimbo niupendao inanikera sana. Mi nadhani mngetupigia tutoe maoni kuhusu matatizo na kero tunazopata kupitia huduma hapo ingekuwa bora katika kuboresha huduma zenu. Mfano nikijiunga kifurushi kisicho na kikomo speed ya internet inapungua kasi nikijiunga hata mb 200 mtandao unakuwa shwari au siku nyingine mtandao wakati wa mchana unazingua ikifika usiku unatulia.
 
Mhhh!!!! nilizani ni mimi tu, kumbe wengi basi hii ndiyo utaratibu wao tutauzoea tu.

Ndio wawekezaji wetu hao

tunachangisha pesa za kampeni

Kwani hamuwajui wenye hisa kwenye hiyo kampuni?

Kumbukeni mwakani tunahitaji viongozi wapya na ni lazima kutumia gharama ili tupate ushindi wa kishindo.
Samahani @Vodacom CS Support, nilikusanya hizi comments nikuite utoe maelezo ila nikagundua kwamba umeshajibu.
 
Vodacom Tanzania jitahidi mfunge mitandao ya 3G nchi nzima kwani walio mijini baadhi ndo wanafaidi mtandao huo. Believe or not nilienda wilaya ya ngara kuna maeneo baadhi lain ya voda kwenye mtandao inasoma Rwanda Cell au tigo ya Rwanda. Unaweza kukaa hewani siku nzima kila anaye kupigia haupatikani. Hata ikisoma network ya Vodacom internet utakesha hata ujumbe wa whatsapp wa maneno utajaribu mara nyingi sana ndo utaenda.
Hiyo kauli mbiu ya kazi ni kwako mnatukomoa kwelikweli.
 
mi nilishahama cku nyingi, kwa sasa dada anakusanya fedha za kumsaidia kaka kwnye kampeni za kura ya maoni.
 
Kwa wiki nzima nimekuwa nikinunua vifurushi vya Cheka bombastiki lakini Hii imezidi.
Jana nimenunu Kifurushi cha kutosha na sina matumizi ya kukimaliza hata Kwa Siku tano.

Hongera!Umenunua Dakika 400 za kupiga mitandao yote,SMS 1500 mitandao yote TZ na 1024MB zitumike hadi 2014-08-10.Piga *147# kujua salio.

Na Leo mchana wananitumia kwamba kimekwisha.

Ndugu mteja, kifurushi chako cha Cheka kimekwisha. Furahia dk 30 kwa Tsh.495 tu saa 24.Kununua piga *149*01# na chagua Cheka Zogo.

Nimempigia customer care akajitambulisha Kwa jima La Ally hakuwa na msaada wa aina yoyote..

Goodbye Vodacom.

Bora wewe, nimejiunga na kifurushi cha 1999, sijapiga hata simu mmoja, sijatuma hats SMS moja lakini nimetumiwa SMS ( Mara tu baada ya kumpigia mtu ambaye hata hiyo namba yake ilikuwa inatumika) kuwa kifurushi chako kimeisha! Nilipojaribu kuwapigia customer service (na sijapiga namba 100 for the past three months) nikaambiwa kuwa "Ndugu mteja, umefikia kikomo cha kupiga siku BURE mwezi huu kwenda Vodacom huduma Kwa wateja. Tafadhali pigs nam a 15366 Kwa Tsh. 100 tu Kwa kila siku. Ahsante"

Kuanzia Leo, ninaanza kuwapa promo Airtel, Tigo, Zantel na TTCL Kwa mtu nitakaemuona tena bure!
 
Back
Top Bottom