Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)


Ahsante Denjo, unaweza kupitia hapa https://www.vodacom.co.tz/mpesa/mpawa/faq kufahamu kuhusu suala lako. Usisite kuwasiliana nasi endapo utahitaji msaada zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana, huduma hii haiunganishwi moja kwa moja. Tafadhali mshauri atume SMS yenye neno ONDOA kwenda 15577. Ahsante
 
Last edited by a moderator:
Habari mputika, tafadhali fafanua suala hili.

nikwamba laini za uwakala zikipotea au kuharibika huwa zana unaweza kurenew baada ya kufata taratibu zote sasa huyo dada aliyepo hapo kwenye hicho kitengo ndo kikwazo anasumbua yaani anachelewesha hilo zoezi pasipo sababu za msingi mwanzo ilikuwa inachukua siku 3 mpaka 4 ila sasa ni hovyo muda wote huo kazi hazifanyiki maana lain hakuna
 
Last edited by a moderator:
Honestly speaking, nawapongeza voda kwa ujasiri wa ku-deal na changamoto hizi live ukizingatia wahanga wa matatizo haya ni wakali sana of coz kwa kuwa wanadhulumiwa. Sasa huko tigo pia matatizo haya ni makubwa zaidi hadi mimi nilihamishia huduma zangu zote voda ila saaa na wao ndo haooo wameanza. Anyway nawapongza kwa maana ujasiri huu ni dalili kwamba wana nia ya kujirekebisha. Pliz team voda. Acheni kutoa majibu rahisi wakati watu wanaumia. Chukueni hatua mara moja kwa hao wapigaji. Kuwashtaki pengine ni mlolongo mkubwa, so to cut it short fire them
 
Ushauri wangu ni kuhusu menu ya Mpesa kwa mawakala.

Ilivyo sasa hivi jina la mteja anayetumiwa pesa huonekana baada ya muamala kukamilika.

Hii tatizo lake ni kuwa, kama wakala akikosea kuingiza kiusahihi namba ya mteja fedha zitakwenda kwa mtu mwingine na utaratibu wa kubatilisha unakuwa mrefu.

Kwa nini Vodacom msitumie utaratibu kama wa Tigo na Airtel ambao huonyesha jina la anayetumiwa pesa kabla wakala hajakamilisha muamala?

Huu ni ushauri tu; otherwise huduma zenu za Mpesa ni za kuridhisha sana!
 
Vodacom Tanzania hivi mtu akifariki hela zake kwenye M PESA zinapelekwa wapi na ni shilingi ngapi zimepatikana ambazo hazina mwenyewe na zimefanyiwa nini?
 
Last edited by a moderator:
Nyie vodacom, mimi nimejiunga na mpawa lakin nashindwa kuingiza salio kubwa kwa sababu kila nikiulizia chochote kuhusu mpawa naambiwa niende kny maduka yenu na kitambulisho, na nimeshakwenda pale Samora NHC nikapewa form na kuijaza details zangu, nikaambiwa nisubiri baada ya siku 5 ndio nianze kuitumia hiyo huduma ya mpawa, lakini hadi hv sasa sijafanikiwa na ni wiki km 3 au 4 zimepita, sasa nyie mtanisaidia vp ili nianze kuweka akiba? No yangu ni 0757 980 448.
 
sasa mbn mnaniongezea maswaliiii na hamjanijibuu exactly what I have asked jmn naomba unielezee hapa kunidirect kwa link hio sio kunipa majibu of what nimeuliza na ninataka kujua maana huko piaa nmeona chenga tu
Denjo tafadhali tutumie namba ya simu tutawasiliana nawe kwa ufafanuzi zaidi.
 
Last edited by a moderator:

Ahsante sana, tumeuchukua ushauri wako na tutauzingatia Asamwa
 
Last edited by a moderator:
Vodacom Tanzania hivi mtu akifariki hela zake kwenye M PESA zinapelekwa wapi na ni shilingi ngapi zimepatikana ambazo hazina mwenyewe na zimefanyiwa nini?

Habari Shark, ahsante kwa kuuliza suala la msingi. Endapo kadi/namba ya mteja itakaa kwa zaidi ya siku 90 bila kutumika hufutwa (hii inaweza kusababishwa na kifo cha mteja au sababu nyingine yoyote iliyopelekea namba kutotumika) inapofutwa pesa hutunzwa katika akaunti maalum.

Mrithi wa mali za marehemu atatakiwa kufika katika ofisi zetu na vithibitisho vya kuteuliwa kuwa mrithi ambapo taarifa hizo zinakua zimethibitishwa na Mahakama, mrithi hujaza fomu katika ofisi zetu kisha taratibu za kuwapatia pesa hizo hufanyika.
 
Last edited by a moderator:

Habari marimba ahsante kwa kulifikisha hili kwetu, tutakupigia simu kwa msaada zaidi. Pole
 
Last edited by a moderator:

Nimekumbana na tatizo kama hili. Nimefatilia miezi mitatu sasa. Nimeenda Arusha summit, vodashop mlimani city, nikapigiwa simu toka makao makuu kuwa kitambulisho hakionekani vizuri. Nikarudi summit wakatoa photocopy kama wiki tatu zimepita lakini shida ipo palepale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…