Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Pia ukijiunga na kifurushi cha mitandao yote undo balaa dk tu salio limeisha,kweli voda kiboko.
 
Nyie voda mbona vifurushi vyenu saivi uzushi mtupu? Unanunua kifurushi cha bombastic unapiga kabla ya dk 3 kuisha unatumiwa msg kifurushi kimwisha, halafu mbona kimyakimya bombastic ya 500 mb zimebakia 50 na dk19 kulikoni???
 
Voda mnakera sana vifurushi venu nimekaa kihuni mtu unajiunga kifurush cha internet hujafanya chochote unapata sms mb zako zimeisha..ila kila jambo lina mwisho wake utakuja mbadala wenu
 
Mnapata faida gani kumfungia mtu laini, kisa tu kuna mtu kakosea namba tena mwenyewe, mmefunga laini yangu mpesa niliyokua nafanya miamala zaidi 80 kwa mwezi!, badala ya ninyi kumcommand awe anapiga customer care kama nna salio mkate, sasa faida ipi mmepata?! mmepoteza miamala mingapi?!, yaani kuangalia salio tu naambiwa akaunti yako ya mpesa haipo! he, kwa utaratibu huo kila mtu tu akiwapigia mnafunga mpesa yake, hamuoni mnapoteza wateja?, mambo haya yanaenda kimya kimya sio kukurupuka tu na kumfungia mtu mpesa! mnategemea nimeona mpesa yako haipo ntaweka pesa!!? u have to think b4 acting, nimehamia eatel wazee
 

Habari Roy, tafadhali tutumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi. Pole
 
Voda mnakera sana vifurushi venu nimekaa kihuni mtu unajiunga kifurush cha internet hujafanya chochote unapata sms mb zako zimeisha..ila kila jambo lina mwisho wake utakuja mbadala wenu
Habari Mihadarati,hapana shaka kuwa kifurushi huisha kutokana na matumizi, la kama unahisi hukufanya matumizi yoyote na kifurushi kimekwisha unaweza kututumia namba yako ya simu
 
Vodacom shop imejaa wezi watupu pale unaingiza vocha haiingii unaambia mtandao.mtandao gani miezi yote hii.jamaa wa kuingiza vocha mshenzi sana yule
 
Mlianza vizuri sana hasa huduma ya mpesa,ukweli ni kwamba huku Kahama Bugarama karibu na Kakola internet yenu iko chini yaani kwa kifupi haipo hivyo mmeruhusu airtel wauze line na vocha kwa wingi na kutulazimisha kumiliki laini mbili,moja ya mpesa na nyingine kupigia simu na internet (airtel) hii issue ni real kwani ukifika Geita mjini internet yenu inakuwa strong kuliko airtel. Hapa Bugarama ndipo familia za watu na pesa zao zipo namaanisha ma miner.
 
Kero Yangu ni kuwa mnashindwaje kumuwezesha mteja kujiunga na vifurushi vya muda Wa maongezi na internet kutoka katika M-PESA? Kusema kweli inanikera sana kuona ni lazima nihamishe fedha halafu nijiunge.. Badilikeni sasa jamani
 
 
nimerenew line 0758101115, ac yangu ya mpawa haipatikani, mawasiliano na huduma kwa wateja sijapata utatuzi. nisaidieni!
 
Nyie voda mnazingua mmenifanya cku hizi nicwe naweka credit nyingi kwenye cm yangu kozi nikiweka nakuta imepungua kiajabu ajabu tu au cku hizi mnatufanyia mazingaombwe? Acheni kuzingua
 
Bora nisubiri VIATEL, lkn hii mitandao tuliyokuwa nayo inafanya kazi kwa kutegemea hali ya hewa, kukiwa na jua kali mitandao mingine inagoma hata kuangalia salio sembuse NET, na ikinyesha mvua ndio kabisaaaaa majanga hata hela unaweza usitoe, nishajichokea nabaki kuwaangalia tu
 
Yaani mpaka leo hela yangu nilitransfer kwa nmb mobile hamjaireverse huo ni wizi au kitu gani?mnakera kwa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…