Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Habari Easymutant mara nyingi hii hutokea pindi mteja anapokuwa amejiunga na zaidi ya kifurushi kimoja hivyo kifurushi cha awali kinapokwisha mteja anadhani ni kifurushi kipya alichojiunga nacho. Inapotokea hali hii tafadhali piga *147# kuangalia salio. Tunaomba namba yako ya simu PM kwa msaada zaidi.

Asante sana kwa kujibu but it's too late... Niko plan B tayari.
 
Katika hali isiyo ya kawaida, mtandao wa vodacom umeanza kuwa wa ajabu ajabu, mtandao huu ambao kipindi cha nyuma ulikuwa miongoni mwa mitandao stable, lakini cha ajabu sasa hivi imefikia hatua hata SMS ILIYOTUMWA LEO INAFIKA SEHEMU ILIYOKUSUDIWA BAADA YA MASAA 12, kusema kweli hali hii inashangaza, inafedhehesha na inasikitisha kwa nini hawatatui tatizo hili.

Si hivyo tu hata huduma ya M-Pesa ambayo ni dhamana ya pesa za wananchi, imekuwa siyo ya kuaminika, mara iwepo mara isiwepo.
Ni wakati muafaka kwa kampuni hii kuinvest katika mitambo yenye nguvu ili kuweza kuhimili load kubwa
 
Mkuu una moyo wa chuma kuweka rehani pesa zako kwenye mitandao ya simu. Nakushauri kama utaweza badili mfumo wa utunzaji na utumaji pesa uwe unatumia taasisi za kibenki kwenye uhakika zaidi.

Huku kwenye mitandao ya simu kumeoza kabisa hasa vodacom. Kwa mawasiliano ya kupiga na kupokea simu pamoja na kutuma ujumbe tumia mitandao mingine yote isipokua vodacom ambao kwa sasa wanaongoza kwa ubabaishaji, wizi na utapeli kwa nguvu.
 
Habari Easymutant mara nyingi hii hutokea pindi mteja anapokuwa amejiunga na zaidi ya kifurushi kimoja hivyo kifurushi cha awali kinapokwisha mteja anadhani ni kifurushi kipya alichojiunga nacho. Inapotokea hali hii tafadhali piga *147# kuangalia salio. Tunaomba namba yako ya simu PM kwa msaada zaidi.

Mmmh, sidhani, hili ni tatizo sugu kwa kweli, kwanza voda hawaruhusu kujiunga na kifurushi kingine kabla ya muda wa kifurushi vha awali kuisha, hii nayo ni kero nyingine.
 
Last edited by a moderator:
Vodacom inanibidi kuweka vocha mara mbili zaidi ya kiwango ninachohitaji kununulia kifurushi,
nimeamua kuhama tu
 
Tutumie namba ya simu na tuambie lini ulipata tatizo hili. Ahsante

Imenitokea last wk zaidi ya Mara mbili na tatizo lingine ni Kuwa na pesa ya kutosha kununua kifurushi fulani lakini kila ukijaribu kujiunga unaambiwa hauna salio la kutosha. Mimi ni mteja was vodacom kuanzia mwaka 2000 na mbaya zaidi kila ukipiga customer care ni kichefuchefu tupu utasubirishwa mud a mrefu halafu mwisho was siku unapewa majibu short
 
Kuko na options nyingi now days, hama ingia mtandao unaouna ni bora zaidi kwako na kuiacha voda kama mtandao wa kupokea cm tu.

sio rahisi kihivyo na tunafanya hivi ili kuwasaidia na wengine pia pamoja na vodacom wenyewe
 
Imenitokea last wk zaidi ya Mara mbili na tatizo lingine ni Kuwa na pesa ya kutosha kununua kifurushi fulani lakini kila ukijaribu kujiunga unaambiwa hauna salio la kutosha. Mimi ni mteja was vodacom kuanzia mwaka 2000 na mbaya zaidi kila ukipiga customer care ni kichefuchefu tupu utasubirishwa mud a mrefu halafu mwisho was siku unapewa majibu short

Pole sana mshana jr tutaomba utupatie namba yako pindi tu unakutana na hali hii kwasababu inakuwa rahisi kufanya utatuzi na kujua tatizo kwa wakati huo. Ahsante sana kwa kuwa mteja wetu na tunaahidi kutoa huduma bora na msaada pindi unapohitaji
 
Last edited by a moderator:
Mmmh, sidhani, hili ni tatizo sugu kwa kweli, kwanza voda hawaruhusu kujiunga na kifurushi kingine kabla ya muda wa kifurushi vha awali kuisha, hii nayo ni kero nyingine.
Tuambie ni kifurushi gani umejaribu kujiunga bila mafanikio ulipokuwa na kifurushi kingine tafadhali.
 
Vodacom Tanzania, mimi nilikua mteja wenu mzuri sana hadi October 2013, lakini mlipoanza mikwaruzo yenu mlinifukuza bila kupenda. Mfano ilifikia na wengi wanalalamika hadi leo kama mdau mmoja hapo juu kwamba unataka kujiunga na kifurushi cha sh 500, mathalani, na una sh 520 lakini unaambiwa huna salio la kutosha kujiunga. Ukiongeza tena salio likafika labda 1000 ndipo unaruhusiwa kujiunga na kifurushi cha sh 500. Sawa umejiunga lakini mbaya zaidi kile kifurushi sekunde chache kabla ya kuisha muda wake mnakamua kwanza salio lililobaki ndipo mnaleta miujumbe eti kifurushi kimeisha.
 
Last edited by a moderator:
Vodacom Tanzania, kuna mambo mengi ya ajabu mlikua mnatutendea na pengine bado mnawatendea wateja wenu walioamua kubaki nanyi, nitakupa baadhi ya kero zenu hapa chini:

1. Mlikua na code #100 ile ya kupiga bure kwa ajili ya msaada, lakini nilikua kila nikipiga nakumbana na matangazo mengi sana zaidi ya dk 7 hadi 8 na mwisho naambiwa "watoa huduma wetu wanahudumia wateja wengine, endelea kusubiri au kata simu upige tena". Sasa utasubiri mpaka uchoke.

2. Niliwahi kupewa code #15366 ya huduma kwa wateja ila unailipia sh 100 kila upigapo. Sasa balaa lake likawa kila nipigapo nakatwa sh 100 lakini naambulia porojo kama kule kwenye code #100 ya bure. Hadi kuwapata wahudumu nilikua nakatwa zaidi hata ya sh 500 hadi 700.

3. Siku nilizokua nafanikiwa kuwapata huduma kwa wateja mara nyingi walikua hawana lugha za kistaarabu na mwisho wake waliniambia nisubiri masaa kadhaa (eg. 24, 48, etc) shida zangu kutatuliwa.

Upande wa mpesa nawasifu mko makini sana na hongereni na kama bado mko makini basi ongezeni umakini na kwenye huduma zingine.

Nikutakie kazi njema ila sitawasahau kwa wizi mlionifanyia October 2013 hadi nikaamua kuwanyoshea mikono nikajisalimisha kwenye mtandao mwingine.
 
Last edited by a moderator:
hivi ni nani atatuokoa kutoka kwenye ulaghai na wizi wa Voda?

nimekuwa mteja wa Vodacom tangu waanze biashara yao nchini. Hii kampuni inaendeshwa kiulaghai-laghai sana na sijui tutawezaje kuwapa somo wawe wakweli.

Kuna ofa ya uongo ya HAPPY hour, miongoni mwa uongo mwingine chungu nzima. Labda hapa sasa utakumbuka na lile tangazo lao eti swala anamfukuza chui. Yaani voda ni wadanganyifu, ni wadanganyifu sana! Nimechagua dakika 60 kwa 200/- mara nyingi. Hiyo ndo happy hour yenyewe. Nikiongea dakika 7 inakata. NDUGU MTEJA KIFURUSHI CHAKO KIMEKWISHA. Mbona mimi naona dakika 60 ni nyingi kuzidi dakika 7?

Leo saa 1.30 nimechagua HAPPY hour ya dakika 20 kwa sh. 100 kujaribu hiyo. nusu saa baadaye nimeletewa ujumbe NDUGU MTEJA KIFURUSHI CHAKO KIMEKWISHA.

Hivi vifurushi vya VODA vinaliwa na nani? Mbona mie siwaelewi hawa? Au hawa watu wanaona Tanzania hatujui kuhesabu dakika?

Au nyie wenzangu vifurushi vyenu vinadumu?
 
Sijui tutaponea wapi?Hakuna mtandao hata mmoja usio na ujanjaujanja huu.Mi natumia yote ulaghai wa aina km hiyo uko palepale.
 
Back
Top Bottom