Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Nyie voda mjirekebishe hivi kweli mtu unakuwa umejiunga kifurushi kweli hata mtu akitumia sekunde 20 mnahesabu ni dakika mna umaskini gani kiasi hicho?
Badilikeni kuna kipindi mlianza kufanya hvyo then mkaacha, tena mmeanza
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania

ushauri wangu kuhusu bandle ya internet mmepunguza sana na ofa za dakika chache mno ukilinganiza na mitandao nyingine kama airtel napenda sana vodacom lakin naelekea kukata tamaaa sana jaribuni kurekebisha tena sitasahau my number one ilipendwa sana na watu wengi sana lakini saiz hakuna ofa ya maana.
 
ushauri wangu kuhusu bandle ya internet mmepunguza sana na ofa za dakika chache mno ukilinganiza na mitandao nyingine kama airtel napenda sana vodacom lakin naelekea kukata tamaaa sana jaribuni kurekebisha tena sitasahau my number one ilipendwa sana na watu wengi sana lakini saiz hakuna ofa ya maana.
Ahsante kwa mrejesho Rich, tutauzingatia.
 
Nyie voda mjirekebishe hivi kweli mtu unakuwa umejiunga kifurushi kweli hata mtu akitumia sekunde 20 mnahesabu ni dakika mna umaskini gani kiasi hicho?
Badilikeni kuna kipindi mlianza kufanya hvyo then mkaacha, tena mmeanza

Habari Lazar, makato ya vifurushi vyetu ni kwa sekunde sio kwa dakika mkuu japokuwa unapoangalia salio huoneshwa kuwa zimebaki dakika kadhaa.
 
university offer yenu haieleweki eti mtu najiunga nipo chuo naambiwa nipo mbali na eneo je toa maelezo kamili juu ya swala hili tujue offer inawahusu akina nan na wakiwa wap
Habari Nkyami, tunaomba namba ya simu na chuo ulichopo PM kwa msaada zaidi.
 
Vodacom mnazingua na huduma zenu za kiboya hasa hii ya SIMU TV, ni wizi mtupu; mie sijawahi kujiunga hiyo huduma na kila cku mnanitumia masms yenu kutoka TBC. Cha kuudhi zaidi mmetaja humu kwenye thread ya mhanga mmoja kama mie kuwa tupige *149*01# kutaletewa hizo options mbona haipo? nitoeni bwana, nimewapigia simu hadi sikio linapata joto hampokei, YA NINI KUHARIBIANA MWAKA MAPEMA HIVYOOOOOOO. Nitoeni bwanaaaaa ahaaaaaaa

Pole sana, piga *149*01# chagua Shangwe-> Simu.tv kisha chagua TBC halafu jiondoe.
 
Vodacom msaada wa internet configuration kwenye sumsung Galaxy S5 G900H.nimejaribu kuweka details zifuatazo bila mafanikio


Account Name: Internet
APN : Internet
Proxy: 10.154.000.008 na pia nilijaribu 8080 zote zili fail
Port: 9201 na pia nilijaribu 9401 zote zika fail
Tafadhali usijaze parameters nyingine zaidi ya hizi;

Account Name: Internet
APN : internet

Hakikisha INTERNET unaiandika kwa herufi ndogo.
 
Vodacom Tanzania acheni uhuni wa kutuibia salio zetu kwenye simu.

Nimenunua salio nikajiunga na kifurushi cha wiki, nikaacha salio... Hee muda wa kurenew kifurushi bado na salio mmekomba...

Soon line yenu naiflash chooni...
Habari Little Angel, tunaomba kupata namba ya simu na tarehe husika kwa msaada zaidi. Tuma PM mkuu.
 
buzuruga na nyasaka smart 4n ukiweka voda ni worse. mwezi wa pili tunadaka E badala ya 3G au H. Kulikoni??? hamna tunachopata zaidi ya bando kuexpire bila kutumika.

Vodacom jitaidi kuboresha mtandao wa 3G kwa sisi tunaopatika Lushoto angarau ata chuo cha SEKOMU tuweze kufaidi internet.

Vodacom Tanzania nipo morogoro mjini nina wiki mbili sasa sipati Huduma ya 3G kila ninapo on 3g network nashindwa kupiga sm wala sipatikani hewan mpaka Leo natumia edge niongea na customers care nimechoka nalazimika kutumia tigo sababu Voda mnasumbua rafiki yangu pia alitaka kuuza sm baada ya kuona tatizo hilo Tafadhali sana hebu shughulikie matatizo hayo.

Mwanza maeneo ya pasiansi hatupati 3G kwa siku nne sasa mfululizo na hata ikijaga huwa haiko stable..tusaidieni jaman la sivo tutahamia kule kwa wale jamaa wengine maana wao tatizo la internet hatujawahi kusikia
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza, tafadhali tutumieni namba za simu kwa msaada zaidi.
 
Tokea asubuhi umekua ukisuasua sana sasa sijui ni maeneo ya kwetu huku au ni kila mahali
 
Tuko nilipojiunga na kifurushi jana hadi muda huu ndio nakitumia na kila baada ya dakika kadhaa unakata,mambo gan haya? Tufidien bhana mi nimeunga bila kikomo jana usiku hakuna kinachoendelea,mnaboa bhana
 
Voda Mmebadilika Mmenipotezea Mamboyangu Mengi System Yenu Ya Swap Kwa Nini Imekufa Haifanyi Kazi Tangu Tr 31 Nikaja Vodashop Samora Ikawa Hivyo System Mbovu Tr 3 Nikaenda Voda Shop Gongolamboto Napo The Same!, Wakaniambia Niende Vodashop Airport Wakaniambia System Ya Swap Imegoma, Jana Ndo Nilitaka Kuzimia Kabisa Vodashop Airport, Wakaniambia System Bado Mbovu, Almost Ten Days Still The Same Problem, Am Tired Of You Imenibidi Ninunue Tigo
 
Nimekuwa mteja wenu wa net kwa muda sasa ila mmeanza kunisikitisha kwa kuniibia salio langu mara tatu sasa. Nimekuwa naweka salio la elfu tano afu najiunga na bundle la internet ya wiki, ila mara 3 sasa nimeweka salio la elfu tano ila nilipotaka kujiunga na internet bundle ya wiki mmekuwa mnanambia sina salio na nikichek salio kweli linasoma sifuri ilhali sijatumia hata senti. Nimewapigia simu mara zote tatu mnadai simu yangu inakula salio hata kama haitumiki what a lame excuse, hawa waajiriwa wenu wasioelewa nature ya tatizo na kumsaidia mteja mnawaokota wapi? Acheni wizi hata kama mtu unasalio kwenye simu si kwaajil yenu kuliiba sh*t soon nitaopt another network provider coz you not the only fish in the ocean
 
Achana nao wao siyo hewa bana wapuuzi kweli tumia zain ila siyo tigo make tigo wako kama sugu ni vurugu kuliko kawaida.
 
Back
Top Bottom