Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Nyie vodacom kiukweli ni MAJIZI SANA,I guess after 10 years mtabakiwa na wateja wa vijijini tu na wale ambao hawana option
Mfano.
KUNA huduma inaitwa "Internet BURE",lkn haijawahi kudownload hata page moja iwe kwenye simu au computer.
KWANINI MTUDANGANYE?.

Tigo na Airtel ndo habari ya mjini.Mjini tunwak
 
Nina line mbili za vodacom ila nilishaacha kuweka salio.Nimehamia kwa wale majirani zenu wale wekundu na wale wa JoTI.
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania

Kuna Jamaa huku anadai mmemtapeli

www.jamiiforums.com/kenyan-news/87...shinda-100-millions-kumbe-2.html#post13125110
 
Naomba mnifunguli vocha yangu 005985269642 yenye namba ya batch no 1051079243, nahitaji kutumia simu haraka.
 
Malalamiko yangu kwa Vodacom ni kwanini mtu akinunua kifurushi mnachelewa kujibu msg
 
Alafu unakuta nilizima mobile data ukiwasha unakuta hela yote imeisha nawaomba mjirekebishe jamani nimeweka 5000 nikajiunga kifurush cha wk nimesubiria majibu hakuna ile kuwasha mobile data tu yote imeisha nusu nianguke
 
vodacom Mji Wa KISARAWE PWANI hauna internet sasa ni siku ya 6
fanyeni kutatua hili tatizo
mnakera sanaaaa

aaaaagggghhhhhhh
😡😡😡😡😡😡😡😡😡😡😡
 
Naomba kuwauliza nyie jamaa....hv mlishawah kufanya research ya mtandao wenu pale Mwanza mjini???epsecially ofisi ya mkuu wa wilaya Nyamagana(ofisi ya mamlaka ya maji).Ukiwa pale hakuna network kabisa.....acheni kukenua,rekebisheni tatizo pale
 
Nipo Kilindi Tanga,tatizo langu ni kwamba ninapowasha simu yangu nikichelewa kuondoa picha ya PAMCHART kwenye screen ya simu yangu,halafu nikifungua OPERAMIN kwa ajili ya Internet basi laini yangu ya voda inaandika INVALID SIM CARD ilhali laini ipo na sijaisogeza wala kuigusa.Na nimejaribu kubadilisha simu nyingine lakini bado na simu ninayotumia ni TECNO 611.Sasa nifanyeje?
 
Vodacom acheni kuzingua, yaani hata kale kakifurushi ka 500 kenye 200MB Mmekanyenga tena na sasa ni 180MB tu!!!!!!!!?????? Jamani tuoneeni huruma sisi watu masikini!!
 
Sasa hats kama ni uchaguzi Msitunyanyase kwani mmeanza kupunguza MB kutoka MB200 kwa Tsh500 sasa mnatoa MB180 je tuamie wapi???
 
Haya majamaa ya voda hovyo kabisa, nchi inapokuwa controlled na wafanya biashara madhara yake ndio haya
 
Back
Top Bottom