Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom kwani hela za kuuza hisa haziwatoshi hadi mhamie kwenye salio tunaloweka kwenye simu? Leo nimepokea ujumbe kuwa hela niliyonayo kwenye salio litumike hadi mwisho wa mwezi huu?

Hivi hadi salio la kwenye simu mnaliwekea limit ya muda? Kwa uhuni huu, kwenye hisa mtakuwa waaminifu?
 
Najua hakosekani mtu wa hii kampuni humu. Kama hamjui basi nawaambia hiviii,"tangu siku ya jumatatu na jumanne inapofika saa sita usiku network inatoweka kabisa! Simu inageuka toy!"

Kwa siku ya jumatatu tangu saa sita network ilivyotoweka sikumbuki ilirejea muda gani, maana hadi napitiwa na usingizi saa tisa, simu haikuwa na network. Nilivyoamka asubuhi ndio nikaikuta!

Jumanne hivyo hivyo ilivyofika mida ya saa sita mkapita nayo tena, ila ikajitahidi kurudi saa nane bando langu likikaribia kuisha!

Leo hii nimeandika hii taarifa kwa kuweka na Kigogo sababu ya hiyo network kusumbua, ila leo angalau ilikuwa inakata "viuno" yaani inatoweka na kurudi.

Pamoja na kero zote hizo, hata kuomba radhi au kutoa taarifa hakuna! Aiseee!! Mngefidia hata huo muda mliopita na bando zetu basi!

Au mnajifanya hamjui kuwa Mkulu kameza funguo za kibubu?! Morogoro.
 
Voda n ikifika iyo saa sita speedi ya internet inaongezeka kwa kasi zaidi uku nilipo
 
Usingizi umegoma kabisa, naskilizia tu mbwa wanavyopuliza sexaphone!![emoji16] [emoji16] [emoji16]
 
Voda n ikifika iyo saa sita speedi ya internet inaongezeka kwa kasi zaidi uku nilipo
Kwenye speed wala sina tatizo nao, maana hata mchana iko fresh. Na ndio mtandao nnaouamini, ila wamenitia hasara sana wa GB zangu kwa hizi siku walizozingua! Halaf wako kimyaa!!
 
Voda kiukweli mnaboa sana mtandao wa uongooo sana mi ngoja niwanawe tu
 
Voda me siwaelewi kabisa siku hiz sijui ndo kuzidiwa na wateja na nunua 1gb kwa 2000 lakini simu hai access network mpak muda hunaisha na simara moja
 
Vodacom Tanzania Hivi tunavyotoa malalamiko yetu hapa na mkaamua kukaa kimya kama hamuoni ni mnatudharau au? Kama kero hizi mnashindwa kuzijibu, mtakuwa wakweli kwenye hisa?
 
Nimetoa hela mpesa sasa muamala umefail nimewapigia customer care eti up to 4 days ndo pesa itarud imagine ndo nauli hiyo si utalala stand[emoji23] badiliken jaman hata kama ni utaratibu sio hivo
 
ngoja kwanza tupe bize na oparesheni ya kuuza hisa,

hiyo buku 10 yako utaipata tu, usihofu.
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

  • Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
  • Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
  • Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
  • Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
  • Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Kuna - sijui niite ni "ujanja" - nadhani kwa kweli. Simu yangu ina laini 2 tu. Voda na Tigo. Niliweka internet ya wote wawili. Lakini hivi sasa upande wa Tigo siwezi kuaccess internet. Nahisi kuna kimchezo ka ku-hack simu za watu hapa. Kama ni kweli, mnaonaje nikiwashitaki kwa mamlaka ya mawasiliano?
 
Jumanne asubuhi nliamka nkakuta mtandao voda umeandikwa emergence na sikuwa na mawasiliano kwa saa 24, jana (juma5) tena sikuwa na mawasiliano kwanzia mchana mpaka leo saa 12 asubuhi.

Cha ajabu nlikuwa nmejiunga kifurushi internet cha wiki ambacho kinaisha ijumaa usiku, leo naambiwa kimeisha. Sasa me sielewi kifurushi kimeishia wapi?
 
Jumanne asubuhi nliamka nkakuta mtandao voda umeandikwa emergence na sikuwa na mawasiliano kwa saa 24, jana (juma5) tena sikuwa na mawasiliano kwanzia mchana mpaka leo saa 12 asubuhi... Cha ajabu nlikuwa nmejiunga kifurushi internet cha wiki ambacho kinaisha ijumaa usiku, leo naambiwa kimeisha. Sasa me sielewi kifurushi kimeishia wapi?

Hawa jamaa wahuni sana. Halafu yanaona hizi complains na hakuna yanachokifanya. Nini maana ya kuwa na support thread sasa kama kero hazifanyiwi kazi?

Ndo maana bado nawaza sana kuhusu hisa zao. Kama kwenye vifurishi wanakosa uaminifu. Huko kwenye hisa yatakuwa makweli?
 
Hata kwangu nimelifutilia mbali li app lao maana linanijazia tuu mafile Kwenye cm yangu
 
Habari wana jukwaa?
Vodacom Tanzania wana application ya simu ya M-Pesa. BIG UP sana kwa hili maana katika dunia ya sasa ya digitali tunahitaji huduma muhimu kama hii iwe katika kiganja.
Ukakakasi unakuja kwenye jambo moja; app hii haifanyi kazi vizuri. Nimeinstall kwenye simu yangu ila haifanyi kazi kwa Wi-Fi inataka utumie mobile data. Ila hata ukitumia mobile data haifanyi kazi. Nimepitia review nyingi za watumiaji wa app hii wanalalamikia tatizo hilo. Sasa Vodacom Tanzania jaribuni kutatua hili tatizo kwa kurekebisha app yenu maana haina siri nyie ndio mnaongoza kwa wateja katika huduma hii ya kifedha.
Wassalam!View attachment 499661 View attachment 499662 View attachment 499662
Alafu wanataka data iwe inatumia ya voda tu
 
Back
Top Bottom