mgeni mwenyeji
Member
- Nov 22, 2017
- 22
- 11
Ndugu mteja,
Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?
Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.
Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:
- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.
Karibu
Vodacom Tanzania
Code:
*VODA KAMA MMETUCHOKA WANA CHUO MTUAMBIE*
Habari ziwafikie popote mlipo........
Sisi ni wanachuo watoto wa maskini kutoka Tanzania ambao tulitokea kuupenda mtandao wa Vodacom na kuona ni mahali sahihi kwa kutokana na matumiz yetu mbali mbali ya simu hususani kimtandao ambayo hutusaidia kutafuta material mbali mbali kwa gharama nafuu .
Sasa mmetuona sisi ndio shamba la bibi kwa kutaka kujinufaisha kwa haraka au yale mamilioni mliyotoa kwenye rambi rambi mnataka mrudishe kupitia sisi ??? Iweje mtupandishie gharama za vifurushi kwa kiasi hicho ??
Kueni na huruma kwa watoto wa maskini kama sisi tunaojariwa kuja kuwa wajengaji wa taifa hili letu pendwa la Tanzania. Kiukweli hatuna hamu tena ya kuendelea kuwa wateja wenu teena kwa haya mnayoyafanya . Tunaomba popote msomapo ujumbe huu mjibu swali hili " MMETUCHOKA WANA CHUO"??? AU "MMEONA SISI NDIO SHAMBA LA BIBI???" .
Msipolirekebisha hili ndani ya siku nne tunahama mtandao wenu mtumie wenyewe Uni offer maana mmeona tunafaidi sana . Kwa leo acha niishie hapo tusubir utekelezaji
Ewe mwanachuo Share hadi iwafikie
~Fulldose~