Ndugu mteja,
Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?
Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.
Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:
- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.
Karibu
Vodacom Tanzania
Muwe wa kweli, tusilete shida hapa halafu iwe ni blablaa. 1. Nimetuma pesa kwa simbanking kutoka CRDB kuja account yangu ya Mpesa tangu asubuhi ya leo haijafika kwenye namba yangu ilihali benki imeshakatwa. 2 sijawahi kuona kitengo cha hovyo kama custormer care ya Vodacom. Hakuna mhudumu anayepokea simu. Mlikiweka cha nini?