Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania

Vodacom transaction number 60319575 euro 206.99 zilitumwa akakosea number mkazizuia kabla hazijatolewa na mkasema mtazirejesha kwa matumaji lakini mpaka leo hamjarejesha. Ni zaidi ya mwezi sasa kunatatizo gani?
 
Vodacom transaction number 60319575 euro 206.99 zilitumwa akakosea number mkazizuia kabla hazijatolewa na mkasema mtazirejesha kwa matumaji lakini mpaka leo hamjarejesha. Ni zaidi ya mwezi sasa kunatatizo gani?
Na Mimi nina Tatizo kama lako naomba Kama una namba za TUME YA USHINDANI Nisaidieni
 
HABARI VODACOM MIMI NAITWA GODWIN NIPO ARUSHA NAOMBA NIWAULIZE INACHUKUA MUDA GANI MTU KUPATA NAMBA ZA UWAKALA MAANA NINA MIAKA MITATU NAJAZA FORM NIMESHATOA KIASI CHA 10000 KAMA MARA TATU KWA AJILI YA MWANASHERIA KUSAIN LAKINI WAPI MPAKA NIMECHOKA
 
Ule mkopo wenu wa M-pawa ni wizi mtupu. Ule mkopo umekaa kiwizi sana.
Mfano. Unakopa 40000 wanakata 19% ya 40000 ambayo ni sawa na 7600.
Na hiyo riba inakatwa ndani ya mkopo ulio kopa hivyo unapewa 32400. Lakini utapaswa kurejesha 40000.
Kama unajua hesabu, huu ni wizi wa mchana kweupe.

1. Mkopo wa 19% riba!!!!!
2. Unakatwa riba ya mkopo wa 40000 lakini hupewi 40000 bali unapewa 32400.
 
Muda huu ,nimetoka kutuma pesa kupitia simu yangu kwenda mtandao wa Airtel nimetuma tshs 52,000/= nimekatwa tshs 4,370/= daaaaah mbona aghali hivyo?
 
Nlikuwa hoi baada ya kukopa 55k M-Pawa nikakatwa 10k baada ya kuitoa nikapata cash 37500. Nyie Vodacom ipo siku nitakopa halafu ndio itakuwa mwisho wa kutumia mtandao wenu
 
Ninachenjoy ni hawajali kuwajibu mnachoandika. Yaani kama Deo Kisandu anaanzisha mada kisha anatokomea ngojeni mletewe Tobi awajibu maswali yenu.
 
kumekuwa na tatizo kubwa sana la sms failure na internet pia, yaan wakati mwingine unaweza ukaunga bando la week la sms cha kuskitisha unaweza ukawa unahitaj kutuma sms muhim lakin unapotuma tu inakwambia not sent, hili limekuwa tatizo sugu na tume report sana kupitia page yenu ya fb lakin hakuna msaada wowote ule tunaoupata

tatizo la pili ni la internet, unakuta mtu umeunga bando kwa ajili ya kuperuzi lakin cha kuskitisha ukitaka kufungua page unakuta ina load karibu dakika 5 nzima baadae unakuta mtandao umeondoka kabisa yaan 3g au 4g haipo kabisa , baada ya muda mfupi inarudi tena, ukianza kufungua page inaload baada ya muda mfupi unatumiwa sms kifurushi chako kinakaribia kuisha hatimaye unaambiwa kifurushi kimeisha kabisa, kwa kwel inatakiwa mjitathmin sana , muwajali pia wateja wenu sababu mnachotufanyia ni uhun, sisi ni wateja na tunatumia pesa kwaiyo tunatakiwa kupata huduma inayofanana na kile tunachotoa na sio kutufanyia uhun.
NAWASILISHA
 
HABARI VODACOM MIMI NAITWA GODWIN NIPO ARUSHA NAOMBA NIWAULIZE INACHUKUA MUDA GANI MTU KUPATA NAMBA ZA UWAKALA MAANA NINA MIAKA MITATU NAJAZA FORM NIMESHATOA KIASI CHA 10000 KAMA MARA TATU KWA AJILI YA MWANASHERIA KUSAIN LAKINI WAPI MPAKA NIMECHOKA
Habari Godwin.
Ahsante kwa kuwasiliana nasi. Tunaomba kufahamu kama ulishawasilisha nyaraka zako zote katika duka la Vodacom kwa msaada zaidi.
 
Vodacom, tafadhali nisipate tena msg zile za Mojaspesho, na zile nyingine za minada, I no longer have interest za hi iyo michezo, nifanyeje please
 
Back
Top Bottom