Nimekuwa na kawaida kila siku kuwasiliana na ndugu na jamaa kupitia international calls. Cha ajabu leo siku ya pili jamaa zangu wote walio katika mtandao wa Vodacom nimekuwa siwapati. Nilidhani tatizo labda ni kwa Tanzania lakini wa mitandao mingine kama, Tigo, Zain na TTCL nawapata pasi na tatizo. Nina watu kama 20 wenye namba za Vodacom hakuna mawasiliano kabisa kutokea nje ya Tanzania. Swali ni je Vodacom wameamua kuachana na simu zote zinazotoka nje ya Tanzania na hasa zile zinazotumia kadi maalum za International call au mitambo yao ina matatizo?.
Hofstede,
Vodacom Tanzania wamekuwa wakitumia Gateway ya Zantel na TTCL kwa muda mrefu kwaajili kama carrier wao wa international calls.lakini hivi karibuni Vodacom group imenunua gateway yao na hivyo wanaacha utegemezi wa zantel na TTCL kwa shughuli hiyo.sasa nafikiri katika transition hapa walikuwa hawajajipanga vizuri lakini nafikiri hilo ndiyo tatizo kubwa.soon mawasiliano na ndugu zako kupitia vodacom yatarejea katika hali ya kawaida.pole kwa usumbufu ulioupata na nafikiri vodacom wenyewe (mimi si mfanyakazi wao) wana regret kwa usumbufu unaowapata watu kama nyinyi.
Asante.
Wamenunua facilities zao lakini bado watatumia Gateway ya TTCL kutolea mawasiliano ya nje. Kumbuka earth station ni moja na ni kwa ajili ya kuwa na monitoring mechanism ya data.Hofstede,
Vodacom Tanzania wamekuwa wakitumia Gateway ya Zantel na TTCL kwa muda mrefu kwaajili kama carrier wao wa international calls.lakini hivi karibuni Vodacom group imenunua gateway yao na hivyo wanaacha utegemezi wa zantel na TTCL kwa shughuli hiyo.sasa nafikiri katika transition hapa walikuwa hawajajipanga vizuri lakini nafikiri hilo ndiyo tatizo kubwa.soon mawasiliano na ndugu zako kupitia vodacom yatarejea katika hali ya kawaida.pole kwa usumbufu ulioupata na nafikiri vodacom wenyewe (mimi si mfanyakazi wao) wana regret kwa usumbufu unaowapata watu kama nyinyi.
Asante.
TCRA waliwashauri makampuni yote ya simu ya-share miundombinu ya mawasiliano pamoja lakini muafaka haukupatikana nafikiri madhara yake ndiyo kama haya;kwasababu umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
Hata hivyo mimi nasubiri hiyo June,2009 ifike ili nijione urahisi,uharaka na wepesi wa teknolojia ya kisasa ya mawasiliano kwa kutumia optic fibre backbone.
kama TCRA as a national regulatory authority walishauri basi wanashangaza sana..huku ulaya its passed in the telecoms regulations kwamba lazma watu washare facilities.. (from minara to gateways.....especially kwa new entrants in the game..) kama ni kweli unayoyasema basi TCRA wanabangaiza tuu...back to the issue of international calls..kweli hata mimi yamenitokea sana napojaribu kupigia ndugu wenye line ya voda ..na celtel ile issue ya kutuma sms mbili mbili internationally especially uk naona bado inaendelea...tatizo ni nini??