Nimekuwa na kawaida kila siku kuwasiliana na ndugu na jamaa kupitia international calls. Cha ajabu leo siku ya pili jamaa zangu wote walio katika mtandao wa Vodacom nimekuwa siwapati. Nilidhani tatizo labda ni kwa Tanzania lakini wa mitandao mingine kama, Tigo, Zain na TTCL nawapata pasi na tatizo. Nina watu kama 20 wenye namba za Vodacom hakuna mawasiliano kabisa kutokea nje ya Tanzania. Swali ni je Vodacom wameamua kuachana na simu zote zinazotoka nje ya Tanzania na hasa zile zinazotumia kadi maalum za International call au mitambo yao ina matatizo?.