A
Anonymous
Guest
Nimekuwa mhanga wa kufungiwa laini yangu ya uwakala kwa sababu ya kufanya miamala batili ambayo mimi sijui kama ni batili kwani tangu nipate laini hiyo sijawahi kupata semina au mafunzo yoyote juu ya miamala batili.
Tukio hili limetokea mwaka huu mwezi wa 6 baada ya kupiga menu ya voda *150*00# kutaka kufanya miamala ndipo ujumbe wa kuonyesha kuwa laini yangu haijasajiliwa kutoa huduma za M-pesa, nilipopiga simu huduma kwa wateja niliambiwa nifike Vodashop iliyo karibu nami (naihifadhi) baada ya kufika niliambiwa laini yangu ya uwakala kuwa imefungwa ila kwenye mfumo hawajaandika sababu ya kuifungia kama ilivyozoeleka kwamba laini ikifungwa inaandikwa sababu iliyopelekea ifungwe.
Niliongea na yule jamaa pale voda shop akaniambia nitoe 10,000 wafanye ku-renew ili itakapokutana kufunguka kwenye menu kawaida ndipo waiombee ifunguliwe lakini mwisho wa siku ilishindikana.
Ndipo ikabidi niulize kwani hiyo miamala batili ni ipi hiyo ? Nikaambiwa ni kukata miamala yaani mteja akija mfano na 100,000 wewe badala ya kutuma 100,000 kwa pamoja ukatuma 50000 kwanza baada ya mda ukatuma 50000 tena au wakala mkuu akikuwekea float ya 1,000,000 na wewe ukamtumia tena wakala mwingine.
Sasa kwa hizo sababu kosa langu hapo ni nini kuna wateja anakuja kutuma au kutoa ela mfano anatuma 50000 baadae akasema ongeza 30000 je natakiwa niache kutuma hiyo ili nisionekane nafanya miamala batili ? Na je wateja watakuelewa ?
Hii kitu inaumiza sana na sio mimi tu watu wengi wamefungiwa na ela zikiwemo