Vodacom wamenifanyia unyama, kesho naenda makao makuu na mwanasheria wangu.

Mkuu hili tatizo limenipata pia.
Nilideposit 20k tar 14 Nov.
Nimetumia hiyo bando siku mbili, leo asubuhi naambiwa sina salio.


Nimezungumza nao wanasema suala langu linashughulikiwa ndani ya 24hrs.

Vodacom wamekuwa hawaaminiki siku hizi
 
Tigo hawaoneshi salio la kifurushi leo siku zaidi ya tano.
Wanasema utatumiwa ujumbe wa SMS shortly wa salio. Haziingii hizo sms milele.
Kifurushi kinakata Kama upepo. Nimerudi Airtel.
Hawa niliwakaba 2007 walinirudishia salio tiGo pesa 25,000. Walikuwa wananiletea matokeo ya soka kwa meseji halafu wanakata hela km 200 kila meseji, sasa wataanza matokeo ya EPL na wapi huko sijui wanakata usiku wa manane wakati nina matokeo tayari. Kiliwaka kwa meneja pale Majani ya Chai wakawasiliana na wahindi in 5 days wakashusha muamala. Nililewaje sasa...!!!!????
 
Voda mi wananikera sana ukitaka kupiga simu kuongea na hduma kwa Wateja... Aiseee utaongea na robot mpaka basi
 
Mimi huwa nanunua bundle la 24 hrs kulingana na matumizi yangu ya siku hiyo.

Hii ni kote( intaneti na dakika).

Na kama hakuna ulazima naendelea na mambo mengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…