KERO Vodacom wananikata hela ya Uwakala, nikiuliza wanasema kuna miamala batili, lakini hawathibitishi kivipi!

KERO Vodacom wananikata hela ya Uwakala, nikiuliza wanasema kuna miamala batili, lakini hawathibitishi kivipi!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Vodacom wananikata hela ya Uwakala, nikiuliza wanasema kuna miamala batili, lakini hawathibitishi kivipi!

Nimekuwa nikikatwa pesa katika kamisheni yangu ya miamala ya uwakala na M-Pesa nikifuatilia naambiwa kuwa nimefanya miamala batili bila maelezo zaidi

Mimi ni wakala wa M-pesa, hivi karibuni vodacom wamekuwa wakinikata hela ya malipo (commission) hivo kunipa hela pungufu.

Awamu ya kwanza kwenye laki 3 walikata elfu 80, awamu ya pili laki nne wakakata elfu 70 na hivi huu mwezi nilikuwa nategemea hela isiopungua laki 3 na 90 elfu lakini cha ajabu nakutana na elfu 80 maana yake laki 3 na kitu yote wamekata kwa kile wanachoita miamala batili ambapo ukiuliza ni ubatili upi huambiwi baadala yake unaambiwa nenda Voda Shop.

Kiukweli mimi nakosa tu namna ya kuifikisha hii kesi ya dhuluma TCRA. Hii ni dhuluma ya waziwazi mtu kufanya kazi mwezi mzima anatengeneza laki 4 kasoro then anapewa elfu 80.

Nimewasilisha changamoto yangu lakini bado hakuna msaada mkubwa ninaopewa zaidi tu ya kuoneshwa miamala iliyokatwa. Utaoneshwa tu ila hela hairudi na miamala mingi ni halali

Kila nikiwapelekea hiyo changamoto Voda shop kama wanavyonitaka, wao kazi yao ni kuonesha tu statement ya miamala iliyokatwa ambayo sasa wewe wakala ujiridhishe ambayo hata ukikubali au ukatae kwamba ni halali au sio halali wao kurudisha hela haiwezekani tena wanasema ni mfumo.

Hata hivyo, ni mimi tu ndo nimepresent hii changamoto lakini kimsingi ni mawakala wengi sana wamefanyiwa hivi haswa huu mwezi.
 
Ndugu kuna kamfumo kawizi kapo kwenye hiyo mitandao sana sana hao YAS ni wezi sana ch
 
Back
Top Bottom