denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,509
- 68,228
Bodi ya ligi (TPLB) imesema kampuni ya mawasiliano ya simu Vodacom iliyokuwa mdhamini wa ligi kuu imeacha hasara ya bilioni 2.5.
Hiyo ni kutokana na kampuni hiyo kushindwa kutimiza masharti ya kwenye mkataba kutoa kiasi cha shilingi bilioni 3 kila msimu, na badala yake kutoa milioni 500.
Makubaliano hayo ambayo yalikuwa ya siri yalifikiwa kati ya Vodacom, bodi ya ligi, na vilabu baada ya Vodacom kulalamika hali yao imekuwa mbaya kiuchumi, na kuahidi kumalizia kiasi hicho msimu wa 2022/2023 wakati mkataba wao unaisha 2021/2022.
Kasongo amesisitiza bodi iliwaomba Vodacom kutoa kiasi cha shilingi milioni 600 ambazo ni robo ya bilioni 3 kwa makubaliano ya siri, lakini kwasababu siri hiyo imevuja, sasa milango iko wazi kwa mdhamini mwingine kujitokeza kuidhamini ligi hiyo.