Vodacom yaacha hasara ligi kuu

Vodacom yaacha hasara ligi kuu

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,509
Reaction score
68,228
Bodi ya ligi (TPLB) imesema kampuni ya mawasiliano ya simu Vodacom iliyokuwa mdhamini wa ligi kuu imeacha hasara ya bilioni 2.5.

Hiyo ni kutokana na kampuni hiyo kushindwa kutimiza masharti ya kwenye mkataba kutoa kiasi cha shilingi bilioni 3 kila msimu, na badala yake kutoa milioni 500.

Makubaliano hayo ambayo yalikuwa ya siri yalifikiwa kati ya Vodacom, bodi ya ligi, na vilabu baada ya Vodacom kulalamika hali yao imekuwa mbaya kiuchumi, na kuahidi kumalizia kiasi hicho msimu wa 2022/2023 wakati mkataba wao unaisha 2021/2022.

Kasongo amesisitiza bodi iliwaomba Vodacom kutoa kiasi cha shilingi milioni 600 ambazo ni robo ya bilioni 3 kwa makubaliano ya siri, lakini kwasababu siri hiyo imevuja, sasa milango iko wazi kwa mdhamini mwingine kujitokeza kuidhamini ligi hiyo.
 
Kama ukweli ndio huu, kwanini TFF na bodi ya ligi wanaogopa kwenda mahakamani kudai fidia kwa Vodacom kutofikia makubaliano ya kimkataba? au wanawaogopa wasije kuzidiwa tena njaa mbele ya safari wakose pakuombea msaada.
 
Kama ukweli ndio huu, kwanini TFF na bodi ya ligi wanaogopa kwenda mahakamani kudai fidia kwa Vodacom kutofikia makubaliano ya kimkataba? au wanawaogopa wasije kuzidiwa tena njaa mbele ya safari wakose pakuombea msaada.
Umeshajijibu mwenyewe, na jibu lako ni ukweli mtupu.
 
hwa ndio walikuwa wanazuia timu nyingine zisipate udhamini wa kampuni nyingine za mawasiliano mfano African Lyon ya Zamnda ilipokataliwa udhamini wa Zantel ni wakati vilabu wavishitaki Bodi ya Ligi na mdhamini wao kwa kukiuka masharti ya mkataba.
 
Back
Top Bottom