Vodacom yaongoza kwa kutoza gharama kubwa za intaneti kwa wateja

Vodacom yaongoza kwa kutoza gharama kubwa za intaneti kwa wateja

Vodacom ina gharama kubwa kweli ila ina kasi kubwa pia. Hao wengine wame-compromise price with speed. Airtel na tigo hata bure huwezi kuniambia nizitumie maana ni mitandao ya hovyo, huduma mbovu ya wateja, kazi ya kinyonga ya mtandao.

Siku zote kitu kizuri kina gharama. Mimi binafsi hua sijiulizi sana inapokuja kwenye bei ya vifurushi vya vodacom kwa sababu hua nina uhakika na ubora wa huduma yao.

2G ya vodacom ni sawa na 4G ya airtel na tigo kwenye kasi.

Mwisho, serikali ipungize au iyadhibiti makampuni ya simu kwenye vifurushi, inaonekana yanajipangia bei ya vifurushi, hakuna usimamizi.
 
Gharama hizo ni endepo hujajiunga na kifurushi,ila wajue kwamba hata ukijiunga na kifurushi cha GB 10 unashangaa unaambiwa kifurushi chako kimeisha,utaona msg MB za kifurushi chako ziko chini ya 15MB mara paap zimeisha hata kama hujawasha data,swali najiuliza huwa wanazikusanyiwa wapi hz MB zetu hazijai tu siku wakatoa hata offer..
Hapo kwenye mb kweli tatizo
Vodacom ndo kama hivyo
TTCL wao ukiona sms "mb chini ya 50" basi ujue huna raund na huambiwi
Halotel ndo utapata tabu sana kama hukuuliza salio unaweza ukadhani mtandao unazingua kumbe ndo bando limeisha
Bora kwenye tigo GB yao ya buku ya wiki inadumu dumu

Lakini wote hao wanazingua hii ya kutuletea "bundle expiry time" WEZI WAKUBWA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haswa wanakela kweli kweli
hakuna kitu kinanikera kwenye voda kama ukitaka kuaccess account yako ya benk na kufanya miamala kama line ya simu haina salio huwezi kuingia, wakati mitandao mingine hata kama huna salio unaweza ku access account yako bila shida na kufanya miamala yako bure kabisa
 
Sisi wa halotel vipi haituhusu? Maana najua mb ni halotel! Kwa tz.
 
Halotel babalao....Kwa TSh.1000/= unapata 1024MB (1GB) ya kutumia wiki nzima. Voda naitumiaga tuu kwenye miamala ya M-PESA na kupiga ni Airtel.
Smile vifurushi vyao vipoje? Mwenye kutumia huo mtandao tujuze tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom