Vodacom yaongoza kwa kutoza gharama kubwa za intaneti kwa wateja

Vodacom ina gharama kubwa kweli ila ina kasi kubwa pia. Hao wengine wame-compromise price with speed. Airtel na tigo hata bure huwezi kuniambia nizitumie maana ni mitandao ya hovyo, huduma mbovu ya wateja, kazi ya kinyonga ya mtandao.

Siku zote kitu kizuri kina gharama. Mimi binafsi hua sijiulizi sana inapokuja kwenye bei ya vifurushi vya vodacom kwa sababu hua nina uhakika na ubora wa huduma yao.

2G ya vodacom ni sawa na 4G ya airtel na tigo kwenye kasi.

Mwisho, serikali ipungize au iyadhibiti makampuni ya simu kwenye vifurushi, inaonekana yanajipangia bei ya vifurushi, hakuna usimamizi.
 
Hapo kwenye mb kweli tatizo
Vodacom ndo kama hivyo
TTCL wao ukiona sms "mb chini ya 50" basi ujue huna raund na huambiwi
Halotel ndo utapata tabu sana kama hukuuliza salio unaweza ukadhani mtandao unazingua kumbe ndo bando limeisha
Bora kwenye tigo GB yao ya buku ya wiki inadumu dumu

Lakini wote hao wanazingua hii ya kutuletea "bundle expiry time" WEZI WAKUBWA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haswa wanakela kweli kweli
 
Sisi wa halotel vipi haituhusu? Maana najua mb ni halotel! Kwa tz.
 
Halotel babalao....Kwa TSh.1000/= unapata 1024MB (1GB) ya kutumia wiki nzima. Voda naitumiaga tuu kwenye miamala ya M-PESA na kupiga ni Airtel.
Smile vifurushi vyao vipoje? Mwenye kutumia huo mtandao tujuze tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…