D
DeletedMember281674
Guest
Wanabodi
Kama kawaida yangu, nikisikia kitu, kama kitu hicho kina maslahi kwa taifa, huwa naki share.
Tangu Makamu Rais Mstaafu, Balozi Dr. Emmanuel Nchimbi aandike barua ya kustaafu kwa shinikizo, hakuwahi kuonekana tena hadharani.
The Chrological of Events
Baada ya kuandika barua ile ya kustaafu siku ya Jumanne, ambapo barua hiyo haikua ombi la kustaafu, ilikuwa ni taarifa ya uamuzi wa kustaafu kwenda kwa mamlaka yake ya ajira, Ikulu ikatoa taarifa kuwa ni ombi la kustaafu na limekubaliwa na rais wa JMT.
Kesho yake Jumatano alitarajiwa kuonekana akihudhuria kikoa cha CC na NEC vya CCM, lakini hakuonekana!
Kikao cha NEC kikamjadili in absentia na kufikia maamuzi ya kufutia uanachama wake wa CCM, hivyo kuitengua ile barua yake ya kujiuzulu na badala yake kumfuta kazi! na kupendekeza jina la VP mpya.
Siku ya Uapisho wa VP mpya akitegemewa kuwepo, hakuwepo.
Siku VP mpya akiripoti kazini, akitegemewa kuwepo, kukabidhi ofisi, katika hafla fupi ya makabidhiano ili kuuthibitishia ulimwengu a smooth transition, hakuwepo.
Kutoonekana kwake public, kumezua taharuki, hata mhimili wa nne wa Media ambao ulipaswa kumtafuta kumhoji sababu za kujiuzulu kwake, umepigwa ganzi!. Baada ya CCM kutoa taarifa ya kumfutia uanachama wake, media ilipaswa kuihoji CCM, kama uamuzi huo umefuata the due process, au CCM nayo sasa inaiga Chadema zile kangaroo cours zake za timua timua!, kila aliyetimuliwa CCM, ile due process huwa inatangwa na taarifa ya kufutw uanachama hutolewa ikieleza sababu, lakini kufutwa huku, CCM haikutoa sababu na media imepigwa ganzi haijahoji!.
Kwenye hili la VP, media ilipaswa itimize wajibu wake kikamilifu kama mhimili wa nne kwa kufanya IJ, kuwaeleza Watanzania what really happened what transpired behind the closed doors, hata kumtafuta tuu, kujua alipo, kumpiga picha kuwaonyesha Watanzania kuwa huyu mtu yupo ni mzima bukheri wa afya, yuko salama!, media tumeshindwa hivyo kuzidisha taharuki huku watu wakidhani ama wamemkolimba, kama Horace Kolimba, ama wamempolepole kama balozi Polepole, ila hofu na wasiwasi wa ukweli umetanda.
Na mimi kama binadamu tuu wa kawaida ambaye pia ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, mtangazaji wa kujitegemea na wakili wa kujitegemea, nilikuwa na wajibu wa kufanya IJ, na kutoa legal Opinion, kama kilichofanya na CCM kumshitaki mtu mwenye kinga ya kushitakiwa ni legal, kumfuta kazi mtu aliyestaafu mwenyewe kwa hiyari ni legal, sikuyafanya yote hayo, na mimi nimepigwa ganzi!, huku nikibaki kujiuliza tuu mwenyewe na kujijibu!.
Ndipo nikaisikia ile sauti, The Voices From Within toka ndani yangu, imenieleza kuwa Makamu Rais Mstaafu Balozi, Dr. Emmanuel Nchimbi yuko salama uu salmini, amejituliza tuu nyumbani kwake, ni yeye mwenyewe ndio kaamua kuzima simu zake, kutulia tuli na kuendelea kutafakari walichomfanyia, lakini hajazuiliwa, hajashikiliwa, haja kolimbwa wala haja polelepoleshwa!, yupo salama ila ameamua mwenye to lie low kwa kunyamaza kimya, maana ukimya nao pia ni jibu!.
NB. Hizi voices from within zangu, huwa ni unaisikia tuu sauti inakuambia jambo fulani, huwezi kuiliza chochote, wala haukupi sababu yoyote, ni unaambiwa tuu kitu, and that is it, hivyo na mimi pia huwa naomba, msiniulize kitu, maana sio mimi ni sauti tuu niliyoisikia!.
Kwa faida ya wale wageni wa voices from within zangu karibuni mitaa hii
- Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
- Tarehe 12 March 2016 saa mbili usiku nilipandisha humu bandiko hili Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa ... angalia kilichotokea na kilitokea lini! Mh. Paul Makonda ateuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar ...
https://www.jamiiforums.com/threads...a-kuwa-mkuu-wa-mkoa-wa-dar-es-salaam.1020403/- Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini...
Pascal Mayalla na the "Voice From Within" ila ni ...
Pascal Mayalla na Voices from within, Je ni utabiri au ndio ...
Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa ...
https://www.jamiiforums.com/threads...-je-ni-utabiri-au-ndio-ukweli-halisi.2015540/
Nawatakia Jumamosi Njema
Mzee Pasco
Watapita nae tu kama walivyopita na Ndugai...tumpe muda tu, kama Mpishi wake DGIS alipita nae bado yeye tu ...it's just a matter of time.
MUNGU akailaze roho yake mahali pema peponi in advance