Voices From Within: Unaweza usiamini! Aliyetoa A Go ahead kwa Mdee na Wenzake ni Kigogo wa Chadema!. Alikuwepo Ukumbini na Vikaoni! Je, ni nani?

Voices From Within: Unaweza usiamini! Aliyetoa A Go ahead kwa Mdee na Wenzake ni Kigogo wa Chadema!. Alikuwepo Ukumbini na Vikaoni! Je, ni nani?

Sijasikia Pascal akiandika kuhusu kauli za Wabunge wa CCM Akina Msukuma na wengine, sijasikia akizungumziw kuhusu Bei ya Mafuta, sijasikia akizungumzia kuhusu Kada wao Anayesota gerezani Sabaya, yeye kutwa kucha Yuko na COVID-19 as if yeye ndio muasisi wa Chadema na mtunzi wa Katiba
 
Kama Mbowe anafanya hivi.Basi yeye na Zitto Kabwe hawana tofauti.Inawezekana hata CCM kule kuna Mambo anatuficha.Ukweli utakuja kujulikana tu siku moja.
Swali linabaki pale pale kwa wale waliokuwa kifungoni je walitolewa kifungoni kwa idhini ya Mbowe?? Na kama walitolewa kwa idhini ya Mbowe ,yeye Mbowe alikuwa nani katika utawala wa yule shetani?? Awamu ya tano ilijaa figisu figisu nyingi,chaguzi za 2019 na 2022 je ziliratibiwa na Mbowe??
 
Paschal,
Kuna shida mahali kwenye mfumo wako wa kufikiri. Hoja hii hii umeiotoa siku mbili zilizopita ukasema hayo hayo. Na umeulizwa maswali mengi sana
Hasa suala la Nusrat alitokaje magereza hujajibu.

Chadema waliomba tume ya uchaguzi wapewe nakala ya uteuzi wa wabumhe hao haikuitoa hadi leo.

Chadema wakasema kuna forgery polisi na vyombo hawajachunguza hadi leo.

Huyo kigogo anayewalinda ni wa serikali au chadema?

Kwa nini kama walikua na baraka ya chama waliapishiwa garage/jikoni na sio kwemye ukumbi wa bunge kama ilivyozoeleka?

Kwa nini Ndugai alijitapa kuwatetea hadi mwisho tofauti na wabunge wengine?

Mojawapo ya mtu mwemye tatizo la afya ya akili ni kuweweseka, kusikia sauti ambazo yeye mwenyewe ndio anazisikia "the voice from within". Ukisoma post hii na kuelewa kamtafute psychiatrist akuponye. Sababu umesahu muda si mrefu umetoka kusema hayo na umesahau. Pia umesema unasikia sikia sauti au echo ambazo zinakupa hizo taarifa kiongozi wa chadema ndio
..

Kama unachotaka kukisema unakifahamu be a man sema Paschal ndio aliyefanikisha huo mchongo kwa kushirikiana na kigogo.
Ukisoma wakati wa kigogo14 aliwahi kumtuhumu mtu lakini alishindwa kutoa ushahidi naona Paschal kapata sauti ya kigogo14 na kusingizia kigogo wa chadema
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, mimi Mzee wa "the voices from within" na Maswali Fikirishi.

Angalizo la Mambo ya Sauti.
Kuna mambo ni yetu, na mambo mengine sii yetu, mambo ambayo ni yetu, unaweza kuuliza, lakini kwa mambo ambayo sii yetu, huwezi kuuliza, miongoni mwa mambo ambayo sii yetu ni pamoja na haya mambo ya mtu kusikia sauti, ni unasikia tuu, hakuna sababu yoyote, wala ushahidi wowote ni unajikuta umeambiwa tuu.

Hapa nimesikia sauti ambayo mimi huwa naiita ""Voices From Within", hii voices from within, ni sauti ambayo unaisikia kutokea ndani yako, inakuambia kitu fulani, huwezi kuiuliza chochote ila unaweza kujiuliza kama hicho ulichoambiwa its makes sense, na kina logic, then inajiuliza nikiseme au nisiseme, unajifanya self objectivity assessment kwa kujiuliza nikisema kina faida, kitasaidia, au ninyamaze just to keep to myself. Unajifanyia self censorship, kisha unafikia maamuzi kusema ili kuwajulisha na wengine lakini sio lazima useme kila ulichosikia.

Hizi sauti ziko za aina nyingi, wengine huoteshwa kama ndoto, wengine huonyeshwa kama visions, na wengine, haswa ma deep thinkers, likitokea jambo, ukalifikiria sana, wakati umetulia, usually usiku mkubwa, kwenye ukimya na utulivu, ndipo unaisikia hiyo sauti au vision, wabunifu na wavumbuzi wengi hivi ndivyo wanavyovumbua!. Archimedes alipovumbua law ya floatation, alikuwa bafuni akioga kwenye bath tub, alitoka hivyo hivyo alivyo from the bathroom hadi mtaani huku akipiga kelele "eureka!, eureka!, ... yaani nimegundua, nimegundua, wala hakukumbuka tena kama alitoka hivyo hivyo bafuni kama alivyozaliwa!, wastaarabu wakamdaka kwa kunshika kwa nguvu kumsitiri wakijua ni kichaa!. Hata Sir Isaack Newton, mvumbuzi wa Newton's laws of motion, kuna siku alikuwa anapima yai linaanza kuchemka dakika ya ngapi, akachukua saa akaiweka kwenye sufuria, na kuichemsha huku amelishika yai mkononi akipima muda!, alikaa hivyo muda mrefu hadi mkewe akamuuliza ndipo akashtuka.

Hiki nilichosikia, unaweza usiamini!., unaweza kuniona Pasco ni kichaa fulani, haijalisi ni sauti ya nani, just take it or lleave it, ikitokea ikiwa kweli, wewe mwana jf, unakuwa na a jf advante "be the firts to know" kumbe aliyetoa a go ahead kwa kina Mdee na kundi lake, ni kigogo wa Chadema!. Mimi niliuliza humu mkaniona kama ni kichaa fulani.

Sasa sauti imeniambia the one behind hii saga yote ya kina Mdee, ni Kigogo mmoja mkubwa tuu wa Chadema!. Sauti hiyo imeniambia Kigogo huyo alikuwepo ukumbini, kwenye vikao vyote viwili vilivyowatimua kina Mdee!. Jee Kigogo huyu ni nani?, andamana nami....

Nilikuwa nachangia mada hii

Kamati Kuu ni mamlaka ya nidhamu ya wabunge but not Halima. Kesi ya wabunge iliendeshwa kikangaroo hivyo hukumu ile ya CC ni batili.

Baraza Kuu ndio mamlaka ya rufaa ya wabunge. Baraza Kuu lilipaswa kwanza kujiridhisha kama CC ilitenda haki, halikufanya, likaubariki ukangaroo wa CC!. Hapa sasa ndio mamlaka ya nidhamu ya Halima Mdee. Hakuna kesi yoyote ya Halima iliyowasilishwa Baraza Kuu. CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka kufukuza Halima wakati hata Baraza Kuu halina mamlaka hiyo?!. Kesi ya Halima ingetoka Baraza Kuu na kuingia Mkutano Mkuu ndio pekee wenye mamlaka hiyo. Kilichofamyika ni uhuni, ambao mimi nimeuita ni ukangaroo.

Kitendo cha kukazia hukumu batili nao ni ukangaroo!.

Rufaa zote lazima zifuate kikao kinachofuatia, Halima alikata rufaa Baraza kwasababu CC sio mamlaka yake ya nidhamu na haina uwezo wa kumfukuza!.

Hawaeezi chochote kwasababu hakuna kikao chochote kilichowateua, kule NEC hawahitaji taarifa za kikao, wanahitaji barua ya uteuzi na fomu zilizosainiwa. Barua ilikuwepo na fomu zilikuwepo na hapa ndipo nikaisikia sauti from within kuwa mtu aliyewapa go ahead kina Mdee ni Kigogo mmoja wa Chadema, ni mjumbe wa CC na siku ya kikao cha Kamati Kuu Chadema, kilichokaa kama a Kangaroo court na kuwatimua, alikuwepo!. Siku ya Kikao cha Baraza Kuu, kubariki ule Ukangaroo wa Kamati Kuu Chadema alikuwepo ukumbini!. Sauti Imeishia hapo.

Jee Kigogo Huyu ni Nani?.

Kule nyuma nimawahi kutoa tuhuma kuwa Chadema kuna kirusi, leo nilitaka ku update huu uzi CHADEMA Kuna Kirusi! Je, Unajua kirusi hiki ni Nani?! Na The Motive Behind? kwa kirusi hiki kipya, nikakuta umefungwa!, kumbe I was wrong, sio kuwa Chadema kuna "ki"- rusi!, Chadema kuna "vi" rusi! maana ni more than one!. Jee unaweza kuamini aliyasaini barua za kina Halima ni mnene mmoja wa Chadema ambaye ni mjumbe wa CC na alikuwepo ukumbini kwenye kikao cha Kamati Kuu na Kikao cha Baraza Kuu?!.

Can you mu imagine Kigogo huyu ni nani?. Anza kutafakari, mimi nitakusaidia

Nilitamani kumalizia nikupe kitu kamili lakini sisi sekta binafsii maisha yetu ni ya kukimbizana, kufukuzia tenda, tenda nyingi deadlines zake ni Monday, hivyo kuna tenda nakimbizana nayo, deadline yake ni saa 4:00 asubuhi hii

Nitarejea...
ila Matokea ya Kikao cha Baraza Kuu Chadema kuwatimua waanawake wa shoka, mashujaa 19 wa Chadema waliokipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu, bado yanatawala mijadala mbalimbali humu jf.

Anza kwa kutembelea haya mabandiko haya anzia
hapa Ni Ubatili Mtupu Mpaka Basi!. CC ya CHADEMA ilipata wapi mamlaka?. Baraza Kuu halina mamlaka hiyo!. Je, inawezekana CHADEMA ni chama majanga ila?
na A Kangaroo Court Moja, Kutoa Hukumu Kikangaroo, Kisha Kikao cha Rufaa, Kikiyabariki Maamuzi yale ya Kikangaroo. Je, nacho ni A Kangaroo?
na Je, wabunge 19 wa CHADEMA walijiteua? Je, CC ya CHADEMA ni Kangaroo Court? Je, Baraza Kuu litabariki ukangaroo ule?
na Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.
na CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao
na Mmezoea vya kunyonga hamviwezi vya kuchinja. Hongera sana Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji
na Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu
na Kufanya Kosa Si Kosa, Kosa Kurudia Kosa, CHADEMA is Almost Dead, Due to deadly mistakes!, This Your Only Survival, Do or Die!, Msirudie Kosa!.
na Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane!
na Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

na JPM, CCM wakishinda, Freeman Aikaeli Mbowe ni lazima ajiuzulu, amwachie Tundu Lissu. Lissu aache Uanaharakati, aonyeshe Statesmanship

na For the sake of National Unity, Je tumshauri Dkt. Magufuli aahidi kumteua Tundu Lissu kuwa Mbunge?

Paskali
Kwa mantiki hii kila kitu hapa ni mchezo wa kuigiza! Kwa sisi tulio nje ya mifumo yao tunaamishwa ndivyo sivyo! Umenifikirisha juu ya hatma ya uongozi wa nchi yetu.
Kama ndivyo ilivyo basi itachukuwa muda nchi yetu kupata chama mbadala wa kuchukua dola.
 
Kaka Pascal Mayalla, kwanini jambo hili likunyanyase na kukunyima usingizi kiasi hiki? Uliwahi kuchambua, kama ufanyavyo hapa, alipofukuzwa uanachama wa CCM Mama Sophia Simba?

Halafu, unapotaka kueleweka pale unapozungumzia sheria ni vyema kuweka vifungu vya sheria husika. Viko wapi vifungu vya Katiba ya CHADEMA unavyojengea hoja yako? Hebu waache CHADEMA wamalizane wao kwa wao, pilipili usioila yakwashia nini kaka? Ha ha ha ha ha
Mwendazake aliwahi kusema"Mayala ni Njaa"
Paskali kama Paskali hana matatizo. Lakini pale Mayala alipovurugwa na Teuzi za kuishambilia CHADEMA , Mayala amekuwa Njaa Kweli Kweli.
 
Mzee Mayalla mbona hili suala linakupelekesha hivi? wewe andika yote ila naomba elezea suala la mtu alitoka magereza usiku na kuwa mbunge straight.

Waende mahakamani tukashuhudie vichekesho Ndugai na Mahera wakipanda kizimbani kujieleza
Mh, yaani ni KADA wa CCM at the same time ni MWANAHARAKATI wa CDM kudai HAKI ndani ya chama. Tutaona mengi .
 
Paschal,
Kuna shida mahali kwenye mfumo wako wa kufikiri. Hoja hii hii umeiotoa siku mbili zilizopita ukasema hayo hayo. Na umeulizwa maswali mengi sana
Hasa suala la Nusrat alitokaje magereza hujajibu.

Chadema waliomba tume ya uchaguzi wapewe nakala ya uteuzi wa wabumhe hao haikuitoa hadi leo.

Chadema wakasema kuna forgery polisi na vyombo hawajachunguza hadi leo.

Huyo kigogo anayewalinda ni wa serikali au chadema?

Kwa nini kama walikua na baraka ya chama waliapishiwa garage/jikoni na sio kwemye ukumbi wa bunge kama ilivyozoeleka?

Kwa nini Ndugai alijitapa kuwatetea hadi mwisho tofauti na wabunge wengine?

Mojawapo ya mtu mwemye tatizo la afya ya akili ni kuweweseka, kusikia sauti ambazo yeye mwenyewe ndio anazisikia "the voice from within". Ukisoma post hii na kuelewa kamtafute psychiatrist akuponye. Sababu umesahu muda si mrefu umetoka kusema hayo na umesahau. Pia umesema unasikia sikia sauti au echo ambazo zinakupa hizo taarifa kiongozi wa chadema ndio
..

Kama unachotaka kukisema unakifahamu be a man sema Paschal ndio aliyefanikisha huo mchongo kwa kushirikiana na kigogo.
Ukisoma wakati wa kigogo14 aliwahi kumtuhumu mtu lakini alishindwa kutoa ushahidi naona Paschal kapata sauti ya kigogo14 na kusingizia kigogo wa chadema
Ufafanuzi ulioenda shule ndiyo huu,hawa akina Pascal Mayalla wanafanya watu watukane bila sababu yoyote,hata kama ni upagani siyo hivyo,kuwa mwandishi wa habari za uongo uongo na uchonganishi,kwa vile ni watu wanaotoka kanda ile ile ya mateso mateso basi kwao mateso na uongo ni halali.
 
Back
Top Bottom