Kupiga kura ingia link hii ⬇ inakupeleka category yake afu piga kura mara nyingi uwezavyo, unabonya neno vote pembeni ya picha ya diamond afu jibu unalopewa unakuwa unalikata (cancel) ili kuendelea kupiga kura, hata mara 20000 ili aibuke kinara best worldwide act kati ya washindi 6 duniani wataopatikana kwenye hiyo category (America, Europe, etc)
Usijali sana, tupo wengi na kura zetu zinatosha kumpa ushindi. Angalia leo kaja na tuzo tano, akiwa bado hata hajatia mguu bongo tuzo ya sita ikamkuta njiani. Kura zetu zinatosha sana, hii tuzo ya saba ni muhimu tuipate, na tutampigia. Hatuna porojo, hapa ni kazi tu, kazi ya kupiga kura na kuzileta tuzo nyumbani. Kwa taarifa yako tu, kwa hii 2015 ameshashinda tuzo nane za kimataifa.