Iamjac16
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 214
- 53
Baada ya kufuatilia usajili wa timu mbalimbali nategemea kuona ligi ya msimu huu wa 2020/2021 utakua msimu wenye ushindani wa hali ya juu kulinganisha na misimu ya nyuma. Simba ambao ni mabingwa watetezi wameendelea kuimarisha kikosi chao kwa malengo ya kuongeza ushindani katika ligi ya ndani pamoja na Caf champions kwa kuongeza wachezaji saba pia Watani Zao Yanga wanaendelea kujiimarisha katika usajili kwa lengo la kusuka kikosi cha ushindani kama wachezaji hawa wataingia kwenye mfumo haraka basi wataleta ushindani wa hali ya juu kwani wanauwezo na uzoefu wa hali ya juu, Pia timu kama Azam nayo inaonyesha jinsi gani imedhamiria kuweka heshima na kutaka kuwa mshindani wa kweli katika ligi ya msimu huu.kila timu inasajili kwa umakini hivyo kutakuwa na ushindani.