VPL 2020/21 itakuwa na ushindani wa hali ya juu

VPL 2020/21 itakuwa na ushindani wa hali ya juu

Iamjac16

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
214
Reaction score
53
Baada ya kufuatilia usajili wa timu mbalimbali nategemea kuona ligi ya msimu huu wa 2020/2021 utakua msimu wenye ushindani wa hali ya juu kulinganisha na misimu ya nyuma. Simba ambao ni mabingwa watetezi wameendelea kuimarisha kikosi chao kwa malengo ya kuongeza ushindani katika ligi ya ndani pamoja na Caf champions kwa kuongeza wachezaji saba pia Watani Zao Yanga wanaendelea kujiimarisha katika usajili kwa lengo la kusuka kikosi cha ushindani kama wachezaji hawa wataingia kwenye mfumo haraka basi wataleta ushindani wa hali ya juu kwani wanauwezo na uzoefu wa hali ya juu, Pia timu kama Azam nayo inaonyesha jinsi gani imedhamiria kuweka heshima na kutaka kuwa mshindani wa kweli katika ligi ya msimu huu.kila timu inasajili kwa umakini hivyo kutakuwa na ushindani.
 
Namungo nao wamesajiri vifaa hatarii
 
Simba ikitolewa CAF mapema...hakutakua na ushindani kama msimu huu tu...yatabaki malalamiko na hata isipotolewa bado sijaona waliojipanga kuchukua kombe..

Yanga wako busy kudanganya mashabiki wao...Azam wanajiandaa kuwatoa Yanga nafasi ya pili pia wachukue na FA Cup.
 
Back
Top Bottom