VPL: Azam FC Vs Simba SC Disemba 12, 2015

VPL: Azam FC Vs Simba SC Disemba 12, 2015

Habari wakuu,Baada ya kipindi kirefu kidogo, ligi kuu Tanzania bara inarejea na mechi yenye hamasa zaidi leo ni kati ya Azam FC na Simba SC wakiendeleza vita ya kugombania ubingwa. Azam anaingia kwenye mechi ya leo akiwa amekalia siti ya dereva na kushikilia usukani wakati Simba akiwa nafasi ya nne akitofautiana pointi nne na vinara, ni mechi muhimu kwa timu zote.Tuwe sote pamoja mishale ya saa kumi alasiri kutoka uwanja wa Taifa kujua pumba na mchele kwenye mechi ya leo. Mechi nyingine leo, Yanga ameenda Tanga kumvaa Mgambo, Mtibwa yuko Mbeya kumvaa Mbeya city, Kagera sugar anamkaribisha Ndanda Kaitaba, Stand anavaana na Mwadui na kutoka Songea, Majimaji anaikaribisha Toto Africans ya Mwanza. [TABLE="align: center"][TR][TD]Pos [/TD][TD] Club [/TD][TD] P [/TD][TD] W [/TD][TD] D [/TD][TD] L [/TD][TD] GF [/TD][TD] GA [/TD][TD] GD [/TD][TD] PTS [/TD][/TR][TR][TD] 1 [/TD][TD] Azam FC [/TD][TD] 9 [/TD][TD] 8 [/TD][TD] 1 [/TD][TD] 0 [/TD][TD] 20 [/TD][TD] 5 [/TD][TD] 15 [/TD][TD] 25 [/TD][/TR][TR][TD] 4 [/TD][TD] Simba SC [/TD][TD] 9 [/TD][TD] 7 [/TD][TD] 0 [/TD][TD] 2 [/TD][TD] 15 [/TD][TD] 5 [/TD][TD] 10 [/TD][TD] 21 [/TD][/TR][/TABLE]
===============
00' Kipenga kinapulizwa kuashiria mwanzo wa mchezo00' :A S soccer:Goooooal, Azam wanapata goli la mapema sekunde ya 56 baada ya John Bocco kutia mpira kimiani06' Azam wanajaribu tena kuingia langoni mwa Simba lakini mpira unaishia mikoni mwa golikipa08' Simba wanapata kona ya kwanza ya mchezo, hata hivyo haikuzaa matunda kwa Aishi Manula12' Twite anawekwa chini, mpira wa adhabu kuelekea Simba ulipanguliwa na kipa kuzaa kona ambayo haikuzaa matunda14' Farid Mussa anakosa goli baada ya kupiga pembezoni kidogo mwa goli.24' :A S soccer:Gooooal, Ibrahim Ajib anasawazisha goli baada ya kupokea pasi nzuri.26' Kadi ya njano kwa Ajib kutokana na kuvua shati wakati akishangilia goli27' John Bocco anakosa goli baada ya kipa kuweza kutoa mpira na kupelekea kona ambayo haikuzaa matunda28' Danny anakosa goli baada ya Manula kujinyoosha na kufanikiwa kuutoa mpira, kona haikuzaa goli34' Kipre anapewa kadi ya njano kwa kujiangusha eneo la hatari37' Simba wanapoteza nafasi nzuri ya kuongoza baada ya kumlenga kipa Manula41' Danny anapata mpira uliorudishwa nyuma, hata hivyo alishindwa kukimbizana na kasi na kuupiga juuu45' Dakika mbili zinaongezwa45+1' Simba wanacheza gonga nzuri golini mwa Azam lakini Aishi anatibua mpango45+2' Kipenga kinapulizwa kuashiria mapumziko=======Matokeo kutoka viwanja vingine(Half Time)Mgambo 0-0 YangaStand 0-1 Mwadui
A%20S%20soccer.gif
Fabian NgwanseMbeya city 1-2 Mtibwa:A S soccer:Ally Sharif
A%20S%20soccer.gif
Bahanuzi=======45' Mpira umerejea kutoka mapumziko52' Ibrahim Ajib anapiga shuti kali lakini linatua mikononi mwa Manula61' Ibrahim Ajib anakosa goli baada ya kujaribu kupiga lakini hakuweza kulenga goli65' Azam wanacheza gonga nzuri kuelekea golini mwa Simba, mabeki wa simba wamefanikiwa kutibua68' :A S soccer:Gooooal, juhudi nzuri kutoka kwa Ajib na anafanikiwa kufunga goli baada ya kumtoka Said Morad69' Kiiza anaingia kuchukua nafasi ya Daniel Lyanga kwa upande wa Simba71' Kavumbagu anaingia kuchukua nafasi ya Salum Abubakar kwa upande wa Azam72' :A S soccer:John Bocco anasawazisha goli katikati ya msitu wa mabeki wa Simba, Azam 2-2 Simba.75' Kipre anakosa goli baada ya kupiga nje kidogo ya lango77' Wachezaji wa simba wanamfata mshika kibendera kwa kutoa faulo kwa Azam, faulo haikuzaa matunda80' Azam wanakosa goli kwa mpira kugonga mwamba na kumrudia mlinda mlango baada ya kumpita82' Mabadiliko pacha: Mwalyanzi anaingia upande wa Simba na kutoka Abdi banda pia Mudathir anaingia Azam84' Nimubona anatoka kumpisha Kessy upande wa Simba 90+1' Golikipa wa Simba, Vincent anapewa kadi ya njano baada ya kumvuta shati mchezaji wa Azam alipozidiwa nguvu.90+2' Kipenga kinapulizwa kuashiria mwisho wa mchezo, Azam 2-2 Simba=============VIWANJA VINGINE(FULL TIME)Mgambo 0-0 YangaStand 0-2 Mwadui
Mkuu, mechi ya Azam na Simba ni nyepesi mno kiasi kwamba ikianza chukua jembe ukalime, ikiisha uende ukavune.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom