VPL : Kagera Sugar Vs Young Africans

Wa mchangani punguza unafiki ,kila mchezaji unajifanya unamjua mara Ngasa,mara Tegete mara Mkude au wewe ni mganga wao .Huyu Maxime aliyekuwa anaifunga Yanga akiwa Mtibwa karibia kila msimu leo amekuwa mshabiki wa Yanga.
Alianza Casillas akapigwa 3 wakafanya sub wakamwingiza Burhan nae akapigwa 3 halafu kama unajua watu wananunua mechi kwa nini msirekodi au mkaenda kuripoti Takukuru/Polisi
 
Tulipo mpa toto afrika mbili pana mtu alifungua mpaka uzi "hawa toto kucheza kitoto toto wanapo kutana na yanga "
Sasa hawa leo sijui wamecheza kikagera gera? Ni utaratibu wetu kupiga watu nyingi mwaka wa jana kuna mtu alikula 8.
 
Naanza kukudharau
 

Mbona Yanga akifingwa au akidroo hamsemi kama nae ameuza mechi? Akishinda mikia mbio mbio ooh kanunua mechi
 
Mnafiki mkubwa wewe shabiki wa mbumbumbu fc,unajua rekodi ya Yanga vs Mtibwa ya Maxme? Yanga kachezea sana chini ya Maxime acha unafiki,halafu wachezaji wa zamani wa Yanga kucheza timu pinzani na Yanga sio uwahukumu eti wamekula mlungula acha ujinga wewe!!Mliwafunga Kagera goli mbili kwa shida kwa upuuzi wenu,usiwe na roho ya kichawi unaongea bila ushahidi, kama unaushahidi peleka TAKUKURU, kwa taarifa yako kabla ya Krismasi mtakuwa kwenye nafasi yenu ya misimu yote, mikia kweli mnamidomo, siku hizi watu wanacheza mpira kazi sio mapenzi ndio maana kuna wachezaji wanacheza hapo mbumbumbu fc ni Yanga damu hasa mliowasajili kutoka mtibwa msimu huu.
 
Ni aibu kwa Yanga kushangilia kuwafunga watu hawana pa kulala kwa mwezi mzima. Chakula hawana ukame. Hata kuoga yao shida. Ni Sawa na kumpiga mlemavu. Yanga hovyooo.
Simba aliposhinda alikuwa anavyo vyote hivyo??
 
Kwa umakini na umahiri wa taarifa yako, naamini una ripoti kamili ya jinsi Casillas alivyohongwa mechi ya leo. Utakuwa una 'mkanda' wote wa ufisadi wa Casillas na Maxime katika kuzihujumu Mtibwa na Simba. Ila nashangaa kwa nini mtu safi, mahiri na makini kama wewe unaficha baadhi ya watuhumiwa na kuwaanika hao wawili tu kwenye taarifa yako hii makini. Nashangaa zaidi kwamba taarifa hizi za kuaminika na zilizotafitiwa kitaalamu umebaki nazo bila ya kuziwasilisha TAKUKURU. Nakuomba sana ziwasilishe huko. Zitadaidia sana kuondoa virusi vya ufisadi ndani ya mfumo wetu wa Soka. Bila ya kufanya hivyo watu watakuwa na haki ya kukuona fisadi zaidi kuliko hao unaowatuhumu, au mbunifu kuliko waongo wote duniani kama siyo mpuuzi kuliko majuha wote!
 
Mkuu umefunguka sana. Kama kweli haya yanafanyika basi tuna safari ndefu sana kuendeleza soka letu.!

Mkuu nalijua soka la Bongo mwanzo mwisho na ' figisu figisu ' zake zote. Tena hayo niliyowaambieni hapo ni ' machache ' sana na ipo siku nitakuja ' kufunguka ' humu Watu ' wataumbuka '.
 
Naanza kukudharau

Nakushauri endelea tena zidisha huko ' kunidharau ' Mkuu. Ningekuwa nadharauliwa na Mwenyezi Mungu ningelia na kuogopa lakini kumbe nadharauliwa na ' Kibushuti ' Wewe wala sina hofu au wasiwasi.
 
Nakushauri endelea tena zidisha huko ' kunidharau ' Mkuu. Ningekuwa nadharauliwa na Mwenyezi Mungu ningelia na kuogopa lakini kumbe nadharauliwa na ' Kibushuti ' Wewe wala sina hofu au wasiwasi.
Huyo kibushuti nahisi ni yule aliyekufyatua.
Over
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…